Ushauri: Ana CPA analipwa laki tatu anataka aache kazi

Ushauri: Ana CPA analipwa laki tatu anataka aache kazi

Kukudume2013

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
1,659
Reaction score
734
Kuna mjamaa mmoja yupo ameajiriwa sehemu rasmi ana sifa zote za kuwa na mshahara usiopungua 3m kwenda juu .maana anayo master ya fedha na anayo CPA kapata mwaka juzi lkn mpk sasa analipawa laki 3 .alikuja kwangu kuniomba ushauri nikamwambia poa nitakupa.maana yeye anataka aache kazi ili ajiajiri mwenyewe.

Hebu tumpe ushauri huyu mjamaa kabla ya kuacha kazi asije kufa njaa
 
Aendelee kubukua... Hajafika mwisho aendelee kusoma huku akichapa kazi... Mambo mazuri hayaitaji haraka...
 
Mie tokea nilivyograduate nikaitwa Graduate Engineer bado sikuona kuwa kuna chakula kinajileta Mezani chenyewe.
Bado naambiwa kuwa inatakiwa uandikishwe Kama Professional Engineer nikajiuliza kuwa kwa iyo hapa ndo maisha yatalainika Sana sawa na kufumbua jipu lililoiva.

Kwanza niliambiwa kuwa Soma nikasoma mpaka chuo bado nikaona maisha ni kuhangaika tu na Wala hayajalainika inabidi ukomae usiku na mchana Kama wataka zaidi ya kulipia bills zako.

Nikawaza kuwa ukishakuwa na mhuri erb bado utakuwa unawapa watu hela kule wanakula za bure sijui kisa ndo wanakupa mhuri.
Nikasema kuwa hapa nilipofikia Kama haitoshi kuyaona hayo maisha mazuri basi hata nikiwa na mhuri hakuna kitaakachokuja bure.
Kuna mtu Ana pe yupo na wahindi na jamaa ni mzima mie ni kilaza kwake zaidi ya Mara Mia.

Ila wahindi wanamlipa laki nane kwa mwezi mpaka huruma. Anadai Kuna muda anasimamia design ya structures Fulani afu kampuni inalipwa 200M afu yeye anaambulia laki 8 kwa akili yake ujue.

Msomi na mkulima ni watu wa kupangiwa Kama watoto ama wanafunzi. Yaani unalima na unasoma kwa juhudi zako afu unapangiwa utauzaje ama utalipwaje Bei gani.hata mazao hayo utauzia wapi usipeleke nje.yaani ni mwendo wa utumwa.

Bado ukifanya kazi unaambiwa kuwa wewe ni mtt utajisahau kujitunza utakapostaafu so lete tukutunzie hela zako utakapoacha kazi tutakuwa tunakupa kidogo kidogo mpaka ufe Mana ulishazoea kutunzwa Kama mtt.

Haya maisha niliyachukiaje. Yaani unitunzie hela zangu Kama pension mbona wabunge wao hamwatunzii ama una mpango wa kunifanya niwe tegemezi mpaka naingia kaburini.

Nikaona sio Aina ya maisha niliyokuwa nayawaza nilipokuwa mdogo. Nashukuru mpaka saivi sijatunziwa hela na hao wanaonipenda nimejitunzia mwenyewe.
 
Kuna mjamaa mmoja yupo ameajiriwa sehemu rasmi ana sifa zote za kuwa na mshahara usiopungua 3m kwenda juu .maana anayo master ya fedha na anayo CPA kapata mwaka juzi lkn mpk sasa analipawa laki 3 .alikuja kwangu kuniomba ushauri nikamwambia poa nitakupa.maana yeye anataka aache kazi ili ajiajiri mwenyewe.
Hebu tumpe ushauri huyu mjamaa kabla ya kuacha kazi asije kufa njaa
1.Jamaa yako ni kilaza plus.
2.Hana jipya lolote analoongeza kwenye kampuni, ni kati ya wale ambao huwa wanaitwa "seat warmers", he does not add any value to the company.

3.Watu huwa hawalipwi kwa thamani ya vyeti/elimu zao au uzoefu, bali huwa wanalipwa directly proportional to the value they add to the company.

4.Kwa sababu ya namba moja na namba mbili hapo juu, hata akijiajiri the chances are, hatafanikiwa katika huko kujiajiri, maana principles ni zile zile.

5.Hapo halipo hawawezi kumlipa milioni 3 maana wanaona yeye thamani anayoongeza kwenye kampuni ni laki 3 tuu..!!
Afanye nini?:

1.Ajiulize kwa kujifanyia self evaluation, je kwenye kampuni anayofanya kazi, what value does he add?

2.Kila siku wakati anaingia ofisini, ajiulize leo ataongeza faida gani kwenye kampuni, na wakati wa kutoka ajiulize ameongeza faida gani kwa kampuni?

3.Aache kufanya kazi kwa mazoea kwamba yeye ana CPA sijui ana masters, aongeze ubunifu kwenye kazi yake, awe bora zaidi ya jana kila siku na ahakikishe kila siku anajifunza jambo jipya ya namna gani anaweza kuboresha kazi yake.

