Ushahidi kuwa binadamu tumeumbwa na hatujatokea tu

always am a Winner

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2012
Posts
230
Reaction score
193
Karibuni sana wana jamvi! Leo nataka kuwashirikisha sababu za msingi kabisa ambazo ni rahisi kuzithibitisha kuwa binadamu na viumbe wengine wote tumeumbwa. Nitaongelea binadamu zaidi ila nitawakilisha viumbe wengine pia. Kabla hatujaendelea napenda kwanza nitoe tofauti kati ya binadamu na mnyama.
Binadamu na mnyama wanatofautiana katika jambo moja tu; Binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Hii ina maana kuwa binadamu;
1. Anajitambua na
2. Anajua chema na kibaya
Mungu ameumba binadamu kwa sababu yake mwenyewe. Ameumba kila kitu for His own pleasure, and to demonstrate HIS extreme POWER and LOVE.
Hizi ni sababu TANO kwanini binadamu na viumbe vingine tumeumbwa;

1. DNA: Kila kiumbe kina instruction code inayokaa latika sehemu ndogo sana ya kila seli ya mwili. Manual hiyo ndiyo inaratibu kila kitu, yaani kila kitu. Kwa kifupi inaratibu maisha yote. Hakuna sababu za kisayansi za kuwa na DNA. Lakini Mungu ana majibu kwani biblia inasema, yeye ndiye aliyeweka sheria. Na pia aliumba kwa kutumia neno, yaani word au instruction.

2. Kuzaliana: Hakuna sababu yoyote ya kisayansi ya kwa nini viumbe huzaliana. Sayansi inaweza kueleza namna mfumo wa uzazi unavyofanya kazi lakini haiwezi kueleza kwanini kuna mifumo hiyo. Yaani haiwezi kueleza kwa nini kuna uzazi. Ila Biblia ina majibu,
"Zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha"

3. Jinsia: Hakuna sababu yoyote ya kisayansi inayoweza kueleza kwa nini kuna jinsia mbili, kwa nini kuna raha na siyo uchungu wakati wa kujamiiana, na kwa nini jinsia zote zipo katikati ya miguu. Kwanini jinsia moja isiwe sehemu nyingine mfano kichwani? Kwanini viumbe huwakwa tamaa ya kujamiiana?

4. Mifumo mbalimbali ya mwili inayofanya kazi kwa nia moja: Mfano mfumo wa upumuaji huungana na mfumo wa damu huungana na mfumo wa chakula huungana na mfumo wa usafishaji damu etc. Katika hali ya kawaida miguu haipishani urefu, mikono pia, moyo upo sehemu ileile ktk miili ya binadamu etc, Sayansi haina majibu ya kwanini mambo yapo hivo.

5. Utashi: Binadamu ana utashi wanyama hawana. Hakuna sababu ya kisayansi inayoweza kuelezea hili. Lakini Mungu anayo sababu;
"Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, akatawale viumbe vyote".

Kutokana na sababu hizi, ni wazi huwa Mungu ameumba binadamu na viumbe vyote.

Cc: Kiranga & the Company
 
Mkuu umeyachunguza vyema uliyoyaandika maana naona mapungufu mengi..?
eg.jinsia umesema hakuna sababu yoyote ya kisayansi ya kueleza kwanini kuna jinsia mbili, kwani hujui jinsia hizi mbili zipo ili kuzaliana na kwenye kuzaliana it makes uendelezwaji wa viumbe.
Raha wakati wa kujamiiana ipo ili kitendo cha kujamiana kiwepo means kusikia raha kwa viumbe hupelekea kuendelea kujamiia na wakijamiiana wanazaa kama kungekuwa nauchungu viumbe wasingependa kujamiiana.

Kabla ya mengine umesema huu ni ushahidi na ushahidi huwa na uthibitisho hebu nithibitishie kuwa hayo uloyataja hapo ni ushahidi kuwa binadamu ameumbwa..?
 
Hayo yote ulioandika yana majibu kwenye sayansi. Na hata kama hayana majibu au ufafanuzi haimaanishi kwamba mungu ndio ameyafanya. Hili ndio tatizo la watu wa dini. Mnatafuta kitu ambacho wanasayansi hawajakipatia ufafanuzi na kusema ni mungu ndio amefanya.
 
