FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Machafuko ya Mashariki ya kati hivi sasa ni mchezo uliopangwa na nchi za Magharibi, hususan USA UK na NATO yote wakishirikiana na vibaraka wao. Ikumbukwe, Israel ni base tu ya Mmarekani.
Haitakiwi kabisa mashariki ya kati machafuko yaishe kwa sasa.
Wakitoka Mashariki ya Kati wanaunganisha Afrika Magharibi ya kati na hatimae kwetu huku.
Bila kufanya hivyo kibabe, uchumi wa Magharibi utaanguka vibaya sana.
Vyanzo vikuu vya uchumi sasa hivi vinahodhiwa Mashariki ya Kati na Afrika. Nchi za magharibi hazitokubali kabisa nchi źa mashariki, hususan Russia na China kuhodhi na kuwa na kauli kwa mali asili zote hizo.
Kwa sasa ni lazima Saudi Arabia iingizwe kwenye machafuko ikitaka isitake. Sababu ni nyingi mno, zikiwemo za kiuchumi na siasa za Kijiografia (geo politics).
Ikumbukwe, Saudi Arabia na nchi za Kiarabu za Gulf (GCC) ni ng'ombe wa maziwa wa Mmarekani, sasa ng'ombe kaonekana analizowea zizi la jirani kwa kasi kubwa sana, ni lazima adhibitiwe.
Kama hiyo haitoshi, Biden ni lazima amtie adabu MBS kwa jeuri anazomfanyia mara kwa mara. Kwa ushahidi kabisa.
Mrusi nae anawekwa bize na Ukraine ili azma yao kwanza itimie huku, huku kwa sasa kuna faida zaidi kuliko Ukraine.
Sisi huku ni lazima tuzicheze karata zetu vizuri, tusijiingize kwenye mtego wa panya.