4.Afanye hayo matatu religiously kwa muda wa miezi 3-6,

5.Baada ya hapo, aanze kuomba kazi mbalimbali sehemu nyingine-Kwenye CV yake ahakikishe ame-include quantifiable achievements ambazo ameweza kufanikisha in his current position. Hapo, akipata nafasi kampuni nyingine, kama kweli alifanya kwa ufanisi hatua namba 1 hadi 3 nilizoandika hapo juu, lazima akituma tu resignation letter, watamuita kwa maongezi na kumwambia wayajenge, hapo sasa ndo anataja hizo 3m; Wakiwa tayari sawa, wakichomoa anaenda zake huko alikopata.
Kukudume2013
 
Nitammwabia lkn ameniambia yeye hapo ktk ofc ya serikali anategemewa sana sana hasa ktk kuandaa maheaabu ya mwaka na ni mtaalamu sana maana anajua sana kompiter ana jua mifumo ya fedha kisawasawa.na kashajitahidi sana kutaka kuhama hapo alipo lkn ofc yake imemkazia akiandika barua ya kuhama wanamkatalia katakata.anatokaje hapo?
Mie tokea nilivyograduate nikaitwa Graduate Engineer bado sikuona kuwa kuna chakula kinajileta Mezani chenyewe.
Bado naambiwa kuwa inatakiwa uandikishwe Kama Professional Engineer nikajiuliza kuwa kwa iyo hapa ndo maisha yatalainika Sana sawa na kufumbua jipu lililoiva.
Kwanza niliambiwa kuwa Soma nikasoma mpaka chuo bado nikaona maisha ni kuhangaika tu na Wala hayajalainika inabidi ukomae usiku na mchana Kama wataka zaidi ya kulipia bills zako.
Nikawaza kuwa ukishakuwa na mhuri erb bado utakuwa unawapa watu hela kule wanakula za bure sijui kisa ndo wanakupa mhuri.
Nikasema kuwa hapa nilipofikia Kama haitoshi kuyaona hayo maisha mazuri basi hata nikiwa na mhuri hakuna kitaakachokuja bure.
Kuna mtu Ana pe yupo na wahindi na jamaa ni mzima mie ni kilaza kwake zaidi ya Mara Mia.
Ila wahindi wanamlipa laki nane kwa mwezi mpaka huruma.
Anadai Kuna muda anasimamia design ya structures Fulani afu kampuni inalipwa 200M afu yeye anaambulia laki 8 kwa akili yake ujue.
Msomi na mkulima ni watu wa kupangiwa Kama watoto ama wanafunzi.
Yaani unalima na unasoma kwa juhudi zako afu unapangiwa utauzaje ama utalipwaje Bei gani.hata mazao hayo utauzia wapi usipeleke nje.yaani ni mwendo wa utumwa.
Bado ukifanya kazi unaambiwa kuwa wewe ni mtt utajisahau kujitunza utakapostaafu so lete tukutunzie hela zako utakapoacha kazi tutakuwa tunakupa kidogo kidogo mpaka ufe Mana ulishazoea kutunzwa Kama mtt.
Haya maisha niliyachukiaje. Yaani unitunzie hela zangu Kama pension mbona wabunge wao hamwatunzii ama una mpango wa kunifanya niwe tegemezi mpaka naingia kaburini.
Nikaona sio Aina ya maisha niliyokuwa nayawaza nilipokuwa mdogo.
Nashukuru mpaka saivi sijatunziwa hela na hao wanaonipenda nimejitunzia mwenyewnit
 
Nitammwabia lkn ameniambia yeye hapo ktk ofc ya serikali anategemewa sana sana hasa ktk kuandaa maheaabu ya mwaka na ni mtaalamu sana maana anajua sana kompiter ana jua mifumo ya fedha kisawasawa.na kashajitahidi sana kutaka kuhama hapo alipo lkn ofc yake imemkazia akiandika barua ya kuhama wanamkatalia katakata.anatokaje hapo?
Hakuna mhasibu wa serikali mwenye CPA anayelipwa laki 3. Hapo unatudanganya.
 
Kuna mjamaa mmoja yupo ameajiriwa sehemu rasmi ana sifa zote za kuwa na mshahara usiopungua 3m kwenda juu .maana anayo master ya fedha na anayo CPA kapata mwaka juzi lkn mpk sasa analipawa laki 3 .alikuja kwangu kuniomba ushauri nikamwambia poa nitakupa.maana yeye anataka aache kazi ili ajiajiri mwenyewe.
Hebu tumpe ushauri huyu mjamaa kabla ya kuacha kazi asije kufa njaa
Wakati nafanya tafiti fulani flani, nilikutana na point muhimu sana; Kuwa
Mshahara wa mtu hutegemea vitu kadhaa muhimu sana

