Usajili Mpya Simba SC: Umakini na utulivu wa kiwango cha juu sana unahitajika

Lusajo kijana wa Yanga ..tulimsajili toka yuko Chuo kikuu hawezi kwenda Simba...anaona jinsi Gadiel,Ajibu na Kakolanya wanavyopata tabu mikiani...kwanza ana elimu kubwa kuliko Haji Manara lazima aje kwenye PHD'S
Yeye anasema ataenda timu yoyote ili mradi wafikie makubaliano huo uyanga unaujua ww wenzako Wana malengo na maisha yao
 
Alan okelo nafikiri keshauzwa Azam walitia mguu wakaambiwa $400,000 Ila ni binge la mchezaji na umri unaruhusu
 
Ngoja tuone,,

Maana kule Yanga pashawaka motto,, ule msemo mwenzako akinyolewa we tia maji ,,

Hawa wadhamini wakitoa pesa pungufu ndo yale kutuletea wabrazil

Da silva,[emoji36]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha, wabrazili mliwasifu na clip za YouTube , mpeni GSM u main sponsor toeni sports pesa kifuani pale ,zengwe liishe
 
Hamuwezi kumpata Allan okello Nyie mikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
breaking newz za ki sport zinazo lindima ni kuwa viongozi na wafadhili wa lile li timu la ovyo la simba sport a.k.a mikia /mbumbumbu fc bado wamemganda na kumng'ang'ania yule striker mahili kabisa wa timu ya 'wananchi' yule aliye wanyorooosha vilivyo adi wakalala na viatu wiki nzima Bernard Morrison a.k.a 'chinja china mnyama' wakitaka asaini kwenye li timu lao lililo poteza mwelekeo hata kama ameisha saini kwenye timu ya pendwa ya wananchi…..
 
Hakuna mchezaji asiyetaka kucheza michuano mikubwa Ila Kama walitaka kumdajili ni Kama wanawakomoa kwa sababu wachezaji Aina ya Morris wako wengi
 
Hakuna mchezaji asiyetaka kucheza michuano mikubwa Ila Kama walitaka kumdajili ni Kama wanawakomoa kwa sababu wachezaji Aina ya Morris wako wengi
Ha ha ha mshalevywa nyie, hata Walter Bwalya viongozi wenu walimnyatia weeee, walipomkosa wakasema Bwalya ndio nani bwana! Kwanza tuna wachezaji wengi Wa type yake pale simba. Sasa tujuzane hapa ni wachezaji gani hao?
 
Mnaongea sana mwisho mnasajili wauza matunda toka Brazil
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Linapokuja swala la usajili kwa upande Simba kwa siku za karibuni imekuwa ni tatizo kubwa sana. Mwaka jana tuliaminishwa kuwa Idris Mbombo, Bwalya, Mugalu, Lazaro Kambole na hata huyo Shonga anayezungumziwa sasa wangekuja Simba lakini mwisho wa siku aliyekuja ni Da Silva.Najiuliza iwapo Shonga ilishindikana kumsajili wakati anatoka Zambia kwenda South Africa je sasa itawezekana kumtoa South Africa kumleta bongo? Ngoja tusubiri labda viongozi kuna kitu wamejifunza kutokana na usajili wa mwaka jana.

