Urusi yaunda jeshi baada ya kuazimia kukalia moja kwa moja mikoa ya Ukraine iliyoiteka

Baada ya kupata kipigo kizito kwenye uwanja wa vita Sasa wameamua kujificha kwenye kichaka Cha referendum
Referendum ni mbinu ya kupata wapiganaji ila mwamba nguvu zimeisha mimi pia nililua namwamini sana ila katutia aibu bora asingepigana hao Ukraine kwao pana vita wengine walikua DRC Kongo wametoka wiki iliyopita kama wanajeshi 250 inaonekana Ukraine ni mabingwa wa vita vya ardhini na hapo Urusi anapigwa maeneo aliyovamia na kuonekana kushindwa angekua anapigwa kwake nae ingekua habari ingine..
 
Limeshindwa jeshi, ndo mgambo wataweza?.

Putin anapeleka raia wake kuuliwa bila sababu!
Kama raia wanauliwa mbona bado anayakalia maeneo aliyoyachukua?? Na je mlipotuambia Russia wamefurushwa Kherson mbona nao wanapiga kura? Je wanapiga kura wakiwa chini ya Ukraine? 😄😄😄😄 fungua macho na akili wewe
 
Sio watu wanazolewa mitaani, ni wale wapigani wa hayo maeneo wanaopambana kujitenga na UKRAINE. Taarifa imeeleweka ila ww unahisi wanakuja kwenu hapo Mbalizi wanakuchukua ukapigane tu.
 
Mikwara mbuzi
 
mzee ameangukia pua hili halipingiki kukusanya raiya mitaani wakalinde maeneo waliyoteka nyara ni ishara ya kuangikia mdomo kama wanajeshi walio na mafunzo hawakuwa na morali vipi kwa raiya ...
 
Umesema Ukraine "wasiyachukue"?? Hata wasiposhawishiwa bado Ukraine hawana uwezo wa kuyarudisha maana hawakugawiwa waliyachukua kwa nguvu na watatumia nguvu kuyalinda
Urusi kashindwa Vita ana siraha za zamani tuu na pia hana nguvu kazi ndio maana anaomba msaada China na India nimesikia Turkey nae anataka kujiunga ila juzi tuu hapa alipata msaada Nchi yao ilipopata matatizo ya Uchumi..
 
Kweli kabisa, huwezi kufanikiwa kwa kuvamia ardhi ya mwenzio

Urusi anajaribu kushindana na nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…