Usajili wa Selemani Mwalimu kwenda Yanga ni uhitaji wa mahitaji ya team au ni kumkomoa mtani?

Usajili wa Selemani Mwalimu kwenda Yanga ni uhitaji wa mahitaji ya team au ni kumkomoa mtani?

Ulaya unaweza kufananisha na bongo, bongo ni sehemu pekee mchezaji anatambulishwa bila kumaliza taratibu za Usajili, bongo pekee wachezaji wanasajiliwa kwa kukomoana Huna kiungo mbunifu kwenye team unaenda kujaza mastriker sita kwenye team moja as if unacheza michuano 10??? Wewe umewahi kuona wapi hii
Mi nimefananisha na Chelsea mtindo wa kusajili wachezaji wanaotakiwa na timu nyingine bila kujali mahitaji
 
Wadogo zangu flan huwa nawaambia, achana na Yanga linapokuja suala la maslahi ya timu yao. Hapo huwa haangaliwi mtu. Yule Hersi yule anaheshimika kwakua anachokifanya ndicho Yanga wanakitaka, siku akitaka kujua watu wanaipenda club kuliko yeye na hata Gsm, aanze kuzingua.
Hakuna somo gumu ambalo yanga wanajiamini nalo kama lile la kupita njia ngumu ya BAKULI na bado hawakuwahi kufungwa na simba wala kushuka chini ya nafasi ya pili! Mpaka kesho wanaamini hata bila tajiri Yanga yao wanaiweza na wataimudu
Hakika mkuu, yanga ndio timu yenye mashabiki chizika inapokuja kwenye maslahi ya timu Yao....!!.
 
Nimeshanganzwa na Usajili wa Selemani Mwalimu unaonesha mambo makuu mawili:

1. Uongozi mzima wa Simba hawafanyi vitu kiprofessional, huwezi kutambulisha mchezaji kwenye tamasha lenu kumbe ujamalizana na club na mchezaji kwa asimilia zote hii maana yake Nini? Mnafanya mashabiki wenu wasiwaamini lakini pia mnatengeneza migogoro isio na sababu za msingi

2. Yanga wamemsajili Selemani Mwalimu kimihemko ili kuwakomoa wapinzani wao lakini ukiangalia kwenye team yao Wana strikers wanne wenye uwezo mkubwa na wanatosha na ujio wa Mwalimu anakuwa watano, pengo la team yao hawana kiungo mbunifu ambaye anayeweza kumchallenge Okello unaona kabisa wanafanya siasa wakati wanatakiwa kuwaza zaidi Caf champions league.
Mtani kawaida ni wakunyooshwa hadi anyone.
 
Mi nimefananisha na Chelsea mtindo wa kusajili wachezaji wanaotakiwa na timu nyingine bila kujali mahitaji
Najua dili la Mudryk linakuuma ile mbaya ni kweli Mudryk hakuwa kwenye mipango yetu kabisa Hilo lilikuwa wazi ila tulikuwa tunahitaji left winger mwingine atakayeleta competition na Sterling kwenye hiyo nafasi na kwakuwa sokoni kulikuwa na mchezaji Bora kama Mudryk na anaelekea kwa wapinzani wetu ndipo tukaingilia deal. Kwa hiyo mkuu hizi ni scenario mbili tofauti na hiyo ya Yanga soma vizuri.
 
H n kama ile ya chama, n bc tuu ilimradi Mtani ateseke
Simba hawezi teseka kwa Sele Gomez. Usajili wake ilikuwa ni backup ya Mpanzu. Tangu last season alikuwa anatokea benchi.

Ajitokeze mshabiki wa Simba ambaye alikuwa anaamini Sele Gomez ndio alikuwa tegemeo la timu kwenye ushambuliaji tumuone.!
 
Nimeshanganzwa na Usajili wa Selemani Mwalimu unaonesha mambo makuu mawili:

1. Uongozi mzima wa Simba hawafanyi vitu kiprofessional, huwezi kutambulisha mchezaji kwenye tamasha lenu kumbe ujamalizana na club na mchezaji kwa asimilia zote hii maana yake Nini? Mnafanya mashabiki wenu wasiwaamini lakini pia mnatengeneza migogoro isio na sababu za msingi

2. Yanga wamemsajili Selemani Mwalimu kimihemko ili kuwakomoa wapinzani wao lakini ukiangalia kwenye team yao Wana strikers wanne wenye uwezo mkubwa na wanatosha na ujio wa Mwalimu anakuwa watano, pengo la team yao hawana kiungo mbunifu ambaye anayeweza kumchallenge Okello unaona kabisa wanafanya siasa wakati wanatakiwa kuwaza zaidi Caf champions league.
Striker alikuwa Shalulile tu.
 