Hivi aliyemleta Chama si bado yupo Simba kwa nini asiingie chimbo tena akaleta wachezaji wa tano tu kama Chama au zaidi ya Chama kwenye nafasi zifuatazo:
1. Beki wa kulia wa kumsaidia Kapombe. Ikumbukwe hapa kuwa Kapombe anapata majeruhi ya mara kwa mara na msaidizi wake Shamte ni pasua kichwa mara leo acheze vizuri mara kesho aboronge. Inaelekea Shamte baada ya kusajiliwa Simba kwa mara nyingine mpira wake wote aliuacha huko Lipuli. Kwa nafasi hii hata mchezaji wa kibongo anatosha kwani Kapombe mwenye namba yake tayari ni wa kimataifa.
2. Mabeki wawili wa kati watu katili wa kazikazi kwa kwenda mbele mmoja mzawa mwingine wa kamataifa. Hawa wanatakiwa wawe vijana wenye kasi kwa ajili ya kupokea kijiti kutoka kwa Nyoni na Wawa. Nyoni kwa sasa hawezi tena kucheza mechi tano mfululizo bila majeraha na Wawa akili ipo lakini mwili unaanza kukataa. Baada ya mwaka mmoja au miwili hawa wote hawatakuwepo Simba. Kuna beki mmoja hivi rasta alikuja na timu ya mojawapo ya Zambia nimeisahau jina jamaa katulia sana yaani bonge la beki angefaa sana Simba. Beki wa ndani kuna Mwamnyeto, Nyoso au "wamrecycle" Mlipili. Naamini Mlipili bado ni bonge la beki ila sijui upepo gani umempitia toka kwa AUSEMS mpaka kwa SVEN
3. Kiungo mkabaji wa kimataifa mkata umeme kwelikweli mwenye kipaji cha kupokonya mipira kwa adui aweze kusaidiana na Mkude na Muzamiru. Hapa ndio shida hasa ya Simba ipo inabidi kamati ya usajili itulie hasa ili kumpata mchezaji sahihi wa hii nafasi. Ikishindikana kabisa kupatikanika basi wampe tena mwaka mmoja Fraga kwa masharti mazito kuwa aongeze kiwango chake zaidi ya alichonacho sasa.
4. Washambuliaji wawili asilia wa wakati mmoja wa ndani na mwingine wa kimataifa. Hapa inahitajika "goal machine" kwa gharama yoyote ile. Wanahitajika wachezaji wenye jicho kali la goli na si watu kubahatisha kama Da Silva na umri wao uwe mdogo. Boko na Kagere ni washambuliaji wazuri sana ila kwa sasa wanatakiwa wacheze mechi moja tu kwa wiki kutokana na umri wao lakini kwa sasa haiwezekani kwa sababu hakuna watu wa kuwapumzisha. Wakipatikana watu wa kuwapumzisha nina hakika watacheza hata misimu miwili mbele kwa ufanisi mkubwa.

Viungo washambuliaji wa katikati na wapembeni (mawinga) waliopo sasa Simba wanatosha sana. Na hapa ndio nguvu ya Simba ilipolala inabidi paachwe kama palivyo pasiguswe kabisa labda tu iwapo litachomolewa jembe na kuletwa jembe jipya kali zaidi.

Mwisho sioni nafasi ya Tshishimbi na Yondani Simba viongozi wawapotezee tu. Wachezaji waandamizi wenye umri na viwango kama Yondani na Tshishimbi wapo wa kutosha Simba sasa hivi wanahitjika vijana wenye umri mdogo damu inachemka kama akina Luis.
 
Ninyi hamna hela ya kununua top 3 goal score Wa timu kama pirates. Tuendelee kuulizia ulizia rejects ambao kwenye ligi yetu wataonekana bora
Southafrica team ni moja tu mamelod zingine takataka ndio maana zinafungwa hata na team ya somalia ,ni ujinga kumnunua mchezaji asiye na msaada Cuf chalpions league kwa bei kubwa
 
Nikiona comment kama hii nashangaa huyo morrison ana magoli mangapi na assist ngapi? Mchezaji ambaye takwimu zake anazidiwa na miraji Athuman asajiliwe na simba kwa kazi gani ?Lawama tunazopata kumsajiri ajibu zinatosha ,leo hii Dilunga akienda Yanga atakuwa mfalme na kuimwa kila saa sekunde ,dakika
 
Nikiona comment kama hii nashangaa huyo morrison ana magoli mangapi na assist ngapi? Mchezaji ambaye takwimu zake anazidiwa na miraji Athuman asajiliwe na simba kwa kazi gani ?
'si -zitaki mbichi hizi'………….
 
'si -zitaki mbichi hizi'………….
Footbal mchezo wa matokeo ni ujinga kwa simba kumpa mkataba morrison wakati wamejaza wachezaji wanaomzidi magoli na assist na experience ya kimataifa
 
Uchebe aliacha list hiyo hiyo ya wachezaji watano aliporudi akakuta wachezaji wapya 12
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…