well, mkuu swali zuri sanaa, kisheria hiko hivi, kuna makosa ambayo yanapelekwa mahakama kuu tu kama mauaji, uhaini, ufisadi wa pesa kubwa na madawa ya kiasi kikubwa lakini pia nyara za serikali, sasa makosa haya yote ni jinai, na kwa mujibu wa sheria za jinai hakuna kesi yoyote itakayopelekwa mahakama kuu moja kwa moja pasipo kupitia mahakama ya wilaya au hakimu mkazi, lengo na maudhui ni kukamilisha ushahidi na utaratibu wote utakao tumika mahakama kuu.
kwaio utaona mshtakiwa anaambiwa na hakimu kua "mshitakiwa mahakama hii haina uwezo wa kusikiliza kesi hii, hapa imekuja kwa maulizo na hautopaswa kusema chochote",,, sasa akishaambiwa hivi upande wa mashtaka/jamhuri utamsomea orodha ya mashahidi watakao toa ushahidi wao mahakama kuu, utamsomea vile vile vizibiti vitakavyotumika kama ushahidi, hatua hii kisheria huitwa PI-Preliminary Inquiries, then wakimaliza utaritibu huu, file linachukuliwa kama lilivyo linapelekwa mahakama kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa rasmi.
sasa kisheria ktk masikilizo ya kesi yoyote ya jinai ni lazima kuwe na masikilizano ya awali ambayo huitwa Preliminary Hearing ambapo hii ina dhima ya kusave muda ambapo kuna vitu mshitakiwa ata vikubali na havitazungumziwa tena kwenye kesi na kuna document hapa inaitwa Memorundum of agreed facts itasainiwa na mshitakiwa.