US kashambulia hewa Iran ilihamisha Kila kitu kwenye vinu vya nuclear vilivyopigwa

We uoni Iran kuruhusu kushambuliwa ni udhaifu?
Kama watu wameweza kumshambulia bila kizuizi, basi hata Kama kweli anehamisha hiyo mitambo nayo itashambuliwa tu wakati ukifika.
Tatizo ni kwamba Iran anaingilika hadi chumbani bila vipingamizi.
 
Exactly!

Na sasa hivi sababu zote wanazo, nia wanayo, na uwezo wanao.

Si unaona kule Korea Kiduku huwa hawamsumbui?

Hayo mabomu yanaleta heshima.
Ukiwa nayo unakuwa unatembea na kitufe mkononi wakikutibua tu unabonyeza.

Yanaleta heshima sana.

Kiduku wana mlia timing iko siku naye ataamka akute maandaki ya mabomu (silos) yamejaa maji.
 
Wangehamisha vitu nyeti Mossad wangejua na wangevifuata huko huko vilikofichwa na kuvikung'uta. Mossad wanawadabua majenerali wakiwa makwao wanakoga kweli washindwe kujua mamitambo makubwa na delicate instruments vilikohamishiwa?😳
 
Ni sawa na kusema tunahamisha bwawa la umeme la Julius Nyerere na mitambo yake ili lisishambuliwe, nuclear project sio magunia ya mchele unayoweza kuyahamisha
Walihamisha vitu muhimu tuu kama zile kg 400 zilizorutibishwa, halafu technology ya Iran si sawa na kizimkazi, hili shambulio liko kimchongo ni Kama kuombea ceasefire tu mbona hamna Hata radiations katka, picha zennyewe hamna yaan sijapaelewa hapa
 
Una PhD ya kutokukubali jambo kirahisi πŸ˜†πŸ˜†(kwa kimo lazima utakuwa mfupi Tu)
 
Hongera Kwa kujua haya ambayo hata CIA, MOSSAD na mashirika mengine na mataifa hayajui. Ila wewe ulienda chuo kikuu cha,UMEJUA. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ HONGERA SANA GENIUS πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Watajulikana tu na kipigo kitawajia haraka kuliko mwanzo pia
 
Kwamba vinu na mitambo ya nyuklia inabebwa na kuhamishwa kwa kichwa.

Kubalini tu Iran ni simba wa makaratasi na kwa sasa hakuna mwarabu au muajemi wa kumshinda mzungu.

Tiini wenye nguvu zaidi yenu na maisha mengine yaendelee humu duniani.
Ni sawa na kusema tunahamisha bwawa la umeme la Julius Nyerere na mitambo yake ili lisishambuliwe, nuclear project sio magunia ya mchele unayoweza kuyahamisha

Inawezekana mnajua kuliko huyu!?



Yeye amesema hivi πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

View: https://x.com/RealScottRitter/status/1936606094870094332
 
Hongera Kwa kujua haya ambayo hata CIA, MOSSAD na mashirika mengine na mataifa hayajui. Ila wewe ulienda chuo kikuu cha,UMEJUA. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ HONGERA SANA GENIUS πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mimi na kuhakishia sio kila kitu mumsikie US na Israel sa we unaye jaribu kujifanya smart, hebu nipe wapi kuna Nuclear duniani ikapigwe isidhuru watu
 
Wao walisema hata wakilipua watatengeneza tena, wakisaign mkataba utawanyima uhuru wa kutengeneza nuclear.

KUlipua sio shida wanasema as long as wanayo knowledge wata rebuld tena this time haraka kuliko mwanzo.
Wanarebuild halafu hawaitumii
 
Unadhani mitambo ya kutengeneza nyuklia ni sawa na machine ya kutengeneza juice?
 
Mkuu tupo 61M na ZAIDI hapa Bongo

Lkn jiulize tuna Nyani Ngabu wangapi wenye sifa kama zako?

Tukikupoteza wewe hatuwezi kupata Nyani Ngabu mwingine kiurahisi ingawa tupo 61m+
Unfortunately, mimi sifikirii kama wewe.

Unapo embark kwenye project kubwa kama hizo ni lazima uwe na mipango inayo anticipate scenarios mbalimbali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…