1: kuna sababu za kisayansi kuhusu uwepo wa DNA na DNA ni nini na source yake kutoka katika simple Amino formula. DNA ndio kithibitisho kuwa wanadamu na viumbe vyote vimetoka katika line moja kwa sababu DNA inafanana katika kiwango fulani. DNA inatumika kulinganisha root ya ancestors kwa kulinganisha usawa. Hivyo ni kipingamizi cha kusema wanadamu na wanyama hapo kale waliumbwa tofauti.
2: Sababu ya kuzaliana ni sababu ya kila kiumbe duniani kuitwa kuimbe. Kila chenye uhai kina sifa saba za uhai ikiwepo reproduction. Ni sehemu ya uhai na characteristic ya uhai. Kama ilivyo kula, kuwa na sense, kutoa uchafu n.k
3: hakuna jinsia mbili katika kila kiumbe duniani. Vipo viumbe visivyo na jinsia. Kuna viumbe vina uwezo wa kuzaliana bila kuingiliana na kiumbe kingine hasa single cellular organisms, kuna viumbe vina both characters na kuna viumbe vina sexual mating kwa kuzaliana au kutaga mayai. Ukisoma historia ya mating imeelezewa kwa kiasi kikubwa sana kwenye sayansi na ushahidi wa viumbe vya mwazo kama bacteria vilivyoweza kuzaliana, mpaka kuja kwa viumbe vinavyotaga na kuja kwa viumbe vinavyozaa. Utajifunza kwa kina kuwa kuzaa au kutaga haikutokea tu mara moja kwa ghafla kama kuna mtu au nguvu iliamua bali ni kutokana na adaptation katika mazingira mbalimbali kama ilivyo adaptation ya skin colour.
4: mifumo ya mwili ukisoma vyema imeelezewa vyema katika kila evolutionary stage na kwanini hata organs zilizopo zipo katika location hiyo na pose na kila sababu ya ilivyo sasa.
5: Utashi wa mwanadamu sio kigezo cha kuwa ni bora sana kuliko wengine. Ni utashi uliotakana na hatua kwa hatua kuanzia kuweza kutumia moto, kula proteins nyingi katika bone marrows kwa sababu mwanadamu alikuwa scavenger na alitumia Oldowan stone tool kuanza kuvunja fat marrow ya mifupa. Akaweza kuongeza intake ya protein bila (unintentionally) na kuongezeka kwa cranial size kwenye kichwa na ubongo kuongezeka na kusaidia kuwepo kwa neuro connections nyingi na pia kutokana na kudevelop language (baada ya bipedalism thorax ilishuka na kuruhusu hewa kupita vyema kwenye voice box) na language ikamsaidia mwanadamu kushare informations, skills na ideas. Kuishi katika social life na primates wana sifa ya kuishi kama familia, kugundua moto kukamsaidia kulainisha nyama na kupunguza digestion time, kukapunguza vijidudu katika chakula na kusaidia uyeyushwaji kuwa effective na kutumia moto Homo erectus na Habilis wakaweza kusafiri na kwa mara ya kwanza mwanadamu akaweza kutoka nje ya Africa na kuishi hata katika mazingira ya baridi baada ya kujua kutumia moto, pia akajilinda na wanyama. Pamoja na tools zinasaidia kurahisisha kazi. Utashi ni series ya progress sio unakuta tu umeumbwa ukawa na utashi.
Pia wanyama wengine wana utashi wao mfano mwanadamu hana sense ya smell nzuri na kusikia vizuri kumlinganisha na paka au mbwa, na hiyo ni nature ya primates wote hata apes na monkeys hawana uwezo huo hivyo tulirithi kwa ancestors wetu.
Nyangumi, anaweza ku sense magnetic fields, nyoka na reptiles wanaweza kujua tetemeko kabla halijatokea kwa sense waliyonayo, sisi wanadamu hatuwezi. Kuna vingi wanadamu hatuwezi kutokana na evolutionary adaptation yetu hivyo sisi sio bora katika kila kitu.
Nakubaliana kidogo na mitazamo yako lakini kutokana na kutoelewa kwako na kushikilia udini na kukataa kujifunza unajikuta unadanganya na kusema sayansi haujaelezea.
Kutofahamu kwako sio sababu ya kusema hakuna wanaojua. Kabla ya ku assume ni vyema kusoma kwa kina kwanza au uliza usaidiwe. Kuna wataalamu na wanasayansi wazuri tu hata hapa J F.
Asante kwa mada yako nzuri.