Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Siku moja nna haraka zangu Mbeya stendi pale jamaa wakaniwai sa 3 inakuja bus abood toka Tunduma.mi poa nimelipa badae bus hilo ngalangala la Abood.

Siti zote zimejaa nikadumbukizwa humo kulikua na kiroba cha mchele sijui kitu gani nimekikalia mpk Dar.

Wale wenye mchele sijui walikuta una hali gani,

Kufika Moro sa tisa tukaambiwa tushuke ngoma ipigwe service.

Sa moja usiku ndo safari ikaanza tena kuitafuta Ubungo
 
Mimi ninadhani hicho ni kiwango cha kawaida tu kwa kampuni kama Abood. Hata alipoingiza hizi zilizopo sasa ni hivyohivyo tu. Ninakumbuka ilikuwa sherehe pale Msamvu, misele ya kufa mtu roundabout wakipokewa na bodaboda.

Ninafikiri kwetu wateja, muhimu sasa ni kuletewa basi zilizo comfortable na rafiki kimatumizi. Yutong tunazoletewa ni za kikuda sana. Pot za kuchajia zinadumu miezi,hazifiki mwaka. AC halikadhalika—ikishabuma mtakoma humo kwenye basi. Siti pia ni ndogoo,ukiwa mrefu ama kibonge imekula kwako.

Ninajua haya ndo huchangia kushusha bei ya basi huko sokoni uchina. Lakini,kwakuwa kampuni ina uwezo, ingia dau kubwa, lete chache za ukweli wenye uwezo wapande kwa bei elekezi. Wateja wapo. Tunaona BM ana zile zenye daraja la kwanza na la pili. Kila siku daraja la kwanza zinajaa fasta.

Halafu Abood kama mnanisoma acheni ubahili. Katikati ya Dar na Moro jengeni kahoteli uchwara ka kupata bites na kujisaidia. Mnahama vihoteli, mnapeleka abiria vihoteli vinanuka choo utasema vyoo vya stend. Bites za kiwango cha chiiini.

Safari ni starehe jamani.
Safari ya saa tatu (3:00) unakula chakula njiani! Ni muda sawa na Mbagala kwenda Mbezi stendi unataka ule njiani!
 
Kiboko yake kafariki. Magu alikuwa anamchamba Nassoro Abood anavyotaka. Ikiwemo lile la kutoa mabasi kupeleka watu misibani huku viwanda kaua.
Magu alimsikiaga afande sele alivyokuwa act, kiwanda kafugia mbuzi, watu tunakufa na njaa kazi hatuna, tunakufa na njaa anatoa mabasi, ya kutuzikia, kipindi kile alivyokuwa anagombea ubunge, na alivyosema afande ni kweli, Kuna mbuzi kibao wakula yeye na familia yake.
 
Asee wakuu kumbe kuna watu wana jax sana hii nchi. Nimeona huko Twitter kuwa huu ni usajili wa mabus 20 mapya ya Abood.

View attachment 1972491
Tutafute hela wakuu.

45C70234-7F55-4635-934B-0F9261423D04.jpeg
 
Safari ya saa tatu (3:00) unakula chakula njiani! Ni muda sawa na Mbagala kwenda Mbezi stendi unataka ule njiani!
Jiongeze kidogo basi, au wewe ni product wa hii elimu yetu iliyologwa nini? Maana kizazi cha shule hizi ni majanga.

1. Umeona hapo sikutaja ugali wala makande, nimesema bites. Hilo umeshindwa kuona inamaanisha nini?

2. Haya, umetoka Moro na gari ya kwanza. Yani ukae mdomo unanuka na njaa mpaka Dar kisa kuna mtu kama wewe anasema safari ya saa tatu huhitaji kula? Siku hizi chai unauziwa kwenye kibobo chako safi, unaingia nacho garini.

3. Kwahiyo, ushawaza na kuona kuwa ulionao wote ndani ya gari mpo sawa. Wamekula kama wewe, wanajisikia haja kama wewe n.k. na hivyo,vile unajisikia wewe,abiria wote wanajisikia hivyo.

Ninadhani hapa umeathiriwa na mawazo yetu yale ya kudhani unachowaza wewe ndiyo ulimwengu. Walimwengu hatupo sawa kama ulivyokariri. Aidha, maisha yamebadilika, mengine tuliyafanya sababu ya kukosa uwezo, fursa na sehemu za kufanya haya. Mwaka 80 si sawa na 2021.

Tafakari, chukua hatua
 
Back
Top Bottom