US yazionya nchi za Afrika kutonunua nafaka kutoka Urusi

Tanzania hatuwezi kufa hatuna njaa na hatushoboki kwa Russia
Wewe unaongea mambo usiyo yajua kishabiki kama siasa za CCM.

Mwaka huu 2022 kuna njaa kali sana inakuja Tanzania. Mavuno ya mazao ya chakula yalikuwa duni sana sababu ya hali ya hewa na bei kubwa za mbolea au ukosefu kabisa wa mbolea nchini kipindi cha kilimo.

Save this comment and come back here December 2022 up to February 2023.
 
Nashukuru jinsi unavyouchukia udhalimu. Mimi ninaandika pia kwa machungu ya kuuchukia udhalimu. Lakini kosa moja halihalalishi kosa jingine.
US kavamia, kaua na Kuunga mkono Israeli kuua Wapalestina kama ulivyoandika hapo juu na nakubali hilo SIO HALALI na pia Tukubali kwamba kumwuunga mkono Mrusi aliyevamia,kuua, kuunga mkono makundi ya wapiganaji dhidi ya Taifa la Ukraine, na kupora Nafaka katika Maghala (Hifadhi za Taifa) SIO HALALI.
Ukiranja wa Marekani mm siujui sawasawa kivile, nnachojua ni kwamba ni mbabe na mpenda vita.
Mimi nafikiri Tusiangalie kauli katoa nani bali tuangalie Mantiki na Uzito wa hiyo kauli.
 
Walete wao.
 
Acha kukariri ,licha ya mavuno duni,kilichopungua ni kiwango cha ziada ila hakuna upungufu wala njaa..

Na usikariri kwamba chakula ni mahindi na mpunga tuu na kuthibisha hilo Serikali imesema kamwe haizuii mipaka kwa hiyo watakaoamua kuuza wauze..👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220606-214800.png
    89.4 KB · Views: 10
Sawa mkuu
 
Wasituweke kati bwana...
Wazungu wanatuona waafrika kama vile ni wake zao, wanataka kutupangia mpaka bikini za kuvaa.
Ila kwa kua waafrika wenyewe tumekubali inabidi tuvae tu hizo bikini za nyota na mistari mistari ili bwana wetu asitukasirikie.
 
Hapa duniani kuna nchi nyingi za kijinga na kipuuzi! Ila Marekani na Israel naona zimepitiliza aisee.
Uko sawa; lakini wanapaswa wajue kwamba nyakati hubadilika; hawawezi kuwa walivyo siku zote, mambo yanaenda yakibadilika.
Zile amri za kiimla za wamarekani ambazo zilikuwa hazibishiwi enzi hizo, sasa zinajibiwa kwa namna mbalimbali; hata kwa kuviziwa kama walivyoviziwa na Osama na kuumizwa vibaya japo wanadai wamemuua.
Nchi zingine kama Korea Kaskazini na Iran, zamani zilikuwa zinaufyata; lakini siku hizi zinaweza kujibizana na U.S; hata kama hazijawahi kumpiga, lakini ana hofu nazo kwa sababu anajua kwamba zina teknolojia ya kivita (nuclear) ambayo inaweza kupiga ndani ya U.S; hata kama ana mifumo ya kukinga mashambulizi hayo, lakini hathubutu ku-risk kuruhusu mashambulizi hayo yafanyike, maana hana uhakika nini kitatokea!!
U.S ataendele kutupelekesha sisi waafrika na nchi zingine duniani ambazo hazina teknolojia ya nuclear.
Tutaendelea kudeki barabara zetu anapokuja Rais wa U.S kama ilivyofanyika kwa Obama na Bush Jr; lakini siyo kwa Russia, Iran, Korea Kaskazini na China.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…