Usafiri wa ndege Dar es Salaam - Mwanza kwa Tsh 120,000, unaanza Machi 13, 2023

Wako wapi kwa sasa?
Kulula alikuja kupotezwa na covid mwaka 2020 kama sikosei, Mango yeye hakudumu sana .kufilisika kupo, kama Pan am , Sabena zilifilisika hakuna jipya

Kumbuka hii ni biashara mpya huku Africa , Naamini conditions ziki settle wako watakao survive
 
Juzi nilionyesha mazingira magumu ya kuendesha airline hapa Afrika na hasa gharama kubwa za uendeshaji. Ni kwa mantiki hiyo kuwa siyo rahisi na almost impossible kwa LCC kuoperate kwenye masoko yetu. Kidogo South Africa maana ukweli ni different market lakini nako imekuwa taabu. Fastjet alikuwa anakwenda nara ngapi mwanza? Is that volume enough to sustain? Kodi alikuwa analipa tofauti na wengine? Landing, Air navigation parking, safety fees ziko kiwango gani? Je zikipunguzwa TAA na TCAA can survive? Groundhandling na inflight services ni kiasi gani? Na bei hizi ni reflection ya udogo wa soko! Ilikuwaje shareholders wa fastjet wakajitoa miaka miwili tu baada ya kuanza operations? Haya madeni waliyoacha Fastjet kwa service providers na pia status ya vitabu vyao? Ningependa kuona hata sisi tunakuwa na LCC lakini without a Dubai approach, yaani gesi na dhahabu zetu zijenge other markets, forget it. Dubai sio tu a strong airline hub ila ni one of the main logistic centre ya waundaji wakubwa wa ndege na spaceport manufacturers. Cash flow ambayo nikutokana na forward sales unayosema lazima iwe generated na wasafiri. Je hata hiyo 120 000 ni watanzania wangapi wenye uwezo huo? Inawezekana issue ikawa ni kujenga uwezo wa nchi kiuchumi ili watu wawe na purchasing power at least to middle class, in it real sense. Nina masna tunajribu kujibu swali la hesabu with a wrong approach but believing, as usual, we have the right formula kwa kusikiliza uongo wa wanasiasa ambao nao huchukua hizo information hapahapa Jamiiforums. Forward sales ni kuwa mauzo ya keshokutwa yatumike leo!
 
Maelezo mazuri sana
Lakini kama nimekusoma vizuri ukiangalia gharama ni kama vile biashara ya ndege lwa Afrika ni kichaa zaidi, kwamba Lcc nyingi kufilisika ni kwa kuwa lcc wapo genuine , transparent kweny vitabu vyao.
Ukiangalia fleets za fastjet ukalinganisha na hizi za Atcl gharama za manunuzi na uendeshaji wake , ni dhahiri Atcl itakuwa inajiendesha kwa hasara sana , ni vile tu data zipo mafichoni.
 
Hilo sina uhakika nalo maana audit principles hazina kificho na wakaguzi hawaendani na hizo siasa. Pia wao kuwa wanachama wa IATA lazima wapeleke vitabu vyao IATA ba kungekuwa na magumashi lazima ungesikia. Labda ile advantage ya umiliki wa serikali na gharama za chini za workforce! Nafikiri ATCL inaangaliwa kisiasa zaidi na wananchi bila kuangalia reality. Ukiangalia wamejitahidi kuaddress gharama mfano kufanya service ya ndege zao na kutumia marubani wazawa. Inawezekaba wamekuwa na nidhamu zaidi baada ya vurugu zilizopita. All Iin all wanaweza kufanya vizuri zaidi wakitenganishwa na siasa kwani wana advantage ya soko la ndani kubwa na uwepo wa infrastructure na location kwa soko la nje (Zanzibar na utitili wa mbuga za wanyama).
 
Ilikuwa inatisha Mkuu, maana unaona kabisa ndege inavyosongwa na upepo mkali wa kule juu.

Unajikuta unakumbuka kusali hata kama hujaenda Church una miaka 3 🤪
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Sasa unasali ili nini kibadilike wakati kanisani hujui hata kama wameshabadili rangi kupaka mpya
 
Daah nouma sana karne ya 21, bado viongozi wanaamin kumiliki gari ni anasa, pumbavu kabisa
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Sasa unasali ili nini kibadilike wakati kanisani hujui hata kama wameshabadili rangi kupaka mpya
Ni ile hali ya kutapatapa kwa roho kabla haijaacha mwili

Mzee kifo kinatisha hasa unapokuwa unakiona

Saivi tunasali lakini Kiongozi 😀
 
Nimewahi kupanda mpaka Songwe Kwa elf 86......aliyeiua fast Jet alaaniwe kabisa
 
Mkuu biashara ya ndege duniani note ulaya na marekani zikiwemo bado hazina faida
 
Ni ile hali ya kutapatapa kwa roho kabla haijaacha mwili

Mzee kifo kinatisha hasa unapokuwa unakiona

Saivi tunasali lakini Kiongozi 😀
Hongera mkuu kama umeanza kusali, kuna siku mwaka jana nilienda kanisani kumbe baadhi ya sala zimebadilika, duh Mungu atuvumilie na kutusamehe. Ila usiende kusali kwa Mwamp...
 
Kwa hii point yako inaonyesha tuna viongozi wa hovyo sana yaani
 
Kwa hii point yako inaonyesha tuna viongozi wa hovyo sana yaani
Na huo Uwanja wa KIA ndege yeyote inashuka yaani tunatengeneza mazingira ya kujihujumu wenyewe harafu tunasema tunahujumiwa ukiuliza kwa nini Uwanja una makato makubwa hawana majibu Kilimanjaro Mlima upo hapo hapo tupewe nini sasa...
 
Tanzania tunajihujumu wenyewe sijui kwa nini pana sheria sijui ya wapi eti Nchi ya Afrika kusafiri mfano kwenda SA ambapo hata bus zinakwenda watu wanalazimishwa kukata ticket ya Return ila Zambia,Botswana,Malawi huwa tunakata ticket moja tuu kwa shirika hilo hilo Tanzania linalosema lazima uwe na return pana vitu wanafanya vinakera sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…