Ushabiki wa Simba na Yanga umewapumbaza Watanganyika

Ushabiki wa Simba na Yanga umewapumbaza Watanganyika

Heshima sana wanajamvi,

Katika miaka ya karibuni ( labda 2020 - 2024) umekuwepo ushabiki mkubwa wa mpira baina ya Club mbili kubwa Simba Na Dar Young Africa.

Ushabiki wa mpira,ngoma,kwaya,sarakasi,sana saana nyinginezo si jambo baya hasa katika kuburudisha na kuboresha afya ya akili.

Nimeanza kubaini kupitia ushabiki wa Simba na Yanga limezaliwa tatizo lingine jipya,Vijana hawajui au hawataki kufahamu kuhusu nchi yao.
Hawajui Bandari zimeuzwa kwa Waarabu.
Hawajui Uwanja wa ndege wa Kimatiafa Kilimanjaro umeuzwa.
Hawajui Ngorngoro imeuzwa kwa waarabu.
Hawajui Zanzibar inaitawala Tanganyika (Tanzania Bara)
Hawajui Ardhi ya nchi yao Tanganyika inauzwa kwa wageni.
Hawajui lolote kuhusu nchi yao.
Wakilala wakiamka Simba day,Yanga day huu upuuzi wa hizi team umewadumaza vijana wengi wa kiTanganyika badala ya kufikiri kuhusu nchi yao inavyoporwa kama wenzao wa Kenya wao wanakuambia "UBAYA UBWELA" siku wakistuka watakuta kila kitu kimeuzwa.

Ngongo kwasasa Gairo.
Nina wasi wasi hizi tema zinafadhiliwa na system inayopumbaza watanzania kwa maslahi ya kijani.
 
Tanzania ina raia zaidi ya milioni sitini, Sina hakika kama ni jambo rahisi kutaka kuwapangia watu wote hao nini wafanye au wasifanye.

Kama hilo ndio jambo wanaloona linawapa furaha waache wafurahie. Kula si ni juu yao wenyewe?
Kwa hiyo wewe unaona Kula ndio issue?

Hand to mouth?
 
Sasa hivi hata ule uvumi wa mauaji ya watoto umefunikwa na simba day na yanga day.

Niliwahi kusema humu labda kizazi kinachozaliwa kuanzia 2020 na kuendeleq kikiwa watu wazima ndio kije kilete mabadiliko lakini so vizazi vya kabla ya hapo.

Mimi binafsi inaweza kuwa hizo timu zinacheza wala hata sijui kuwa leo kuna mrchi zao. Ukiniambia nikutajie hata wachezaji watatu wa hizo timu siwajui. Lakini mambo ya siasa na kinachoendelea dunia nzima ninajua.
Your are brave.
 
Yaani golden generation of youth wa kipindi cha UDSM ya mwalimu Nyerere, Mwinyi na kuishia kwa Mkapa ilishindwa (proved failure and misbehaved to become corrupts) leo hii utegemee kizazi cha DP WORLD kweli? Hawa watoto broilers kama wa Mwigulu Nchemba ndo waje walete maajabu? Can't be serious at all.

Ni kwamba, inabidi tuzoee tu milele na milele. Mfumo unafurahi mno kuona citizens wako Simba na Yanga all the time. Leo rais wa inchi atakuwa mgeni rasimi, kesho atakabidhi kombe.They like it, they encourage it. Unazi wa Simba na Yanga unaipa nafuu Serikali. Mbwa warushie mifupa, then fanya yako kwa raha zako.
 
Media houses ni kama Yale makanisa ya upako! Zina maelekezo kuwa-brain wash wadanganyika!
Sure mkuu, na hili ndo tatizo...
Sasa hivi redio stations zinazoongelea michezo for almost 6-7 hrs a day ni nyingi mno.
 
Hakika ina kera sana, vijana wenzangu Siasa ndio Maisha, tushiriki na kuishi nayo
Rai kwa vyama makini vya siasa, Viongozi wa Dini, NGOs, Vyama vya Kitaaluma na Waandishi wa Habari, kulichukua hili na kulifanyia kazi, la sivyo TUTAKWISHA!
 
Kuna midingi huwa inakaa pale Posta mpya, yaani saa 12 asubuhi inakunywa tangawizi na kubishana bishana habari za Simba na yanga. Yaani siyo Gen Z tu, hata hizo generation nyingine katika hii nchi ni za hovyo kupindukia.
 
Kwa kifupi tumekwisha,
 
Hakika ina kera sana, vijana wenzangu Siasa ndio Maisha, tushiriki na kuishi nayo
Rai kwa vyama makini vya siasa, Viongozi wa Dini, NGOs, Vyama vya Kitaaluma na Waandishi wa Habari, kulichukua hili na kulifanyia kazi, la sivyo TUTAKWISHA!
Tushakwisha mkuu, kama huwazi huwezi kuhoji,
 
Media za nje kama taarifa ya habari ni nusu saa ,wanaacha dakika tano za mwisho za sports na entertainment, hapa kwetu asubui asubui tu ni mpira mpira mpaka unajiuliza tumekuwaje,
 
Hii project ya watawala kuwazubaisha watanganyika kuacha kufikiri mambo ya msingi.
 
Hii mada ishajadiliwa sana humu.

Kama wewe hupendi michezo endelea kufuatilia habari za Mwabukusi na safari za mpiga mwingi. Haiwezekani wote nchi nzima wawe busy na siasa tu. To each their own.

Ubaya ubwela 😅 japo sijui maana yake.
 
Hakika hunishindi mimi ninavyochukia ,.kuna broh mmoja yule hata ukimuuliza mkuu wa Mkoa anaitwa nani hajui,kunaendelea nini kimataifa hajui muda woooote yeye ni Yaaaanga eeenh Yangaaa akipiga nyimbo ni za Yanga akiwasha tv anataka habari za yanga akipiga stori yanga akiingia you tube anamsikiliza Manara tuuuh nachukia mbaya yani
Je ameshawahi kukuomba umpe chakula au ulipie watoto wake ada?...Wewe fuata mambo yako.
By the way ni vizuri mtu kujua yanayoendelea nchini kwako ila kubwa zaidi kila mtu apambanie maisha yake anavojua
 
Media za nje kama taarifa ya habari ni nusu saa ,wanaacha dakika tano za mwisho za sports na entertainment, hapa kwetu asubui asubui tu ni mpira mpira mpaka unajiuliza tumekuwaje,
Yaani ni mambo ya AIBU kabisa..michezo masaa 3-5..MEDIA badilikeni
 
Back
Top Bottom