Sasa kma Simba wote mna akili mnashindwa vipi na wenye akili wawili?. Unapigwa MITI wewe 😂😂🤣. You better watch your back.
 

Attachments

  • IMG-20260810-WA0018.jpg
    IMG-20260810-WA0018.jpg
    99 KB · Views: 12
Mimi kama shabiki wa Simba kilichonikera ni kwamba viongozi wetu hawako professional, unamtambulishaje mchezaji ambae hujamalizana nae yeye personally pamoja na timu yake..... Seleman Mwalimu kwenda yanga hata hainisumbui maana mchezaji mwenyewe hana output yoyote ya maana ni kuruka ruka tu pale mbele... Ilifika kipindi kocha akawa anamtumia Mpanzu kama false nine atleast ana convert nafasi vizuri....

Hata siku ya Simba day niliona ni upumbavu kulingia kuendelea kubaki na Seleman Mwalimu as if kwamba ana umuhimu wowote... Kwenye ligi ya Tanzania ni Fei Toto pekee ningependa atue Simba but wapuuzi wengine sina habari nao..
 
Kwakua mchezaji mzawa wala hakuna shida acha tu aende hapo akapambanie namba. Mimi nachojiuliza ni kitu kimoja, Magori anasema hawawezi kutoa karibu 1B kwa mchezaji kama Sele Mwalimu kwa mkopo wa mwaka mmoja, kwanini hawakutoa ile USD 75k walotajiwa na Wydad Casablanca ambayo ni ndogo sana ukilinganisha na USD 200k walotoa Yanga kama inavyodaiwa? Hivi kweli uende sokoni kununua nyanya unaambiwa fungu linauzwa Tsh 500 unasema nitakuja kesho kulipa hela then anakuja mtu anatoa Tshs 2000 ananunua nyanya zile zile baadae unakuja kusema siwezi kutoa hela yote hiyo kununua nyanya mbovu kama zile? Hapo jibu ni moja tu HAUKO serious na hiyo biashara, kwakifupi ni mbabaishaji. By the way Magori anadharau thamani ya Mtanzania mwenzake akiona hastahili hizo PESA. Nje ya mada kidogo hivi ile kitu inaitwa Financial Fair Play hapa Africa haipo eeeenh?
 
Nimeshanganzwa na Usajili wa Selemani Mwalimu unaonesha mambo makuu mawili:

1. Uongozi mzima wa Simba hawafanyi vitu kiprofessional, huwezi kutambulisha mchezaji kwenye tamasha lenu kumbe ujamalizana na club na mchezaji kwa asimilia zote hii maana yake Nini? Mnafanya mashabiki wenu wasiwaamini lakini pia mnatengeneza migogoro isio na sababu za msingi

2. Yanga wamemsajili Selemani Mwalimu kimihemko ili kuwakomoa wapinzani wao lakini ukiangalia kwenye team yao Wana strikers wanne wenye uwezo mkubwa na wanatosha na ujio wa Mwalimu anakuwa watano, pengo la team yao hawana kiungo mbunifu ambaye anayeweza kumchallenge Okello unaona kabisa wanafanya siasa wakati wanatakiwa kuwaza zaidi Caf champions league.
Yanga msimu huu imeondokewa na washambuliaji wake wote wa kati! Kuanzia Dube, Depu na Mwanengo. Mzize bado hayuko fit. Na wamesajiliwa washambuliaji wawili pekee wa nje (Shalulile na Toure). Hivyo sioni kama kuna tatizo kumsajili mshambuliaji mwingine mzawa wa kiwango cha Mwalimu.

Isitoshe msimu mpya una mashindano mengi, na ligi itatakiwa kuisha mapema kwa ajili ya AFCON ya 2027, ambayo Tanzania ni mwenyeji.
 
Back
Top Bottom