Kuna mjamaa mmoja yupo ameajiriwa sehemu rasmi ana sifa zote za kuwa na mshahara usiopungua 3m kwenda juu .maana anayo master ya fedha na anayo CPA kapata mwaka juzi lkn mpk sasa analipawa laki 3 .alikuja kwangu kuniomba ushauri nikamwambia poa nitakupa.maana yeye anataka aache kazi ili ajiajiri mwenyewe.
Hebu tumpe ushauri huyu mjamaa kabla ya kuacha kazi asije kufa njaa
1.Jamaa yako ni kilaza plus.
2.Hana jipya lolote analoongeza kwenye kampuni, ni kati ya wale ambao huwa wanaitwa "seat warmers", he does not add any value to the company.
3.Watu huwa hawalipwi kwa thamani ya vyeti/elimu zao au uzoefu, bali huwa
wanalipwa directly proportional to the value they add to the company.
4.Kwa sababu ya namba moja na namba mbili hapo juu, hata akijiajiri the chances are, hatafanikiwa katika huko kujiajiri, maana principles ni zile zile.
5.Hapo halipo hawawezi kumlipa milioni 3 maana wanaona yeye thamani anayoongeza kwenye kampuni ni laki 3 tuu..!!
Afanye nini?:
1.Ajiulize kwa kujifanyia self evaluation, je kwenye kampuni anayofanya kazi, what value does he add?
2.Kila siku wakati anaingia ofisini, ajiulize leo ataongeza faida gani kwenye kampuni, na wakati wa kutoka ajiulize ameongeza faida gani kwa kampuni?
3.Aache kufanya kazi kwa mazoea kwamba yeye ana CPA sijui ana masters, aongeze ubunifu kwenye kazi yake, awe bora zaidi ya jana kila siku na ahakikishe kila siku anajifunza jambo jipya ya namna gani anaweza kuboresha kazi yake.
4.Afanye hayo matatu religiously kwa muda wa miezi 3-6,
5.Baada ya hapo, aanze kuomba kazi mbalimbali sehemu nyingine-Kwenye CV yake ahakikishe ame-include quantifiable achievements ambazo ameweza kufanikisha in his current position. Hapo, akipata nafasi kampuni nyingine, kama kweli alifanya kwa ufanisi hatua namba 1 hadi 3 nilizoandika hapo juu, lazima akituma tu resignation letter, watamuita kwa maongezi na kumwambia wayajenge, hapo sasa ndo anataja hizo 3m; Wakiwa tayari sawa, wakichomoa anaenda zake huko alikopata.
Kukudume2013