Ushahidi kuwa binadamu tumeumbwa na hatujatokea tu

Ushahidi kuwa binadamu tumeumbwa na hatujatokea tu

Hayo yote ulioandika yana majibu kwenye sayansi. Na hata kama hayana majibu au ufafanuzi haimaanishi kwamba mungu ndio ameyafanya. Hili ndio tatizo la watu wa dini. Mnatafuta kitu ambacho wanasayansi hawajakipatia ufafanuzi na kusema ni mungu ndio amefanya.
Majibu hayo hayana na kamwe hayatokuja kuwa na majibu ya kisayansi. Trust me!

Siongelei dini, naongelea Reality!

Maswali muhimu kama haya hayana majibu ya kisayansi na bado unaiamini sayansi?

Think Big!
 
Kwa kweli JF ni 'Where we dare to talk openly'....Yaani mada kama hii ipo JF Intelligence?

Mleta mada kama ulitumia miaka 10+ Shuleni, inabidi urudishe gharama ulizozitumia.
Jibu hoja. Acha kuzunguka.

Kwanini kuna gender? Gender imetoka wapi? Where did this intelligence of gender came from? Dont you see any intelligence?

Think Big!
 
Jibu hoja. Acha kuzunguka.

Kwanini kuna gender? Gender imetoka wapi? Where did this intelligence of gender came from? Dont you see any intelligence?

Think Big!
Inaonekana unawaza ngono sana,.....Kwanini uwe bothered na uwepo wa Gender badala ya vitu vingine kama ubongo?
 
Mkuu huyu Mtu anashangaza sana.... Eti DNA ni ushahidi wa uumbaji wa Mungu, sasa mbona kuna natural errors nyingi sana kwenye DNA?.... Mbona kuna mutations?

Halafu anasema Mungu alimuumba Mtu akiwa na utashi wa kujua jema na baya, ili hali Kulingana na Bible Mtu alipata ufahamu wa jema na baya baada ya kuasi kwa kula matunda yaliyokatazwa....kwa hiyo Mungu alimuumba Mtu asiye na utashi na kama alimuumba kwa mfano wake, basi Mungu hana utashi wa kujua jema na baya unless na yeye alikula matunda ya mti wa katikati

Hoja nyingine hazina mashiko, eti science haijui Kwanini watu wanazaliana, eti science haijui Kwanini kuna jinsia mbili, eti science haijui Kwanini kuna mifumo mbalimbali mwilini...... Hahahaaaa dah! huyu jamaa ana matatizo makubwa mno.
1. Kuna errors katika DNA kwa sababu ya dhambi.

2. Binadamu ameumbwa mwenye uwezo wa kujua jema na baya, haijalishi amejua jema na baya kwa njia ipi au wakati gani. Kiujumla ameumbwa na uwezo wa kujua jema na baya na ndio maana amejua jema na baya.

3. Hoja zingine hazina mashiko kwako; kwa sababu hauna majibu.

Think Big!
 
Halafu na neno analitoa kwenye bible et zaeni mkaongezeke mkaijaze dunia! sasa mbona tunadanja..? tutaijaza lini sasa na tukiijaza inafaida gani..?hii ni hatari ya ubongo!
Tunakufa kwa sababu ya dhambi. Binadamu aliumbwa akiwa na asili ya kutokufa. Akamuasi Mungu akavaa mortality.

Think Big!
 
1. Kuna errors katika DNA kwa sababu ya dhambi.

2. Binadamu ameumbwa mwenye uwezo wa kujua jema na baya, haijalishi amejua jema na baya kwa njia ipi au wakati gani. Kiujumla ameumbwa na uwezo wa kujua jema na baya na ndio maana amejua jema na baya.

3. Hoja zingine hazina mashiko kwako; kwa sababu hauna majibu.

Think Big!
Nadhani nilikuambia hapo mwanzo, kama ulitumia miaka 10+ Shuleni, tafadhali lipa hizo gharama ulizotumia ili ziweze kusomesha wenye akili!.....Unapost pumba bila aibu hata kidogo.....kweli IDs fake zinaficha mengi mno.
 
Majibu hayo hayana na kamwe hayatokuja kuwa na majibu ya kisayansi. Trust me!

Siongelei dini, naongelea Reality!

Maswali muhimu kama haya hayana majibu ya kisayansi na bado unaiamini sayansi?

Think Big!
Tatizo la hii dunia ni binadamu kujaribu kumreplicate God...how can you separate God and science...it is crazy when human are in dark and they can not understand something they call it supernatural but when they do they brand it science...
 
"Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, akatawale viumbe vyote".

Je, wingi kwenye hii nukuu unaiongeleaje?
 
Ni dhambi kubwa sana tena ni tusi kubwa sana na nidharau kubwa sana na ni kumvunjia heshima Mwenyzimungu kwa kumsingizia eti aliumba mtu kwa mfano wake, na kama yupo huyo mungu alie umba binaadam kwa mfano wake basi mungu huyo ni dhaifu sana kama alivyo dhaifu binaadamu.
Mimi naamini Mwenyezimungu sio dhaifu hivyo, huko ni kumtusi Mungu
 
Duh! Yaani umeandika pointless na bado kuna kiumbe ka like? Dah!

Hujajibu swali. Kwanini kumekuwa na jinsia? Sijauliza umuhimu wa jinsia.

Nimeuliza jinsia zimetoka wapi? How can big bang create gender? How can evolution creates gender?

Think Big!
Kazi ya jinsia ndio sababu ya uwepo wake.
Jinsia ni mfumo kama mifumo myengine ktk mwili ambapo kila mfumo unakazi yake kuhusu swala la wapi jinsia imetoka ni ktk mfumo unaoratibu uundwaji wa mwili DNA lkn pamoja na hayo bado sayansi inaendelea kuchunguza nini chanzo cha hayo yote what we need is time.
naomba nikukumbushe kuwa sayansi hukua, leo wanaweza kukosa majibu lkn kesho wakapata kuwa mwangalifu usemapo "Hakuna sababu yoyote ya kisayansi inayoweza kuelezea kwanini...." nini kama ikiwezekana kueleza na ikawa proved..?

kuhusu bing bang na evolution siwezi kukuelezea how zimecreat gender coz binafsi sijaziamini bado na hazina prove kwamba zenyewe ndo source of life
 
Nadhani nilikuambia hapo mwanzo, kama ulitumia miaka 10+ Shuleni, tafadhali lipa hizo gharama ulizotumia ili ziweze kusomesha wenye akili!.....Unapost pumba bila aibu hata kidogo.....kweli IDs fake zinaficha mengi mno.
Dawa imekuingia
 
"Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, akatawale viumbe vyote".

Je, wingi kwenye hii nukuu unaiongeleaje?
Hiyo siyo mada ya hii thread.

Hata hivyo jibu ni kuwa wakati Mungu anaumba binadamu hakuwa peke yake.

Kulikuwa na viumbe wengine wa kiroho at least, ambao aliwaumba kabla.
 
Ni dhambi kubwa sana tena ni tusi kubwa sana na nidharau kubwa sana na ni kumvunjia heshima Mwenyzimungu kwa kumsingizia eti aliumba mtu kwa mfano wake, na kama yupo huyo mungu alie umba binaadam kwa mfano wake basi mungu huyo ni dhaifu sana kama alivyo dhaifu binaadamu.
Mimi naamini Mwenyezimungu sio dhaifu hivyo, huko ni kumtusi Mungu
Kwa hiyo msimamo wako ni upi?
Unamwamini Mungu ila hauamini kama binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu?
Kwani unaelewa nini kuhusu "Kuumbwa kwa mfano wa Mungu"?
Pengine una maana tofauti.
 
Kazi ya jinsia ndio sababu ya uwepo wake.
Jinsia ni mfumo kama mifumo myengine ktk mwili ambapo kila mfumo unakazi yake kuhusu swala la wapi jinsia imetoka ni ktk mfumo unaoratibu uundwaji wa mwili DNA lkn pamoja na hayo bado sayansi inaendelea kuchunguza nini chanzo cha hayo yote what we need is time.
naomba nikukumbushe kuwa sayansi hukua, leo wanaweza kukosa majibu lkn kesho wakapata kuwa mwangalifu usemapo "Hakuna sababu yoyote ya kisayansi inayoweza kuelezea kwanini...." nini kama ikiwezekana kueleza na ikawa proved..?

kuhusu bing bang na evolution siwezi kukuelezea how zimecreat gender coz binafsi sijaziamini bado na hazina prove kwamba zenyewe ndo source of life
Sayansi haitakuja kujua majibu ya maswali. Na ikija kuyajua itakiri kuwa kuna intelligence in creating all these! Which will directly prove that God exists.

Randomness can not create intelligence. Only intelligence creates intelligence.
 
