Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kuna mambo mengi huyajui na bado unasema una hoja! Hivi nilipokuuliza Lipumba alifanya harakati gani dhidi ya UKAWA kwa kutumia pesa aliyopewa na CCM ulijibu nini?
Unasema hujui katiba ya CUF inaelekeza nini kuhusu kujiuzuru kwa kionfozi na bado unaona Lipumba alikosea au alipendelewa na uamuzi wa mahakama!
Yaani kwa kudhihirisha hujui chochote unssema Lipumba alijitoa kwenye chama! Kwa taarifa yako alichofanya ni kujiuzuru uwenyekiti ili asijihusishe kama mwenyekiti mwenza wa UKAWA kumnadi Lowassa kada la ccm, bali alitaka abaki kama mwanachama wa kawaida. Kwa mujibu wa maneno ya Lipumba mwenyewe kadi yake ya uwanachama wakati anajiuzulu ilikuwa hai hadi 2022.
Lakini unaposema kulikuwa na ulazima gani arejee uwenyekiti nilishakujibu wanachama tulikuwa tunamuhitaji arudi kwenye nafasi yake.
Lakini jifunze kuanzia sasa kwamba endapo kungefanyika uchaguzi ili kuziba nafasi ya mwenyekiti, Lipumba bado angeweza kugombea kwavile ana haki kutokana na kuwa mwanachama hai. Sasa jiulize kwa ufahamu wako kwanini akina Maalim Seif hawakufuata utaratibu huu ili Lipumba akataliwe kwa njia ya kidemokrasia?
Bado unahoja?
Lipumba angefanya harakati gani dhidi ya Ukawa, kwani ana mvuto gani? Maana hata harakati zinatakiwa uwe na mvuto kwa watu, mwenye mvuto wa watu huko Cuf alikuwa Seif.
Siijui katiba ya CuF inasema nini kwenye nafasi ya uwenyekiti hilo ni kweli, lakini kwanini alazimishe kurudi kwenye uenyekiti kwa msomi kama yeye, tena akiwa ameshaandika barua ya kujiuzulu nafasi yake? Kulikuwa na ulazima gani wa yeye kuleta tafrani kwa nafasi ya uwenyekiti. Au nafasi pekee anayoitaka ni lazima awe mwenyekiti?
Ni kweli kwa mujibu wa katiba yenu angeweza kugombea, kwanini hakungoja tena hadi hali iwe nzuri bali akawa analazimisha tena kwa backup ya ccm? Hao akina Maalim seif wanahaja gani ya kusubiri utaratibu kwa mtu aliyekimbia? Haya sasa hao akina Maalim Seif wameondoka baada ya mizengwe, mbona chama hakina mvuto? Au nyie wanachama mliokuwa mnamtaka Lipumba hamna mvuto kama yeye?