Urusi yasitisha safari za ndege kati yake na Tanzania

Urusi yasitisha safari za ndege kati yake na Tanzania

Urusi ndio nchi ilikuwa inajaza raia wake pale Zanzibar tangu corona ianze. Hapa naona uwanja wa ndege Zenji unaenda kupungua sana shughuli zake na wageni watapungua mno.
 
Na hii ni mfano wa ile 666 ambayo wanasema huwezi kuuza wala kununua kama hauna chapa, alama au utambulisho.
Aahh wapi. Mimi sielewi kwanini chanjo ya corona imekuwa nongwa... chanjo zipo kibao tanzania na watu wanachanjwa bila kelele.

Mbona chanjo ya manjano yenyewe haina kelele? Na yenyewe bila kuwa na yellow card nchi nyingi huwezi kwenda..lakini haina kelele za 666. Ila kwa corona watu wamevimba.

Mimi nadhani serikali ilete hizo chanjo lakini isilazimishe watu kuchanjwa..ifanywe jambo la hiari kama ilivyo kwa chanjo zingine..kila mmoja ajiamulie kama anataka kuchanjwa au la.
 
Pigo kubwa kwa sekta ya utalii, mahoteli kwa Zanzibar yetu.

Muda wa kuchukua likizo mpaka Julai tuombee warudi tena hawa watalii toka Poland, Ukraine, Russia maana walitoa mchango mkubwa sekta hii muhimu kwa Zanzibar.
 
Elimu elimu elimu

Ungeweka pointi bila kunipaparikia ungepungukiwa na nini. Kisebengo na hidemsede
Kwakweli elimu..elimu..elimu.

1. Mimi sio mzanzibari...ila natambua athari ya huu uamuzi kwa zanzibar.

2. Inakua vipi usifahamu kwamba usafiri wa anga ni jambo la muungano? Russia wakisema wanazuia ndege kuja tanzania inamaana zanzibar hazitaenda.
 
Chanjo lazma itakuja tu. Itakuwa kama homa ya manjano..bila kuchanjwa husafiri
Homa ya manjano unachanjwa? Utofauti ni kuwa homa ya manjano ukipima ukakutwa hauna unapewa certificate.
Ila corona uwe nayo Usiwe nayo unapigwa chanjo
 
Kwahiyo wamesitisha kwa ajili ya Corona? Mama atuharakishie Chanjo ya Pfizer.
Chanjo hatutaki. Na kama ikija iwe kama dawa za malaria tu. Ukitaka ukanunue. Sisi wengine hata hapo Nairobi hatujawahi kufika. Chanjo ya nini? Tumeshajizoelea kuishi Na corona Sisi! !
 
Mzee wa busara ushapata lift mxiiiewww
Wanajamvi habari ya muda huu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu naomba kwa mtu anaeenda Arusha kutokea Dar na gari binafsi siku ya tarehe 24/12/2020 anipe lift, tutachangia wese kidogo. Kama yupo tafadhali sana aje chemba tuyajenge chap.

Huwaga kuna busara kubwa sana mtu unapokaa kimya ili uendelee kupata maarifa. Hakuna sababu ya kuchangia jambo usilolijua.
 
Kusema kweli mimi sijaiona ndege ya urusi ikija tanzania,
Kuna ndege za 'charter' kama 3 au 4 zilikuwa zikitua Zanzibar kutoka Urusi moja kwa moja na nyingine 2 kutoka Ukraine tangu mwezi wa 10 mwaka jana.

Na kama wanavyosema wengi humu, ni kweli utalii wa Tanzania utapata athari kdg kwa kipindi chote ambacho ndege hizo zitakuwa hazifanyi safari zake nchini, sababu zaidi ya 80% ya watalii waliokuwa wanaingia nchini tangu mwezi wa 10 mwaka jana ni kutoka eneo hilo, na imesaidia kwa kiasi kikubwa mno kutatua mdororo wa kipato kwa watu wa sekta hiyo.

Ingawa athari haitokuwa kubwa sana, sababu ndege hizi zimesitishwa kipindi cha 'low season' ambayo kila mwaka kuanza mwezi wa April mpk mwezi May mwishoni.
 
Back
Top Bottom