1: kuna sababu za kisayansi kuhusu uwepo wa DNA na DNA ni nini na source yake kutoka katika simple Amino formula. DNA ndio kithibitisho kuwa wanadamu na viumbe vyote vimetoka katika line moja kwa sababu DNA inafanana katika kiwango fulani. DNA inatumika kulinganisha root ya ancestors kwa kulinganisha usawa. Hivyo ni kipingamizi cha kusema wanadamu na wanyama hapo kale waliumbwa tofauti.

2: Sababu ya kuzaliana ni sababu ya kila kiumbe duniani kuitwa kuimbe. Kila chenye uhai kina sifa saba za uhai ikiwepo reproduction. Ni sehemu ya uhai na characteristic ya uhai. Kama ilivyo kula, kuwa na sense, kutoa uchafu n.k

3: hakuna jinsia mbili katika kila kiumbe duniani. Vipo viumbe visivyo na jinsia. Kuna viumbe vina uwezo wa kuzaliana bila kuingiliana na kiumbe kingine hasa single cellular organisms, kuna viumbe vina both characters na kuna viumbe vina sexual mating kwa kuzaliana au kutaga mayai. Ukisoma historia ya mating imeelezewa kwa kiasi kikubwa sana kwenye sayansi na ushahidi wa viumbe vya mwazo kama bacteria vilivyoweza kuzaliana, mpaka kuja kwa viumbe vinavyotaga na kuja kwa viumbe vinavyozaa. Utajifunza kwa kina kuwa kuzaa au kutaga haikutokea tu mara moja kwa ghafla kama kuna mtu au nguvu iliamua bali ni kutokana na adaptation katika mazingira mbalimbali kama ilivyo adaptation ya skin colour.

4: mifumo ya mwili ukisoma vyema imeelezewa vyema katika kila evolutionary stage na kwanini hata organs zilizopo zipo katika location hiyo na pose na kila sababu ya ilivyo sasa.

5: Utashi wa mwanadamu sio kigezo cha kuwa ni bora sana kuliko wengine. Ni utashi uliotakana na hatua kwa hatua kuanzia kuweza kutumia moto, kula proteins nyingi katika bone marrows kwa sababu mwanadamu alikuwa scavenger na alitumia Oldowan stone tool kuanza kuvunja fat marrow ya mifupa. Akaweza kuongeza intake ya protein bila (unintentionally) na kuongezeka kwa cranial size kwenye kichwa na ubongo kuongezeka na kusaidia kuwepo kwa neuro connections nyingi na pia kutokana na kudevelop language (baada ya bipedalism thorax ilishuka na kuruhusu hewa kupita vyema kwenye voice box) na language ikamsaidia mwanadamu kushare informations, skills na ideas. Kuishi katika social life na primates wana sifa ya kuishi kama familia, kugundua moto kukamsaidia kulainisha nyama na kupunguza digestion time, kukapunguza vijidudu katika chakula na kusaidia uyeyushwaji kuwa effective na kutumia moto Homo erectus na Habilis wakaweza kusafiri na kwa mara ya kwanza mwanadamu akaweza kutoka nje ya Africa na kuishi hata katika mazingira ya baridi baada ya kujua kutumia moto, pia akajilinda na wanyama. Pamoja na tools zinasaidia kurahisisha kazi. Utashi ni series ya progress sio unakuta tu umeumbwa ukawa na utashi.

Pia wanyama wengine wana utashi wao mfano mwanadamu hana sense ya smell nzuri na kusikia vizuri kumlinganisha na paka au mbwa, na hiyo ni nature ya primates wote hata apes na monkeys hawana uwezo huo hivyo tulirithi kwa ancestors wetu.

Nyangumi, anaweza ku sense magnetic fields, nyoka na reptiles wanaweza kujua tetemeko kabla halijatokea kwa sense waliyonayo, sisi wanadamu hatuwezi. Kuna vingi wanadamu hatuwezi kutokana na evolutionary adaptation yetu hivyo sisi sio bora katika kila kitu.

Nakubaliana kidogo na mitazamo yako lakini kutokana na kutoelewa kwako na kushikilia udini na kukataa kujifunza unajikuta unadanganya na kusema sayansi haujaelezea.

Kutofahamu kwako sio sababu ya kusema hakuna wanaojua. Kabla ya ku assume ni vyema kusoma kwa kina kwanza au uliza usaidiwe. Kuna wataalamu na wanasayansi wazuri tu hata hapa J F.

Asante kwa mada yako nzuri.
 
Back
Top Bottom