US aliiwekea USSR ukaguzi pale Cuba. Unajua maana ya naval kuwekwa karantini ni dharau iliyoje superpower USSR kuwekewa na kupewa masharti kwamba hapa hufanyi hiki na hapa hupeleki silaha bali utazitoa.
Meli za Marekani zilizuia za USSR, zikakagua kama kuna silaha hakuna kwenda na kama hakuna silaha basi ruksa. Marekani ilitaka kuishambulia Cuba pamoja na uwepo wa majeshi ya USSR. Ndipo USSR ikakubali kutoa silaha zao pale.
Hapo unasemaje Marekani alilialia? Badala yake USSR ndio ililialia kama inatoa silaha Cuba basi na Marekani itoe makombora Uturuki ili angalau serikali ya Soviet ipate pa kuficha uso wake isionekane imenyanyaswa. Na Marekani ni wanadiplomasia, wakakubali.