Najua wewe lazima utakuwa ni mfuatliaji wa matukio mbalimbali, japo sina uhakika kama lile tamko la mkuu wa Nato ulilisikia.
Mwakajana NATO walisema kuwa uwezo wa kivita wa Urusi, ulikuwa exagerated. Kumbuka Urusi walipoivamia Ukraine, na kudai ile operation itachukua siku 3, hakuna nchi yoyote iliyoipa Ukraine msaada wowote, kwa sababu nchi zote, kwa kile walichokiamini nguvu ya kijeshi ya Urusi, kisingekuwa na maana yoyote. Baada ya Ukraine kumfurusha mrusi Kyiv, na mrusi kukimbilia ile mikoa ya Mashariki, ndipo Dunia ilipoona kuwa kumve uwezo wa Urusi wa kivita ni wa kawaida sana. Nguvu pekee kubwa ya mrusi anayoitegemea nibmakombora ya nuklia, sawa na ilivyo North Korea.
Kumbuka, hata katika kipindi cha kawaida, uchumi wa Urusi ni mdogo sana. GDP yake ni ya chini kupindukia ukilinganishia na mataifa kama US, Germany, France, n.k. Uchumi wa Urusi ni mdogo kuliko wa South Korea.
Sarafu ya Urusi iliporomoka ghafla baada ya ule uvamizi kutokana na hofu. Baadaye ikaimarika kutokana na mauzo ya mafuta. Lakini mwaka huu imekuwa ikiporomoka, na haitegemewi kunyanyuka tena, labda vita ikome. Ikumbukwe kuwa sarafu ya Urusi ilipanda kutokana na kupanda sana kwa bei ya mafuta, na wakati huo huo mataifa hayo ya Magjaribi yalikuwa hayajapata mbadala wa mafuta na gas ya Urusi. Kwa sasa mataifa hayo yamepata alternative sources, na yanazaidi kufuta mahusianobya kibiashara wajati tayari kulikuwa na miundombinu iliyokuwa imejengwa toka Urusi kwenda Ulaya kwaajili ya gas na mafuta. Miundombinu hiyo haina kazi tena, na kujenga mingine kwenda mataifa kama ya China au India, siyo kazi ya muda mfupi.
Mnunuzi mkubwa wa mafuta ya Urusi ni India, lakini India imekuwa inafanya processing ya hayo mafuta kwaajili ya kutoa products mbalimbali kama vile mafuta ya jet engines, soko kuu likiwa Ulaya. Lakini sasa tayari India imekwishatangaziwa tishio kuwa kwa vile zile products zinatokana na mafuta ya Urusi, hazitaruhusiwa kuingia Ulaya. Hiyo ina maana kuna uwezekano wa India kuacha kununua mafuta toka Urusi ili kuokoa soko lake la bidhaa zitokanazo na mafuta.
Ikumbukwe pia, ndege na zana mbalimbali, vipuli vyake vilikuwa vinatoka Ulaya, na Urusi haina uwezo wa ndani. Kwa sasa Urusi inaitegemea China kuziba hilo pengo, lakini China nayo ina mapungufu mengi kwenye ubora. Makampuni yanayotengeneza bidhaa zenye ubora yaliyopo China, ni makampuni ya Ulaya yaliyowekeza China ambayo yanalazimiki ku-comply na masharti ya mataifa yao ambako ndikobyaliko makao makuubya makampuni yao.
Vijana wengi wasomi na wenye uwezo wa kifedha, wanafanya kila namna kuondoka Urusi. Na hao ndio wazalishaji na wataalam ambao wangekuwa na mchango kwa Urusi, sasa wanaondoka.
Pole sana. Lakini utegemee mabaya zaidi kadiri siku ziendavyo. Labda vita isimame. Mataifa ya Magharibi, kama alivyosema Biden, yataendelea kuisaidia Ukraine mpaka watakapohakikisha Urusi siyo tishio kwa nchi yoyote Duniani. Wanataka wammalize mrusi kiuchumi na kitekinolojia na katika nguvu za kivita. Baada ya hapo wataijenga Ukraine kama walivyofanya kwa Korea Kusini, na warusi wengi watahangaika sana kutaka kuhamia Ukraine kwa sababu huko kutakuwa na maisha bora zaidi ukilinganisha na Urusi, nchi ambayo kwa muda mrefu imeishi kwenye uchumi duni na udikteta.