always am a Winner
JF-Expert Member
- Nov 16, 2012
- 230
- 193
Karibuni sana wana jamvi! Leo nataka kuwashirikisha sababu za msingi kabisa ambazo ni rahisi kuzithibitisha kuwa binadamu na viumbe wengine wote tumeumbwa. Nitaongelea binadamu zaidi ila nitawakilisha viumbe wengine pia. Kabla hatujaendelea napenda kwanza nitoe tofauti kati ya binadamu na mnyama.
Binadamu na mnyama wanatofautiana katika jambo moja tu; Binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu. Hii ina maana kuwa binadamu;
1. Anajitambua na
2. Anajua chema na kibaya
Mungu ameumba binadamu kwa sababu yake mwenyewe. Ameumba kila kitu for His own pleasure, and to demonstrate HIS extreme POWER and LOVE.
Hizi ni sababu TANO kwanini binadamu na viumbe vingine tumeumbwa;
1. DNA: Kila kiumbe kina instruction code inayokaa latika sehemu ndogo sana ya kila seli ya mwili. Manual hiyo ndiyo inaratibu kila kitu, yaani kila kitu. Kwa kifupi inaratibu maisha yote. Hakuna sababu za kisayansi za kuwa na DNA. Lakini Mungu ana majibu kwani biblia inasema, yeye ndiye aliyeweka sheria. Na pia aliumba kwa kutumia neno, yaani word au instruction.
2. Kuzaliana: Hakuna sababu yoyote ya kisayansi ya kwa nini viumbe huzaliana. Sayansi inaweza kueleza namna mfumo wa uzazi unavyofanya kazi lakini haiwezi kueleza kwanini kuna mifumo hiyo. Yaani haiwezi kueleza kwa nini kuna uzazi. Ila Biblia ina majibu,
"Zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha"
3. Jinsia: Hakuna sababu yoyote ya kisayansi inayoweza kueleza kwa nini kuna jinsia mbili, kwa nini kuna raha na siyo uchungu wakati wa kujamiiana, na kwa nini jinsia zote zipo katikati ya miguu. Kwanini jinsia moja isiwe sehemu nyingine mfano kichwani? Kwanini viumbe huwakwa tamaa ya kujamiiana?
4. Mifumo mbalimbali ya mwili inayofanya kazi kwa nia moja: Mfano mfumo wa upumuaji huungana na mfumo wa damu huungana na mfumo wa chakula huungana na mfumo wa usafishaji damu etc. Katika hali ya kawaida miguu haipishani urefu, mikono pia, moyo upo sehemu ileile ktk miili ya binadamu etc, Sayansi haina majibu ya kwanini mambo yapo hivo.
5. Utashi: Binadamu ana utashi wanyama hawana. Hakuna sababu ya kisayansi inayoweza kuelezea hili. Lakini Mungu anayo sababu;
"Na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, akatawale viumbe vyote".
Kutokana na sababu hizi, ni wazi huwa Mungu ameumba binadamu na viumbe vyote.
Cc: Kiranga & the Company