Kwa kweli JF ni 'Where we dare to talk openly'....Yaani mada kama hii ipo JF Intelligence?

Mleta mada kama ulitumia miaka 10+ Shuleni, inabidi urudishe gharama ulizozitumia.
 
Hii haina tofauti na ile mada yako ya sijui makosa mangapi ya Mungu.....

Nyani haoni ..........

Utamalizia hapo....
 
Karibuni sana wana jamvi! Leo nataka kuwashirikisha sababu za msingi kabisa ambazo ni rahisi kuzithibitisha kuwa binadamu na viumbe wengine wote tumeumbwa. Nitaongelea binadamu zaidi ila nitawakilisha viumbe wengine pia. Kabla hatujaendelea napenda kwanza nitoe tofauti kati ya binadamu na mnyama.
Binadamu na mnyama wanatofautiana katika jambo moja tu; Binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Hii ina maana kuwa binadamu;
1. Anajitambua na
2. Anajua chema na kibaya
Mungu ameumba binadamu kwa sababu yake mwenyewe. Ameumba kila kitu for His own pleasure, and to demonstrate HIS extreme POWER and LOVE.
Hizi ni sababu TANO kwanini binadamu na viumbe vingine tumeumbwa;

1. DNA: Kila kiumbe kina instruction code inayokaa latika sehemu ndogo sana ya kila seli ya mwili. Manual hiyo ndiyo inaratibu kila kitu, yaani kila kitu. Kwa kifupi inaratibu maisha yote. Hakuna sababu za kisayansi za kuwa na DNA. Lakini Mungu ana majibu kwani biblia inasema, yeye ndiye aliyeweka sheria. Na pia aliumba kwa kutumia neno, yaani word au instruction.

2. Kuzaliana: Hakuna sababu yoyote ya kisayansi ya kwa nini viumbe huzaliana. Sayansi inaweza kueleza namna mfumo wa uzazi unavyofanya kazi lakini haiwezi kueleza kwanini kuna mifumo hiyo. Yaani haiwezi kueleza kwa nini kuna uzazi. Ila Biblia ina majibu,
"Zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha"

3. Jinsia: Hakuna sababu yoyote ya kisayansi inayoweza kueleza kwa nini kuna jinsia mbili, kwa nini kuna raha na siyo uchungu wakati wa kujamiiana, na kwa nini jinsia zote zipo katikati ya miguu. Kwanini jinsia moja isiwe sehemu nyingine mfano kichwani? Kwanini viumbe huwakwa tamaa ya kujamiiana?

4. Mifumo mbalimbali ya mwili inayofanya kazi kwa nia moja: Mfano mfumo wa upumuaji huungana na mfumo wa damu huungana na mfumo wa chakula huungana na mfumo wa usafishaji damu etc. Katika hali ya kawaida miguu haipishani urefu, mikono pia, moyo upo sehemu ileile ktk miili ya binadamu etc, Sayansi haina majibu ya kwanini mambo yapo hivo.

5. Utashi: Binadamu ana utashi wanyama hawana. Hakuna sababu ya kisayansi inayoweza kuelezea hili. Lakini Mungu anayo sababu;
"Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, akatawale viumbe vyote".

Kutokana na sababu hizi, ni wazi huwa Mungu ameumba binadamu na viumbe vyote.

Cc: Kiranga & the Company
Naungana na wewe 100%,
 
Kwa kweli JF ni 'Where we dare to talk openly'....Yaani mada kama hii ipo JF Intelligence?

Mleta mada kama ulitumia miaka 10+ Shuleni, inabidi urudishe gharama ulizozitumia.
Acha utoto. Hujui kitu zaidi ya kushinda unauliza viswali vyako vya mtandaoni and not product of your own mental faculty.
 
Hii haina tofauti na ile mada yako ya sijui makosa mangapi ya Mungu.....

Nyani haoni ..........

Utamalizia hapo....
Kwahiyo umekubali aidha mada zote ni mbovu ama zina mashiko? Maana unasema haina tofauti.
 
Acha utoto. Hujui kitu zaidi ya kushinda unauliza viswali vyako vya mtandaoni and not product of your own mental faculty.
We umejuaje kwamba maswali yangu huwa sikifikirii mwenyewe?

