Ushauri: Anataka kuacha kazi Serikalini sababu ya maslahi madogo

Huu uongo
 
Mwanao ni muongo,
1.baada ya super speciality in cardiology hakuna internship
2.Ili uwe cardiologist inachukua zaidi ya miaka 10,MD=5,MMED=3,MSc Cardiology =2,hakuna mtu aliyemaliza supercialist hapa bongo akakosa KAZI ya kufanya ama hajui cha kufanya
Muulize vizuri,alisoma nini huyo mwanao na kabla ya kwenda the so called India,alikua ana elimi gani
 
Hapa mdau umeongea ukweli mtupu aisee,🤣🤣
 
Kuajiri watu wanaotoka kwenye jamii husika kunadumaza eneo husika.

Angalia baadhi ya halmashauri kongwe haziendelei kwa tabia hiyo.
 
Kuna jamii sio za kutangamana nazo yaani yafaa waajiriwe wa kulekule
 
Afanyekazi kwa malengo, kumbuka kwamba ajira ni sehemu pia yakujipatia mtaji wakufanya biasha, hususani ajira za serikalini, kwanza angalee fursa kwenye maeneo yanaomzunguka.
 
Kuna jamii sio za kutangamana nazo yaani yafaa waajiriwe wa kulekule
Kuna sehemu inaitwa Nana iko mpakani na wilaya ya Kilosa na Gairo ila ni rahisi kufika Kidete Kilosa kwa pikipiki.

Pale nilinunuwa mgodi wa Moonstone na nikakaa kambini na timu yangu.

Kiasili sehemu zenye madini hakuna maji, maji na madini havikai pamoja.

Kuagiza maji mwanakijiji namtuma alfajiri na punda anarudi saa 10 jioni imagine na hayo maji si salama naweka water guard.

Katika kupelekeza hawa watu wanaishi vipi natafuta mihogo ya kuchemsha kunywea chai kwanza nikapata sehemu ya kuchaji simu kuna kilabu cha pombe.

Kuna kitu sikuelewa ilibidi niulize mbona kila anayekuja kunywa ana kibegi mgongoni? Ndio nikaambiwa huku watu hawana pesa wanaleta mahindi wanapewa pombe.

Hayo maeneo kwanza yana baridi kali halafu maji hakuna mtu kukaa wiki bila kuoga ni kawaida na mvua ikinyesha ni neema, sasa imagine mwalimu amekulia Dar unamtupa hapo ni mateso matupu, mimi nilirudi mjini mweusi tii.
 
Maisha ya kijijini mazuri sana nimezaliwa kijijini, nimesomea kijijini na mitikasi mingi nimefanyia kijijini napakubali kinoma huku mjini nililoea after chuo

Sio kila mtu atakuwa tajiri na concept ya mafanikio ni perception za mtu na malengo aliojiwekea

Wengi wenye malengo na mindoto mikubwa huishia kuwa masikini wa kutupwa na hopeless ni bora ukaishi uhalisia

Aache kazi asiache kazi uhalisia wa maisha yake utabaki vile vile hakuna kitakacho badilika
 
Wazo zuri sana
 
Hatari dogo ana degree ya nn?jaribu kumtia moyo mkuu ukimuacha hata potea.
 
Wakati nipo field Mwalimu mmoja alinambia kuwa

Upo willing kuwa Mwalimu ?

Nikamwambia yes

Akasema huku chakula, sehemu ya kulala uhakika Ila mambo makubwa makubwa haiwezekani kiyafikia kirahisi.

So na Kama UPO ndani ndani kijijini lazima uone hali IPO hivyo.


So fanya mahesabu vizuri ujue kipi hasa ukifanya kitakupeleka mbele na kipi hasa ukifanya kitakupa furaha.

All the best
 
Wewe huelewi hata ulichokiandika, vijiji vya Tanzania vinafanana?

Kuna mwalimu anaweza kulalamika yupo Uchagani mazingira magumu? Vijiji vina umeme na maji tangu mkoloni na walimu na mapadre wanaheshimika sana.
 
Katika hali hiyo,je hajaona fursa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…