USA hata kama akasimama pekeake dhidi ya dunia nzima kivita, bado tutapigwa tu

Mwandishi wa Newsweek Magazine la Marekani aitwaye Fareed Zakaria aliwahi kusema kwamba Marekani ana uwezo wa kupigana na nchi zote za Ulaya zikija pamoja na Marekani ikashinda. Pia akaongeza kwamba Marekani can fight in five different fronts and win!
 
Unauliza maswali ya miaka 250 halafu unajijibu kwa majibu ya miaka 50.
Empires/Superpowers zote kubwa duniani huwa zinatawala kwa kushirikiana na vassal states na kupitia alliances. Mataifa madogo ndio huwa yanapigana vita peke yake. Wamarekani hawapendi kabisa watu wao wafe vitani hata kama watashinda hivyo vita.
 
Kwenye masuala ya kijeshi makosa ya zamani huwa yanatumika kama reference hadi leo. Ndio Black Hawk down iliwafundisha wa Marekani na majeshi yote duniani kuwa mashambulizi ya juu ya helcopter mara zote yanabidi yasaidiwe na wanajeshi walioko chini hasa kwenye rescue mission.
Na ndio wanakufa hivyo, wamekufa Vietnam, wamekufa Iraq na wamekufa Afghanistan na kwa kujua hilo ndio maana hajajiingiza less pale Syria maana anajua kama taliban tu walimsumbua Mrusi atawafanyaje
 
Bajeti ya ulinzi ya Marekani ni dola bilion 820, hizi sio stori za vijiwe vya kahawa, ni real business.
 
Kwanza hakuna vita ya vietnam na USA ila nachojua kuna vita kati ya south vietnam vs North vietnam huku USA na China Kama belligerent states tu. Kwanza nisijekuwa najichosha bure ulishawahi kufuatilia chanzo chake? Na iliishaje ishaje
Ona takwimu, yani zaidi ya watu wake milion 3 walihusika katika vita hiyo halafu useme kwamba US hakupigana kwenye hivyo vita.
 
Vita vya Vietnam hawakushindwa, waliamua kuachana na vita kwa sababu za kisiasa, halafu Marekani ya miaka ya 70 ni tofauti sana na hii ya leo.
Marekani haikushindwa Afghanistan, waliamua kuondoka baada ya kuikalia hiyo nchi kwa miaka 20 huku wakiona hakuna hamasa ya WaAfghanistan wenyewe wa kawaida kujipambania na kuondokana na Taliban.
Somali ilikuwa special military operation ya masaa machache, haikuwa vita. Kwenye SMO ya kumnyakua hata gaidi mdogo kwenye nchi dhaifu ni suala la ujasusi na intelejensia zaidi kuliko nguvu za kijeshi, na kosa dogo linaweza kuharibu mission nzima.
 
Tufanye hivi umeshinda πŸ˜†πŸ™Œ
Basi sawa Russia ndo taifa pekee lenye operations NYINGI zaidi za kijeshi duniani na zote succesfully halafu ni kidume anapigana peke yake bila allies wala misaada
 
Bila shaka mtoa mada ni mpenzi wa movie kama ''without remorse'' nk....zile movie hua zinaonyesha nguvu ya marekani kijeshi lakini sio uhalisia....
hata Russia ni vile tu muvi zinashangaza.....
kwenye mada yako marekani akiamua kupigana na kila nchi bas wale majirani tu kina cuba,mekiko watammaliza...huku wnangu urusi wakiuwa na missile za masafa marefu
(of coz hyo vita haiwez kutokea)
tunasema haiwez kutokea sababu wenzetu(wazungu) wanatumia akili sana kuchambua hatari ya jambo so vita kama unayoizungumzia mtoa mada ni vita yenye hasara kubwa kuliko faida baada ya vita
 
Ona takwimu, yani zaidi ya watu wake milion 3 walihusika katika vita hiyo halafu useme kwamba US hakupigana kwenye hivyo vita.
View attachment 3010835
Umeelewa nilichosema? Au unadandia tren kwa mbele? Nimesema officialy hii ilikuwa ni north vietnam vs south vietnam, Russia, China na USA ni washirika ila uhusika wa Usa ndo ulivuta watu kufuatilia vita hiyo unajua kwa nini? ni nchi inayoogopwa

Kuhusu kushindwa au kusitisha vita hivyo ni jambo lingine maana kuna mengi nyuma ya pazia.
Ndiyo maana wanasiasa wa marekani wengi iliwagharimu vibaya pale walipotaka kujitoa mpaka pale umma ulipoanza kupiga kelele.
 
Utoto raha Sana
 
Kuna watu hapa walifikia hatua ya kusema Iran anaweza kumpiga USA, mimi nawashangaaga sana sijuwi wanawazaga nini
Kuna mwamba mwingine akatwambia China ana Teknolojia kubwa kuliko USA, shida watu wanaongozwa kwa hisia wanashindwa kuona ukweli..
 
Sasa ndipo hapo mjue, kama South ilisaidiwa na nchi tatu na bado US akashindwa na hizo nchi tatu zilizomsaidia North hadi akatoa majeshi yake, ndipo sasa aweze pigana na dunia nzima ashinde.
Mind you wakati huo alikuwa ana teknolojia kubwa ambazo nchi nyingine hawakuwa nazo kwa wakati huo kitu ambacho ni tofauti kwa sasa.
Mfano wakati wa vita vya Iraq watu walikuwa wanashangaa drones ambazo zinakuwa operated kwenye military base remotely, now hata turkey anayazalisha tu na kuyauza.
 
Huyu anaweza akasema kwamba mfano jeshi la Tanzania linaweza kupambana na raia wote na wakashinda kisa wana silaha, kumbe haoni huu wingi unaweza ukakushinda hata kma hawana silaha
 
US hakushindwa vita katika uwanja wa vita bali aliamua kuachana na hivyo vita baada ya upinzani mkali wa hivyo vita nyumbani kutoka kwa raia ambao walikuwa hawaoni maslahi yoyote kwao kuongezeka.
 
Kwa mfano angetumia nukes? Hapo ungesemaje angeshindwa tena? Kwa hiyo si kweli kwamba alitumia uwezo wake wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…