Bw.
Proved
Athari ya mionzi huwezi kuificha, na ni kwa sababu kuna CTBTO (Comprehensive Nuclear-Test-Ban Treaty Organization).
Hili shirika kazi yake kuu ni kuweka na kuendesha mfumo wa kimataifa wa ufuatiliaji wa majanga ya nuclear duniani kote.
Aidha, huwezi kuficha athari za mionzi kwa sababu mionzi huenea kupitia hewa, maji na udongo. Na mionzi ina tabia ya kusafiri. Ukiacha hilo shirika hapo juu la kimataifa halikadhalika kuna maelfu ya vituo huru vya kuichunguza dunia. Kwa msingi huo, huwezi kuficha taarifa ama athari za mionzi nchini mwako.
Laiti kama ingelikuwa hivyo vituo vilivyolipuliwa na lengo lingefanikiwa na kwa asilimia ya urutubishaji ambayo Iran imeifikia, mpaka muda huu tungelikuwa tunajadili athari za majanga ya hiyo mionzi na tusingelikuwa tunajadili kama lengo la US la ulipuaji limefanikiwa ama laa!