Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 7,091
- 15,519
Lugha ambayo alikuwa anamaanisha huyo mchangiaji ni kuwa: Enriched uranium inaweza kuhamishwa. Yaani Uranium iliyoboreshwa ambayo inaweza kuhamishwa kupelekwa kwenye mitambo ya nuclear kwa matumizi au kuhifadhiwa.Hayo mimi sijui ila Ugomvi wangu na jamaa yako ilikuwa ni pale aliposema mitambo ya nyuklia ilikuwa imeshahamishwa. Kati ya watu hapa JF niliokuwa nawaamini ni pamoja na yeye.
An intelligent person huwa haongelei vitu asivyovijua. Ila anatafuta kuvifahamu kwa kusoma au kuuliza.
Halikadhalika, kwa vifaa navyo vinaweza kuhamishwa kama hiyo mitambo.
Kama unavyofahamu haya mataifa makubwa yana kawaida ya ku share taarifa za kijasusi, au kwa namna yoyote vile Iran inaweza kujiongeza na kuhamisha hiyo uranium iliyoboreshwa.
Ndiyo maana mpaka muda huu hakuna taarifa za wazi zilizothibitika kuonyesha kuvuja kwa mionzi ya nuclear. Hii inatuambia nini?
Logically, ni mambo mawili! Imma, Iran ilihamisha uranium ambayo imekwisha rutubishwa, yaani; iliyokwisha ku-enrichiwa, siyo mitambo yenyewe ya enrichment.
Au, mitambo yao ipo chini zaidi (mita kadhaa kwenda chini) kuliko nguvu ya uharibifu wa bomu lenyewe.