US yazionya nchi za Afrika kutonunua nafaka kutoka Urusi

Kwahyo USA ndo wame attach ushahidi wa huo wizi wa ngano? Hivi seriously unahitaji ushahidi wa jinsi waafrika wanavyopigwa kwenye resources zao?
Unabishana na mtoto....uelewa bado mdogo.
Mwache aendelee kusoma akikomaa atajua kwamba alikuwa hajui.
 
Wao kama nani na kwa mamlaka gani waliyonayo.

Wao mbona wakienda kuipiga Iraq,Iran na Palestine sisi hatutoi matamko.
 

Na Raisi wetu humwambii kitu kuhusu Marekani
 
Yet, kuna wanasiasa wa Afrika wasiotathmini sawa sawa trends (mitindo? mwelekeo?) hapa duniani. Wao ikitajwa Marekani tu wanajiharishia surualini na wanataka kufanya kila amri. Maskini hawajui nchi hiyo inaelekea kukosa taji la kuwa nchi tajiri zaidi na yenye nguvu zaidi duniani, na kuelekea kwenye dimbwi la nchi za Ulimwengu wa tatu! In fact, maeneo kadhaa ya Marekani ni third world.
Nchi ambayo export yake ni silaha na kuchapisha dola. Hata ufundi wa kuunda ndege inanyang'anywa katika miaka si zaidi ya kumi. Pia semi-conductors, Mchina yupo kooni kabisaaa.
Usinifahamu vibaya. Ningependa sana Marekani iwe ndiyo inayoongoza dunia, kuliko Urusi, China na hata India. Marekani ina watu wazuri sana, waelimika, wenye dini (kwa maana tabia zlizo karibu na zile zilizohimizwa na dini). Lakini, hell, sijui viongozi wao wanawatoa wapi. Kila mmoja wao yuko busy kuifukarisha nchi yake hadi kipindi chake kimalizike achukue mwingine!
 
Hivi Hawa wapumbavu wanaona jinsi wananchi wa somalia wanavyo pata tabu kifo na njaaa
 
Marekani ni wowowo ya dunia

By the way tuwaache tu ndio kimbilio la viongozi wetu kuombea vijihela... Hiyo vijihela "kwa sauti ya sa 100
 
Kutaifisha(Confiscate) ni tofauti na wizi kwani kutaifisha inakuja pale ambapo Taratibu zilizowekwa (kwa makubaliano) hazijafuatwa.e.g. Meli ya mafuta yoyote hairuhusiwi kupita hapa; mara paap!Wewe Iran kinyemela unapitisha waki ikamata watahamua watakavyotaka wakamataji. Lakini wizi ni Uporaji , kuchukua kitu cha mwenzio bila ridhaa yake na kwa kutumia nguvu na pengine kukuua ww mwenye mali.
Tunawasakama sana Wamagharibi ila tunashindwa kujiona ni Sisi wenyewe tunakulana.
Dulma ni dhulma tu iwe imefanywa na West au East; Haikubaliki.
 
Mkuu nikuulize swali. Fedha Urusi zilizokuwa bank ya marekani amezichukua, je huo tunaiita ni nini? Au mtu kuchukua mali yako kwa nguvu unaiita ni nini?
 
Mkuu tofauti hapo ni tafsiri tu na si kingine?
 
Mkuu nikuulize swali. Fedha Urusi zilizokuwa bank ya marekani amezichukua, je huo tunaiita ni nini? Au mtu kuchukua mali yako kwa nguvu unaiita ni nini?
Huyu hatakuelewa hata kidogo kaamua kuziba masikio
 
Mkuu unaandika haya ukiwa bar gani? (Samahani lakini)

Wakati Marekani anaivamia Iraq, Afghanistan, na mataifa kadhaa ya kiarabu na kuua maelfu ya raia wasiokua na hatia wanawake na watoto huku ndege zao zikihusika moja kwa moja kubeba mamilioni ya pipa za mafuta ghafi walikua sahihi?

Wameungana na washirka wao kumuondoa Gadafi na kumuua kokatili nani aliwanyooshea kidole?

Marekani anamsapoti Israel kuua mamia ya wapalestine kila wiki halafu sisi tuendelee kutumia mitambo yake ya kufua umeme ya songas pale ubungo kwa kia yeye ni nani?

Kwa haya yote marekani kapata wapi ukiranja wa kutuambia waafrika hiki tufanye na kile tusifanye....kwa kua anatupenda sana?

Hii dunia haiko fare..pengine ile hukumu ya "HAKI" atakayoitoa Mungu kwa walmwengu wote siku ya siku ndiyo itakayo tafsiri kila kinachotendeka sasa hivi na kila mtu atapata ujira wake.......

Ee mola tujaalie tupokee kitabu chetu kwa mkono wa kuloa siku hiyo Aamin!
 

Wajinga sana US, wao wameiba hela za Libya, Afghanistan tena wanatangaza eti wametaifisha mali za nchi nyingine hadharani. Wamenyakua mali za wafanyabiashara wa kurusi kisa ni marafiki wa Putin au wanahusiwa kuwa marafiki ila ni haki.

Ujinga wa Marekani hauvumiliki tena duniani.
 
Because we are spoon feed.
 
Kama Urusi ni wezi basi wanaiba kwa ajili ya Africa, ni wiki moja tu imepita tangu kiongozi mkuu wa (AU)kusafiri Hadi Urusi na kumuomba Rais Purtin alifikirie bara la Africa.
"Za kuambiwa changanya na zako"
 
Watatupa wao au? Waache ujinga wao mara moja!
Wao chakutupa hawana, walichotaka kuona ni Mwenyekiti wa AU Mack Sally, angeenda kwao (Marekani) kuomba hicho alichokwenda kukiomba Urusi, Cha Ajabu wao wenyewe bado wanaendelea kulialia kwa Urusi kwa shida hiyohiyo!
 
Mkuu nikuulize swali. Fedha Urusi zilizokuwa bank ya marekani amezichukua, je huo tunaiita ni nini? Au mtu kuchukua mali yako kwa nguvu unaiita ni nini?
Asikuhadae mtu wala kupindisha maneno. Fedha ya Mrusi iliyoko Benki za Marekani na kwingineko bado ni za Mrusi. Kilichofanyika ni Uzuiaji/Usitishaki wa matumizi ya Akaunti hizo. Labda nitumie mfano hai (Ila naomba msamaha kwa wahusika) Mh. Mbowe a/c zake zilizuiliwa i.e. Hawezi kutoa wala kuweka fedha lakini Fedha iliyokuwepo ni ya kwake na imekuwepo hadi Zuio lilipoondolewa juzi i.e. sasa anaweza kufanya miamala kwa kutumia A/C zake. Na kimataifa ni hivyo hivyo. Baada ya hii vita, na vikwazo vikiondolewa Mrusi (kwa Ufasaha zaidi Watu wa Urusi) wenye A/C kwenye mabenki ya Marekani zilizokumbwa na zuio zitafunguliwa na maisha yataendelea.
Mikataba ya Kilaghai ni wizi tu unaohalalishwa na wakubwa
Ndio nakubali na ni Wakubwa wetu sisi ambao sisi wenyewe ndo tumewapa dhamana. Wametugeuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…