Uchaguzi 2020 Usaliti ni laana : CUF yakosa wagombea, Lipumba aanza kuokoteza mitaani, aomba wote wanataka kugombea wajitokeze


Lipumba angefanya harakati gani dhidi ya Ukawa, kwani ana mvuto gani? Maana hata harakati zinatakiwa uwe na mvuto kwa watu, mwenye mvuto wa watu huko Cuf alikuwa Seif.

Siijui katiba ya CuF inasema nini kwenye nafasi ya uwenyekiti hilo ni kweli, lakini kwanini alazimishe kurudi kwenye uenyekiti kwa msomi kama yeye, tena akiwa ameshaandika barua ya kujiuzulu nafasi yake? Kulikuwa na ulazima gani wa yeye kuleta tafrani kwa nafasi ya uwenyekiti. Au nafasi pekee anayoitaka ni lazima awe mwenyekiti?

Ni kweli kwa mujibu wa katiba yenu angeweza kugombea, kwanini hakungoja tena hadi hali iwe nzuri bali akawa analazimisha tena kwa backup ya ccm? Hao akina Maalim seif wanahaja gani ya kusubiri utaratibu kwa mtu aliyekimbia? Haya sasa hao akina Maalim Seif wameondoka baada ya mizengwe, mbona chama hakina mvuto? Au nyie wanachama mliokuwa mnamtaka Lipumba hamna mvuto kama yeye?
 
We kijana vipi? Mbona mgumu kuelewa na hutaki kujifunza?

Hii ni mara ya tatu sasa nakujibu kwamba Lipumba hakulazimisha kurejea uwenyekiti bali ni sisi wenye chama ndiye tulimtaka arejee na hii ni kutokana na jinsi tunavyofahamu utumishi wake na misimamo yake juu ya CUF. Tuliona ni bora tukosane na mamluki wa ccm kwenye chama chetu akina Maalim Seif na Mtatiro waliompenda kada mwenzao Lowassa kuliko kumpoteza Jembe letu ambalo limetutoa mbali.

Maalim Seif alijipima ubavu na Lipumba lakini siyo saiz yake na akaamua akimbie chama. Eti Katibu Mkuu wa CUF wakati haijui Tanzania bar zaidi ya Dar. Hata CDM walitaka kujaribu kuvamia Buguruni kusaidia Maalim, daaadeki tukasema ngoja waje ndipo watajua Buguruni wanaishi wahuni na hawakuthubutu. Wakaishia kulalamika eti ooh Lipumba analindwa na vyombo vya dola!

Lakini unaposema hana mvuta kwani amekosa kitu gani ambacho wanasiasa wengine wanakipata? Na kama unakili alishindwa kufanya harakati dhidi ya upinzani kwavile hana mvuto, basi tuambie hiyo pesa ambayo nyie CDM mnasema alipewa na ccm ilitumikaje? Na kama alishindwa kuitumia kama alivyotakiwa kufanya je ana deni na ccm?

Na kama unadhani CUF haina watu, subiri uone wagombea kila kona ya nchi wakipeperusha "bendera kubwa" kwenye kampeni mwaka huu.
 

Wanachama mliomtaka arudi kwenye uenyekiti ni nyie wenye maslahi naye. Aliyekuwa na mvuto huko Cuf alikuwa Seifu hilo halina mjadala. Afanye harakati zipi, kwani alilipwa hela gani ya maana zaidi ya kuahidiwa fadhila fulani, ikiwemo hiyo kurudishwa kuwa mwenyekiti wa CUF.

Hana mvuto, na hapati apatacho seif kwa kuwa na mvuto kuliko yeye. Kusimamisha kweli mtasimamisha wagombea nchi nzima maana mna backup ya ccm, shida itakuja kupata kura za wananchi. Labda Magufuli awagaie baadhi ya majimbo kwa kumnyenyekea, maana yeye sasa hivi ndio anapanga nani atangazwe mshindi.
 
Nashukuru kwani mpaka sasa somo limeeleweka kwavile hoja zako hadi sasa zimeshindwa kupinga au zinakubalians na mambo yafuatayo.
1. Lipumba alikuwa sahihi kupinga Lowassa kuwa mgombea urais wa UKAWA, bali hata wewe unaona CDM walicheza pata potea,
2. Hakuna pesa yoyote aliyopokea Lipumba toka ccm,
3. Lipumba hakufanya harakati yoyote dhidj ya ukawa,
4. Lipumba hajakiuka katiba ya CUF wala sheria ya vyama vya siasa kwa maamuzi ya kujiuzuru na kurejea uwenyekiti,
5. Maalim Seif na wafuasi wake walifanya makusudi kutozingatia katiba ya CUF kufanya uchaguzi ili apigiwe kuraku ya "HAPANA" na kumthibitishia Lipumba kuwa hatakiwi na wanachama awe mwenyekiti.

Asante sana!
 
Huwa najiuliza kwanin ccm hamlali kila siku mnawaza cdm wakati wao hawana habari na nyie hata kidgo. Cdm ni kimbilio la wananchi, fisiemu wanajaribu kujiaminisha kuwa chedema imekufa huku kila siku wakiinandi bila kujua. Jiwe ataiuwa fisiemu bila kujua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chizi fresh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeulizwa mbona chama hakina mvuto tena? Au na nyie hamna mvuto kama Lipumba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona shati lake kama vile mtumba ??
 
Hii hainihusu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…