Ushahidi huu hapa, hakukuwa na Tender kama Waziri Mbarawa alivyosema leo

Waswahili wanasema, Kwa enzi hizi, Muogope MUNGU na Teknolojia. Naomba msome kipende AView attachment 2687881
Jana wengi tuliingia mkenge kuamini alichosema Waziri na timu ya serikali.

Inawezekanaje serikali ikasema uongo kwenye sensitive issue kama hii? Wanalinda maslahi ya nani kutudanganya sisi wananchi hususan wapigakura wake?

Kwa aibu hii ni vyema likaitishwa Bunge la DHARURA kujadili mustakabali wa nchi ili kupiga kura ya imani kwa serikali.
 
Hawa jamaa safari hii wameingia cha kike. Kila uongo wao unapanguliwa na ushahidi wa kuwasuta kabisa.

Bibi kajazwa akajazika mwisho wa siku jumba bovu litamuangukia yeye mwenyewe
Sisi tunaompenda kwa kumkosoa na kumshauri wametuundia sheria kali sana sana

Asijilaumu maana kila kitu anafanya kwa hiyari yake
 
Hakuna unachokijua sioni hoja yako ,ulitaka kwamba hao DP world wa aknowledge competitors wao kweny hayo makubaliano ?
 
Na usisahau kuwa huo mkataba kuja kwa wananchi ni kwa njia ya KUVUJA. Haukuletwa rasmi kwamba uwafikie wananchi ili nao watoe maoni yao.
 
Kabla ya Mkataba huu niliamini Wazanzibar wote ni wacha Mungu na Wana hofu ya Allah, kumbe Nilikuwa najidanganya. Wapo waongo, Wanafiki, Wazandiki na hata Wazushi.
Na wako upande wa Ibilisi na wanakula naye na kucheka naye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…