Weka ushahidi wa ulisemalo..... Tofauti na hapo una guess tu kama unavyo guess uwepo wa Mungu.
 
Mkuu umeyachunguza vyema uliyoyaandika maana naona mapungufu mengi..?
eg.jinsia umesema hakuna sababu yoyote ya kisayansi ya kueleza kwanini kuna jinsia mbili, kwani hujui jinsia hizi mbili zipo ili kuzaliana na kwenye kuzaliana it makes uendelezwaji wa viumbe.
Raha wakati wa kujamiiana ipo ili kitendo cha kujamiana kiwepo means kusikia raha kwa viumbe hupelekea kuendelea kujamiia na wakijamiiana wanazaa kama kungekuwa nauchungu viumbe wasingependa kujamiiana.

Kabla ya mengine umesema huu ni ushahidi na ushahidi huwa na uthibitisho hebu nithibitishie kuwa hayo uloyataja hapo ni ushahidi kuwa binadamu ameumbwa..?
Mkuu huyu Mtu anashangaza sana.... Eti DNA ni ushahidi wa uumbaji wa Mungu, sasa mbona kuna natural errors nyingi sana kwenye DNA?.... Mbona kuna mutations?

Halafu anasema Mungu alimuumba Mtu akiwa na utashi wa kujua jema na baya, ili hali Kulingana na Bible Mtu alipata ufahamu wa jema na baya baada ya kuasi kwa kula matunda yaliyokatazwa....kwa hiyo Mungu alimuumba Mtu asiye na utashi na kama alimuumba kwa mfano wake, basi Mungu hana utashi wa kujua jema na baya unless na yeye alikula matunda ya mti wa katikati

Hoja nyingine hazina mashiko, eti science haijui Kwanini watu wanazaliana, eti science haijui Kwanini kuna jinsia mbili, eti science haijui Kwanini kuna mifumo mbalimbali mwilini...... Hahahaaaa dah! huyu jamaa ana matatizo makubwa mno.
 
Halafu na neno analitoa kwenye bible et zaeni mkaongezeke mkaijaze dunia! sasa mbona tunadanja..? tutaijaza lini sasa na tukiijaza inafaida gani..?hii ni hatari ya ubongo!
 
Pengine alikurupuka.....hawa watu wanakurupuka tu kongeaongea....hata tukirudi nyakati kabla ya kula tunda..... Hivi dunia ingekuwaje kama pasingekuwa na kifo?
 
Rudi tena kafanye reseach. Alafu huwe unasoma maandiko yako kabla hujayapost humu.
 
Ulimwengu wote huu na sayari zote hizi zingetumika kwa wanadamu. Hakuna linaloshindikana kwa Mungu.
 
Rudi tena kafanye reseach. Alafu huwe unasoma maandiko yako kabla hujayapost humu.
Hakuna nilipokosea andiko. Tofauti ipo katika interpretation yako. Toa sababu ya kisayansi za kwanini kuna jinsia.

Wengi hawajaelewa topic kwa sababu hawafikirii kwanza, werevu walio wachache wameelewa sana.
 
Mkuu umeyachunguza vyema uliyoyaandika maana naona mapungufu mengi..?
eg.jinsia umesema hakuna sababu yoyote ya kisayansi ya kueleza kwanini kuna jinsia mbili, kwani hujui jinsia hizi mbili zipo ili kuzaliana na kwenye kuzaliana it makes uendelezwaji wa viumbe.
Raha wakati wa kujamiiana ipo ili kitendo cha kujamiana kiwepo means kusikia raha kwa viumbe hupelekea kuendelea kujamiia na wakijamiiana wanazaa kama kungekuwa nauchungu viumbe wasingependa kujamiiana.

Kabla ya mengine umesema huu ni ushahidi na ushahidi huwa na uthibitisho hebu nithibitishie kuwa hayo uloyataja hapo ni ushahidi kuwa binadamu ameumbwa..?
Duh! Yaani umeandika pointless na bado kuna kiumbe ka like? Dah!

Hujajibu swali. Kwanini kumekuwa na jinsia? Sijauliza umuhimu wa jinsia.

Nimeuliza jinsia zimetoka wapi? How can big bang create gender? How can evolution creates gender?

Think Big!
 
Back
Top Bottom