1. Production ya muhusika mf: Kama mtu ana CPA halafu anafanya kazi ya mtu wa Cheti ina maana mshahara wake utafanana fanana namtu wa Cheti au Niseme Elimu yake haijaleta tija kwenye Shirika husika hivyo hawaoni umuhimu kumpandisha
2. Uwezo wa shirika/Kampuni wa kulipa. mf: ukiomba kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza chakula cha Paka ambapo mkurugenzi analipwa laki 5; hata kama una CPA usitegemee kulipwa zaidi ya mkurugenzi
3. Elimu yake

Ukiangalia hapo utaona kuwa Elimu ni namba tatu; inamaana atumie namba moja na namba mbili kwenye mipango yake;
Ushauri:
1. Aombe kazi inayo endana na Elimu yake; inaweza kuwa kwenye shirika hilo hilo ila afanye kazi inayofanana na elimu yake au ambayo anaweza kuonesha elimu yake (umuhimu wake kwa shirika)
2. Kama shirika haliwezi kumlipa au halina nafasi aombe kazi shirika linalo hitaji watu wa level yake na achape kazi kwelikweli
3. Muhimu zaidi, mashirika mengi hasa ya binafsi, cheti kina nafasi kama 50% tu na 50% iliyobaki ni uwezo wa kufanya kile ulicho omba kwa usahihi na pia kwenda extra mile

Muhimu pia: Anaweza kuomba kazi mahali pengine ila akiwa anaendelea na kazi hapo hapo; akisha pata ndio aache
 
Kuna hela ya kulipwa na hela ya kujilipa, jaribu kuchunguza tena anajilipa kiasi gani
 
Mshahara ni mapatano baina ya mwajiri na mwajiriwa, mshahara sio hisani wala msaada, kama mwajiriwa anaona mshahara huo hauendani na ujuzi na elimu yake, njia rahisi ni kuongea na mwajiri ili mshahara upande, na wakishindana ni vyema akafikiria kuacha hiyo kazi ili akafanye kazi itakayomfaa.
 
Mie tokea nilivyograduate nikaitwa Graduate Engineer bado sikuona kuwa kuna chakula kinajileta Mezani chenyewe.
Bado naambiwa kuwa inatakiwa uandikishwe Kama Professional Engineer nikajiuliza kuwa kwa iyo hapa ndo maisha yatalainika Sana sawa na kufumbua jipu lililoiva...
Nishaushtukia huu mchezo yani natakiwa kuzeeka nasoma ili nipewe vyeti na kutambuliwa na bodi. Nimeanza darasa la kwanza mwaka 2006 mpaka leo nasoma weee alafu ukute nikiajiriwa nitalipwa hela ya kunifanya nisife, hiyo hiyo wakate kodi, wanitunzie na niwalipe bodi eti sijui wanisimamie na niwalipe HESLB. Sasa kama miaka 15 ambayo nimesoma mpaka leo ina tija kidogo hivi kuna haja gani ya kuongeza sijui Master's. Kwanza nyumbani kuna Master's na hazina maisha.

Ukitumia source kama YouTube, Google, WordPress na Udemy kwa elimu ya form six na akili zinazofundishika unaishi maisha. Uzuri wa internet unasoma unachokitaka kwa muda huo, sasa syllabus unasoma takataka kibao.

Kuna watu nilikuwa nakaa nao darasani tusome Projectile Motion ila leo wanasoma MD, sasa kutibu figo na kufyatua maroketi vina uhusiano gani. Lakini kwa ajili ya vyeti tusome formal education, kwa ajili ya mafanikio tujiongeze
 
1.Jamaa yako ni kilaza plus.
2.Hana jipya lolote analoongeza kwenye kampuni, ni kati ya wale ambao huwa wanaitwa "seat warmers", he does not add any value to the company.
3.Watu huwa hawalipwi kwa thamani ya vyeti/elimu zao au uzoefu, bali huwa wanalipwa directly proportional to the value they add to the company...
Sure we don't pay you by hour but what you add or produce for that an hour.

Zalisha 100TZS tukulipe 1TZS ndo maisha ya msomi. Yaani nikikumbuka la sita naenda shule sifiki bro ananilazimisha shule. Huku muda huo nishakuwa chinga mzoefu I know how to produce money
 
Nishaushtukia huu mchezo yani natakiwa kuzeeka nasoma ili nipewe vyeti na kutambuliwa na bodi. Nimeanza darasa la kwanza mwaka 2006 mpaka leo nasoma weee alafu ukute nikiajiriwa nitalipwa hela ya kunifanya nisife...
Sure formal education can give you a living but self education gives you fortune
 
Pole yake sana...

Wenzake wanalipwa Million4.5 take home...
 
Pole yake sana...

Wenzake wanalipwa Million4.5 take home...

Watu wengi wenye taaluma za uhasibu wanalipwa vizuri sana.. ila ni wale majembe..

Mhasibu ambaye ana nafasi kubwa ya kulipwa vizuri kwenye soko la ajira ni yule aliyeanzia kazi big 4 auditing firms..

Hao watu wanajua kazi za uhasibu sana.. hizo kampuni pwc, delloite, ernst and young, kpmg zinawaandaa wahasibu wazuri sana. Na hao ndio wanalipwa vizuri wakitoka hizo big 4
 
Back
Top Bottom