Mimi sijui idadi yake lakini sitasahau tukio la almost 20 years ago!!!
Nimefika zangu Ubungo nimekuta basi la kampuni fulani hivi (nimesahau jina lake lakini sio Islam) likiwa na watu zaidi ya robo tatu kama sio zaidi.
Wakati huo huo, basi moja ya Aboud ndo lilikuwa linajitayarisha kupakia abiria, na kwahiyo halikuwa na abiria hata mmoja!!
Sasa kwavile sikuwa na uzoefu na mabasi yaendayo Morogoro, nikapanda lile nililoona limejaa zaidi ya 3/4 huku nikiamini ndo nitawahi kuondoka!!
Kitu ambacho sitasahau, ziliondoka Aboud kama sio 4 basi 5 wakati basi letu lililokuwa limejanza zaidi ya 3/4 kabla yao tukiwa pale pale!!
Na ninachotaka kusema kwamba, labda siku hizi kwavile magari ni mengi lakini kwa wakati, hiyo nusu saa ingekuwa zinaondoka Aboud angalau 3 kwa route moja!!!