GWAJIMA NA MKAKATI HATARI WA MGAMBO WA MSITUNI - JE KUNA TAFSIRI GANI KWA MAFUGULI KUTUMIA NGUVU HADI MISHIPA KUMTOKA KUMPIGIA KAMPENI HADI ANAFOKA NA KULIAA???KUNA SIRI GANI
March 3 ·
Askofu Gwajima ahojiwa na Polisi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemuhoji Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima, kwa tuhuma za kusambaza kipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma zenye lengo la kuhamasisha watu kuunda kikundi cha kikabila nchini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, -Camillius Wambura amesema kuwa, kipeperushi hicho chenye picha ya Rais John Magufuli kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kikiwa na maandishi yanayosomeka kwa lugha ya kisukuma.
Ameongeza kuwa, Askofu Gwajima pia ametoa ujumbe wa sauti unaompongeza Rais na kuhamasisha wasukuma kurejesha utamaduni wao wa zamani wa kutumia lugha yao, kusaidiana katika shida na raha na kuwataka wasukuma kuunda vikundi kwenye mitandao ya kijamii vya watu elfu mbili kwa lengo la kufuatilia watu wanaomtukana Rais Magufuli na kuwashughulikia.
Katika ujumbe huo wa sauti Askofu Gwajima amewataka wasukuma wenye uwezo wa kifedha kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuwasaidia wasukuma wasiojiweza ili kuondoa dhana ya kwamba wasukuma ni masikini na ni washamba.
Kufuatia jumbe hizo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemuhoji askofu Gwajima kutokana na jumbe hizo kuonekana kuhamasisha vitendo vya kikabila jambo ambalo linaweza kuwagawa Watanzania na kupelekea kuvunjika kwa amani na mshikamano wa Taifa utakaotokana na uwepo wa matabaka ya kikabila.
Baada ya mahojiano hayo, Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limemuonya Askofu Gwajima kuacha mara moja vitendo vya kuligawa Taifa kwa kutumia vigezo vya ukabila na kutoa onyo kwa wote wenye nia ya kutaka kuligawa Taifa kwa njia ya ukabila, udini au ukanda.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi nchini imesema kuwa jeshi hilo halitamuonea haya mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya aina hiyo na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Limewataka Watanzania wote kuendeleza umoja na mshikamano uliopo bila kujali dini, kabila wala rangi ya mtu kama ambavyo baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyopinga vitendo vya kibaguzi na kuliunganisha kwa lugha ya Kiswahili.
#tbcfmhabari#tbcfmtz #updates