Kila mmoja ana mtazamo wake lakini kwangu mimi sioni Simba kama inahitaji idadi kubwa hivyo ya wachezaji
Kwenye defence tatizo lililopo ni Umri tu na hilo litamalizwa kwa kuongeza mchezaji mzawa mmoja tu.
Katika ligi yetu Bakari Nondo Mwamnyeto atafaa lakini hana uzoefu wa kutosha sana na ni last defender sijui kama ataweza kucheza kama namba nne aliyekuwa akicheza Juuko.
Katika Ligi za Afrika Mashariki yupo Timothy Awany wa KCCA ya Uganda huyu nae ni bonge la beki na anaweza kucheza hiyo nafasi hata national team ya Uganda alicheza hivyo baada ya kuumia Juuko.
Midfield.
Kimsingi Simba hawana tatizo kubwa sana la Midfielders has DM wanaye Mkude, Fraga, Mzamiru na Shiboub hawa ni midfielders wazuri sana tatizo moja wote hawana kasi kubwa sana.
Mkude na Fraga wanacheza kama Register lakini hawana speed na siyo wanabaji wazuri kutatua tatizo lazima wacheze na mtu anayekaba sana na hapo simba yupo mmoja tu MZAMIRU YASSIN.
CM Midfield simba ndiyo kuna tatizo wachezaji wengi viwango vyao vimeshuka sana na wengi siyo clinical CM ukiondoa Chama, na Dilunga wengine viwango vyao vinaleta changamoto sana hasa kina Ndemla, Shiboub, Dilunga kunahitajika mtu anayeweza kucheza double role lakini mtu huyo tayari simba wanaye. JONAS MKUDE na SHIBOUB, MZAMIRU YASSIN hawa watu unatakiwa kubadili mfumo tu ili waweze kupata nafasi . Uchebe aliweza kuwachezesha Kotei na Mkude pamoja au Mkude na Mkude na Mzamiru pamoja mmoja anacheza kama CM akicheza double role defence and attacking.
CENTRAL ATTACKING MIDFIELD hapa ndiyo kuna utata wachezaji wote ukiondoa Chama hawafanyi vizuri wengi wa wachezaji kwenye eneo hili wanacheza vizuri wakiwa wide. Kina Kahata na Kanda ,na Miraj kama Ajib angekuwa kwenye kiwango bora basi eneo hili lingemfaa sana lakin Ajib siyo wa kutegemea sana he is so slow and predictable.
Nani Aongezwe hapa namuona Konde Boy huenda akaleta impact zaidi, japo anaweza kununuliwa ALLAN OKELLO wa KCCA ya Uganda huyu bwana mdogo ni replica ya OKWI.
ATTACKING. Hapa ndipo naona tunahitaji kasi na ubunifu mkubwa. Wachezaji tulionao wote umri umekwenda sana na siyo wabunifu sana na kibaya zaidi hawana madhara nje ya 18 Kagere hana madhara nje ya 18 Bocco nae ni hivyo hivyo hapa ndiyo mtu wa kuja kuingia kwenye kikosi moja kwa moja na awe na kasi na mwenye uwezo wa kupiga long range shot. Mtu wa aina hii sioni EA labda wamsajili Heritier Makambo ni clinical finisher na anaweza kufanya runs nzuri zitazowapa space Kagere na Bocco.
Kama atakosekana Simba kwenye kikosi chake cha vijana wa mtoto anaitwa EDWARD GERALD mrefu hivi kama Emanuel Gabriel anaweza kupewa nafasi the dude is good ila hajapewa nafasi tu.
Wingers sina shida sana we have loads of quality wingers
Sent using
Jamii Forums mobile app