USA wako serious sana. Uchumi wao ni mkubwa sana 30 trillion USD

Ndio maana nimesema kuwa hakuna uhusiano wa maendeleo ya nchi na mfumo unao tumika kuongoza nchi.

Mfano kuna nchi nyingi tu ambazo mifumo ya uongozi wake ni kama wa nchi yetu lakini zina maendeleo wakati sisi ni masikini wa kutupwa.
Nchi gani ina mfumo wa uongozi kama wa kwetu ambayo ina maendeleo makubwa??
 
Uongo mkubwa. Marekani haizalishi??
Hata mimi nimewaza hilo,ivi wanapo sema G7 USA ikiwemo ni nchi zenye viwanda na uchumi mkubwa duniani Ina maana wanatudanganya sio!!?? Labda itakuwa inazalisha mazombi yale tunayo yaona kwenye muvi na zombi mmoja ndio huyo jamaa kajipinda mwenyewe mchumi kipindupindu kuongelea uchumi kama anajua vile kumbe ni mwendo wa kuarisha tu praaaaa praaaaa paaaaaaaa!!!!!!!!
 
Nchi gani ina mfumo wa uongozi kama wa kwetu ambayo ina maendeleo makubwa??
Uturuki ,hata Ufaransa ukiangalia mgawanyo wa Madaraka ni kama wa Tz.
 
Hisa za nini? Za hewa? Sio za za makampuni na viwanda??
Coca-Cola, adidas, iPhone, dell, Pfizer n.k wakiuza hisa sio viwanda vimeuza hisa??
Umemuuliza vzr. Hizo hisa za hewa..? Kama sio makampuni makubwa saana imagine kampuni kama apple ambayo ni kubwa sana njoo kule boeing nk makampuni/viwanda vikubwa vipo US aaache upuuzi wake. Eti Us haina viwanda 😂😂😂😂 eti haizalishi. Hizo boeing, iphone nk ni mawe yakuokota ty ama
 
Sisi ndio wazaramo. Hata kama suruali langu limetoboka ukinunua gari langi sijapenda lazima nikuseme.
Povu siruhusu
 
Umechanganya mambo.
 
Unafikiri Usipo fanya kaz unaweza ishi USA? Yasni ile fomul asiefanya kaz asile 🇺🇸 nimpaka maladhi.....
Ni nchi gani nyingine ambayo utaishi bila kufanya kazi?
 
Uturuki ,hata Ufaransa ukiangalia mgawanyo wa Madaraka ni kama wa Tz.
Hujui, Mikoa ya Ufaransa wakuu wake ni marais wa Halmashauri za mikoa(President of the regional Council), wanachaguliwa na halimashauri za mikoa zenye wajumbe waliochaguliwa na raia, Rais wa Ufaransa anateua waziri mkuu lakini hawezi kumfukuza, Rais wa Ufaransa anawajibika kufuata ushauri wa baraza la mawaziri na maamuzi ya Rais lazima yasainiwe na waziri mkuu pia. Ufaransa haina makamu wa Rais, pia rais wa Ufaransa anashitakiwa na kuna rais mstaafu mmoja alifungwa kwa makosa ya rushwa miaka ya karibuni.

Uturuki kabla ya 2007 bunge ndilo lilikuwa linachagua Rais, kabla ya mabadiliko ya katiba 2017 rais aliyekuwa anachaguliwa alitakiwa aachane kujihusisha na siasa za aina yoyote za chama chake, magavana wa mikoa hawaruhusiwi kisheria kuwa wafuasi wa chama chochote cha siasa, mkuu wa usalama wa mkoa ni naibu gavana ambaye ni mkuu wa police wa mkoa. Idadi ya majaji uturuki imewekwa katika katiba, nusu ya majaji wanachaguliwa na bunge na nusu iliyobaki inachaguliwa na serikali, ili mtu achaguliwe kuwa jaji lazima afanye mtihani wa ujaji na afaulu na asome miaka miwili jinsi ya kuwa jaji katika shule maalumu ya ujaji. Wana baraza la majaji ambalo ni huru kutoka serikali. Mawaziri sio sehemu ya bunge.
 
Usilete ubishi GDP ya Marekani ukuaji wake kwa kiasi kikubwa unategemea hisa na masoko ya kifedha na sio viwanda kama China , Ujerumani au Japan
Uchumi unaotegemea kilimo na viwanda ni uchumi ambao haujaendelea. Nchi nyingi maskini hutegemea kilimo, halafu viwanda then finance.
Ni sawa na mkulima na mfanyakazi wa kiwandani vs. mfanyakazi wa Benki kuuu, tra etc...
Siyo sifa kutegemea kilimo na viwanda, maana yake wewe ni mlalahoi.
 
Usilete ubishi GDP ya Marekani ukuaji wake kwa kiasi kikubwa unategemea hisa na masoko ya kifedha na sio viwanda kama China , Ujerumani au Japan
Bora tu kuwa tajiri kama Switzerland, unakusanya pesa za wajinga huko duniani ambao hawaeshimu mifumo ya kibenki halafu unazikopesha tena nchi zao na raia wako wanapata mikopo bwerere.
 
Sisi ndio wazaramo. Hata kama suruali langu limetoboka ukinunua gari langi sijapenda lazima nikuseme.
Povu siruhusu

bora hata wangekuwa wanaishia kukusema tu lkn wanakucheka na kukukejeri, watu ambao hawana kitu wanamcheka mtu aliyewazidi karibia kila kitu …
 
Uchumi wa masoko ya hisa hauna tofauti na uwe na simba wa makaratasi, anaweza kuogopesha wetu kwa mbali ila akisogolewa jirani anapoteza maajabu

USA ukiondoa jeshi na sarafu yake kuwa global reserve currency uchumi wake hauna maajabu; kapoteza hadi industrial capacity ya kuzalisha silaha zoke kama vita ya pili ya dunia, na mbaya zaidi ya hapo kahamishia shughuli za uzalishaji Asia na nchi za Amerika ya kusini; misingi yote aliyotumia kujenga uchumi wake sahizi imekuwa tope
 
Kwa hiyo Uchumi wa Japan na Ujerumani haujaendelea kwa sababu ya kutegemea viwanda?
 
Bora tu kuwa tajiri kama Switzerland, unakusanya pesa za wajinga huko duniani ambao hawaeshimu mifumo ya kibenki halafu unazikopesha tena nchi zao na raia wako wanapata mikopo bwerere.
Na je hao wajinga siku wakidhibitiwa ?
 
Uongo mkubwa. Marekani haizalishi??
Huwezi kulinganisha uzalishaji wake na nchi kama China au Japan; USA ukiangalia kampuni kubwa sana zinazoingiza pato kubwa hata hazizalishi bidhaa bali huduma; fikiria kampuni kama Meta (FB, Whatsapp, instagram etc), hawa wanatengeneza pesa ndefu ila wanaajiri watu wachache
Nenda nchi zenye viwanda vingi au kilimo ndio uti wa mgongo hata utajiri uliopo nchini unaakisi asilimia kubwa maendeleo ya watu
Jiulize tajiri kama Elon Musk, yaani ndio tajiri wa kwanza duniani lakini karibia kampuni zake zote bado hazizalishi faida kujustify yeye kuwa tajiri wa kwanza duniani (utajiri wake wa $400 B upo kwenye makaratasi pamoja na imani juu yake katika soko la hisa na kukopesheka mabenki)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…