USA yaionya Afrika kuhusu Uchaguzi; We will not hesitate to consider consequences

viongozi wa afrika hawapo huru kimamlaka, wana option 2 za kuchagua either wawe kibaraka/adui wa beberu, ukiwa kibaraka tegemea kutukumika kama msaliti wa raslimali za taifa lako na ukiwa adui tegemea kuchafuliwa kwa propaganda za kila aina na migogoro isoisha, hata migogoro ya wakimbizi wao ndo huitengeza kwa maslahi yao sema vijana mnaufaham mdogo wa haya mambo japo mnayadandia kwa mbele
 
Check ulivyo zuzu, Mugabe yupo madarakani na Mseveni umewakumsikia ameenda Ulaya au Marekani? shame on you mpuuzi wewe inamaana sisi hatuelewi maana ya uhuru unaelewa wewe na bibi yako pekee?
maandishi yako hayawezi nifanya zuzu, hapo kwa mugabe ni typing error nilimkusudia kagame, kutokwenda ulaya kwa museven haimanishi hashirikiani nao, unadhani asingekua kibaraka wao wangekubali avunje katiba ili aendelee? jitahidi kujadili mambo kwa lugha za staha maana hapa tupo katika kubadilisha fikra na si kutoleana mapovu
 
Sasa kwakuwa IMF na WB ziko marekani ndo tukubali kibaraka wa wazungu lissu mbeliviji atutawale na tumpe kura za huruma?
 
Ungejua kisababishacho wakimbizi usingewalaumu hao.Watawala wa kiafrica ndio chanzo cha vurugu afrika.Shida ni kutojua namna ya kuwatumia mabeberu positive Kama walivyofanya singapore, Malaysia, south korea,Dubai,nk huwezi ukashirikiana na beberu ukawa fukara
 
TRUE
 
Ni baraka kwa Mungu kunyimwa visa ya kwenda USA lakini umezuia nchi kutumbukia kwa vibaka kina Amsterdam na wazee wa faragha.
Hata Gabgo alinyimwa visa na kisha wakamchota. Hiyo ni lugha ya kidiplomasia tuu.
 
popote uonapo mgogoro wa kisiasa na kusababisha wakimbizi ujue kiongozi aliyepo madarakani si kibaraka wao hivo wanawatumia upinzani na waasi kwa maslahi yao, ukiona kiongozi wa kiafrika anang'ang'ania madaraka na wamemuacha tu ujue ni kibaraka wao na wananufaika sana kupitia yeye, huyo ndo beberu kama ulikua humjui vizuri.

ingelikua kushirikiana na beberu huwezi kua fukara basi afrika ingekua na maendeleo zaidi maana mataifa mengi yanashirikiana na beberu, ulowataja hawajafanikiwa coz wanashirikiana na beberu la bt wamefanikiwa coz wanajua elimu ni maarifa yatokanayo na akili zetu ndo maana na wao wanavumbua na kufanya the same kama marekani
 
NEC na CCM msifikiri ni utani...hawa jamaa huwa hawataniagi!!
 
Mbona Marekani wamesema jambo jema.
Au mnataka chaguzi za nchi za Kiafrika zisiwe zinazingatia uwazi, haki na usawa ?
Na nani asipewe haki na kwanini ?
Mantiki yake ninini ?
 
Kwani anaewaambia watawala wa kiafrica waue watu,wazulumu,wawafanye waafrika wawe masikini ili wawatawale,wafiche fedha mabenk ya ulaya, wawekeze kwenye white elephant project, kujilimbikizia mali, kununua magari ya kifahari mfano ma v8 yasiyotija badala ya kuboresha maisha ya waafrika, ni mabeberu? chanzo cha Vita congo ni mobutu, Sudani Ni Bashir, afrika ya Kati, rwanda, burundi ni udini, ukabila, somalia ni siadi barrey, Ethiopia na eritrea ni mengustu mariam, libya ni Gadaffi kote huko ni watawala kutoheshimu katiba zao
 
ukitaka kuwajua vizuri mabeberu tizama walivyokua wanatoa takwimu za hovyo namna waafrika tutakavyopukutika na corona, pia jiulize kwa nini walitaka wafanyie afrika hizo chanjo za corona akati wao ndo waathirika zaidi? endelea kujifunza zaidi kuhusu mabeberu huenda siku1 ukawaelewa vizuri
 
Watanzania tunaunga mkono uamuzi wa USA, Swali letu, Jee serekali ya akina Trump na Pompeii mbona wanapinga upigaji kura wa posta kama kawaida yao kwa miaka mingi iliyopita, na Trump amejutayarisha kutokubali maotokeo iwapo atashindwa, na hataondoka WHITE HOUSE. Ikitokea hivyo Africa Inaweza wawekea sanctions, ama kuwalazimishe wafuate haki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…