Usajili Mpya Simba SC: Umakini na utulivu wa kiwango cha juu sana unahitajika

Mikia bwana! Hivi Tshishimbi ni hitaji madhubuti kwenye timu yenu? Au mnajinasibu kuendesha timu kisasa kwa mbinu za zamani!? N way time will tell
 
Kila mmoja ana mtazamo wake lakini kwangu mimi sioni Simba kama inahitaji idadi kubwa hivyo ya wachezaji

Kwenye defence tatizo lililopo ni Umri tu na hilo litamalizwa kwa kuongeza mchezaji mzawa mmoja tu.

Katika ligi yetu Bakari Nondo Mwamnyeto atafaa lakini hana uzoefu wa kutosha sana na ni last defender sijui kama ataweza kucheza kama namba nne aliyekuwa akicheza Juuko.

Katika Ligi za Afrika Mashariki yupo Timothy Awany wa KCCA ya Uganda huyu nae ni bonge la beki na anaweza kucheza hiyo nafasi hata national team ya Uganda alicheza hivyo baada ya kuumia Juuko.

Midfield.
Kimsingi Simba hawana tatizo kubwa sana la Midfielders has DM wanaye Mkude, Fraga, Mzamiru na Shiboub hawa ni midfielders wazuri sana tatizo moja wote hawana kasi kubwa sana.

Mkude na Fraga wanacheza kama Register lakini hawana speed na siyo wanabaji wazuri kutatua tatizo lazima wacheze na mtu anayekaba sana na hapo simba yupo mmoja tu MZAMIRU YASSIN.

CM Midfield simba ndiyo kuna tatizo wachezaji wengi viwango vyao vimeshuka sana na wengi siyo clinical CM ukiondoa Chama, na Dilunga wengine viwango vyao vinaleta changamoto sana hasa kina Ndemla, Shiboub, Dilunga kunahitajika mtu anayeweza kucheza double role lakini mtu huyo tayari simba wanaye. JONAS MKUDE na SHIBOUB, MZAMIRU YASSIN hawa watu unatakiwa kubadili mfumo tu ili waweze kupata nafasi . Uchebe aliweza kuwachezesha Kotei na Mkude pamoja au Mkude na Mkude na Mzamiru pamoja mmoja anacheza kama CM akicheza double role defence and attacking.

CENTRAL ATTACKING MIDFIELD hapa ndiyo kuna utata wachezaji wote ukiondoa Chama hawafanyi vizuri wengi wa wachezaji kwenye eneo hili wanacheza vizuri wakiwa wide. Kina Kahata na Kanda ,na Miraj kama Ajib angekuwa kwenye kiwango bora basi eneo hili lingemfaa sana lakin Ajib siyo wa kutegemea sana he is so slow and predictable.

Nani Aongezwe hapa namuona Konde Boy huenda akaleta impact zaidi, japo anaweza kununuliwa ALLAN OKELLO wa KCCA ya Uganda huyu bwana mdogo ni replica ya OKWI.

ATTACKING. Hapa ndipo naona tunahitaji kasi na ubunifu mkubwa. Wachezaji tulionao wote umri umekwenda sana na siyo wabunifu sana na kibaya zaidi hawana madhara nje ya 18 Kagere hana madhara nje ya 18 Bocco nae ni hivyo hivyo hapa ndiyo mtu wa kuja kuingia kwenye kikosi moja kwa moja na awe na kasi na mwenye uwezo wa kupiga long range shot. Mtu wa aina hii sioni EA labda wamsajili Heritier Makambo ni clinical finisher na anaweza kufanya runs nzuri zitazowapa space Kagere na Bocco.

Kama atakosekana Simba kwenye kikosi chake cha vijana wa mtoto anaitwa EDWARD GERALD mrefu hivi kama Emanuel Gabriel anaweza kupewa nafasi the dude is good ila hajapewa nafasi tu.


Wingers sina shida sana we have loads of quality wingers


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lusajo kijana wa Yanga ..tulimsajili toka yuko Chuo kikuu hawezi kwenda Simba...anaona jinsi Gadiel,Ajibu na Kakolanya wanavyopata tabu mikiani...kwanza ana elimu kubwa kuliko Haji Manara lazima aje kwenye PHD'S
 
Mikia kwa kujipa moyo ..Allan Okello waulize Azam waliambiwa sh ngapi??(800m)Gabachori wenu hana hela hiyo..alafu Makambo Horoya analipwa $7000 mnaweza kumlipa zaidi ya hiyo..msijipe moyo na huyo muhindi wenu
 
Umefafanua vizuri. Tatizo la wachezaji wengi Simba ni kukosa speed kama ya Konde Boy, ndio hapo linapokuja hitaji la kukiongeza speed kikosi hasa kwa ajili ya game za kimataifa.

Nitofautiane na wewe kwenye beki kuongeza mzawa mmoja. Huyo mzawa atakayeweza kudhibiti AS Vita ni yupi? Au una maana watacheza walewale kina Wawa?Hata ndipo inapokuja hitaji na beki katili wa kigeni
 
Wawa bado ni defender mzuri sana akiwa na partner mobile na mwenye kasi kama Mwamnyeto maana kazi yake yeye itakuwa kufanya clearance tu.

By the way simba ina defender mwingine mzuri sana tu Yusuph Mlipili huyu anaweza kuvaa viatu vya Wawa bila shaka yoyote kwa uwezo wake.

Msimu aliopewa nafasi na Mario's Omog pamoja na Lechantre simba iliconcede magoli machache zaidi ukilinganisha na misimu ya kina Wawa na Nyoni.

By the way nimemtaja TIMOTHY AWANY humo kama Wawa kachoka basi Awany atafaa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trust me
Wanaondoka ni
Tairone
Shamte
Mlipili
Ndemla/fraga
Dilunga kuna biashara



Wanaokuja suggestion
Shonga
Mwamnyeto
Kelvin kijiri
Yondani
Papy Shishimbi 2years contronct /tayar huyu
Wangemchukua lusajo na Lucas Kikoti ingekuwa poa sana
 
Huyo umri umeenda
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwa kichuya hata sielewi na mimi
Kichuya ilikuwa ni issue ya busara ktk kumtunza kijana wetu kama shukrani kwake kwa kazi nzuri aliyofanya hapo kabla . Kwahiyo tusilalamike sana kuhusu Kichuya . Ilikuwa ni uungwana tu ili awe anasukuma maisha akisikilizia mipango mingine . Ni kijana wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Boko nadhani ninyi ni mashabiki ila hamjui umuhimu wa John Boko ila mjue majerui ya John Boko ndio yalichangia Simba Kutolewa Mapema na UD Songo.

John Boko character yake Sio Mfungaji Bali ni Msumbuaji mabeki na mtengeneza nafasi Ndio maana makocha wote wanampa namba kikosi cha kwanza hilo mlijue kama mlikua Hamjui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnatukosea sanaa mashabiki, endeleen tu ila siku tusipokuja uwanjani ndo mtashika adabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee baba clab bingwa africa si lelemama,, kumtegemea bocco? Acha masihara



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…