USHAURI: Halima Mdee na wenzake wafukuzwe CHADEMA

USHAURI: Halima Mdee na wenzake wafukuzwe CHADEMA

Kuna uwezekano hata wakifukuzwa uanachama ndugai akawalinda waendelee kihudhuria bungeni, ref yule mbunge alievuliwa ubunge lakini ndugai alimkingia kifua na aliendelea kuhudhuria bunge
Hii kweli kabisa, lakini hao wanawake kufukuzwa ni mjadala mzito
 
Huyu jamaa na ICC ni kama pete na kidole[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yaani kila sehemu anatishia ICC ICC baada ya ile"Ni Yeye" kubuma.
Wa hivi ukifukua makaburi utakuta 2015 pia alitisha watu na ICJ. Wameshapoteza mwelekeo, ni maombi tu yanaweza kuwaokoa na huu udhalilishaji wanaojifanyia
 
Nimeona Halima Mdee na kundi lake wakila kiapo kwa spika wa bunge kama wabunge wa viti maalumu CHADEMA, kama kweli wamerubuniwa na CCM na hatimaye kula kiapo bila kuwa na ridhaa ya chama wafukuzwe unachama Mara mmoja.

Hii itasaidia kujenga nidhamu ndani ya chama. Ni bora kujenga chama upya kuliko kuwa na watu wasio na nidhamu ndani ya chama.

Ifahamike kuwa chama hiki ni mali ya wanachama na si watu wachache. Kuna watu tumepoteza kazi serikalini kwa sababu ya kukipigania chama.

Narudia kama wamekengeuka na kula kiapo bila ridha ya chama ,basi wafukuzwe wote Mara moja bila kujali jina la MTU.

Utakuwa na mtindio wa akili

Unamwamini nani chadema?
 
Wa hivi ukifukua makaburi utakuta 2015 pia alitisha watu na ICJ. Wameshapoteza mwelekeo, ni maombi tu yanaweza kuwaokoa na huu udhalilishaji wanaojifanyia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na wanaonaga kushabikia chadema ni ujanja kweli

Ona sasahivi wanavyotia huruma[emoji38]

Sasahivi ameweka matumaini yake huko ICC
Yaani jamaa analala anaamka yuko na ICC tu[emoji38]
 
Mliambiwa muandamane ili waingie bungeni mliandamana ? Acha wakale mema ya nchi ! Uchaguzi umekwisha !!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Eti mliambiwa wakat wewe ni mfuasI mmoja wapo !Sema tuliambiwa, waliambiwa akina Nani ?

Hivi Mbona watu wanakataa humu kulikoni
 
Watanzania tukubaliane kwamba maumivu yetu yapo moyoni lakini bado ayajaanza kuandamana na matendo. Natambua Watanzania walivyomuunga moono Tundu Lisu ikiwa ni pamoja na kugharamia kampeni zake kwa kidogo walichokuwa nacho.

Kabla Tundu Lisu ajaingia hapa nchini kila mmoja wetu aliamini upinzani Tanzania umekufa lakini alipowasili hali ya siasa ilibadilika na kwa kuwa ccm awakuajiandaa kwa uchaguzi ilibidi wabadili gia na kuotumia tume na dola kufanya yaliyotokea.

Baada ya matokeo tuliuzunika sana na uzun yetu haiwezi kuondoka leo Wala kesho. Tutazidi kuumia na kuumia ndani mwetu huku tukiwapeleka wanetu shule, tukiiweka nchi kwenye ibada ipate ukombozi na tukiendelea na maisha yetu binafsi.

Hakuna Kati yetu asiyejua kwamba mihimili yetu kwa sasa haitendi haki, kila mtu katika nafasi yake anaangalia uhai wa familia yake hadi pale Taifa litakaporejeshwa mikononi mwa wanaotambua amani ni zao la amani.

Upo wakati unaweza ukajidanganya kwamba Halima mdee na wenzake wangeweza kugomea Bunge, hata Mimi nilitamani iwe hivyo. Ila nilipotamani iwe hivyo nafsini mwangu ilinipasa kuchukua hatua kuwaunga mkono kupigania haki. Hakuna Kati yetu aliyethubutu kusimama na kusema anawatete bali tulikaa majumbani kwetu kuomba waendelee kupata ujasiri wakususa.

Wao wana familia na yamkini amani ya familia zao imepelekea wao kuwa na afya Bora ya akili ya kututetea sisi. Tuwape nafasi watutetee japo kwa Yale machache watakayofanikiwa kuyafanya.

Tunapoona wanaingia Bungeni iwe faraja kwetu kwamba at least wapo watu ambao wanaweza kusukuma agenda ya mabadiliko itakayomwezesha mwanao kukua na kufikia kiwango Cha kupokea kijiti Cha mabadiliko kutoka kwa wapiganaji Hawa.

Tazama ccm wanavyoshangilia utagundua wazi kwamba hata wao ushindi walioupata haukiwa wa haki. Tazama namna walivyopokelewa bungeni na walivyoapishwa kinyemela utagundua hakukuwa na haki. Lakini hakuna Kati yetu aliyenyoosha mkono kwa tume ya uchaguzi Wala Bunge kulaani uovu wanaofanya. Hii inatafsiri kubwa sana kwetu, hatujadili hoja bali tumejikita kujadili watu.

Siku tukianza kuona kuwa tatizo la Taifa letu siyo watu Bali ni mfumo tutakua tumefikia kiwango chakuidai Tanzania huru aliyoieleza Lisu.

Halima na wenzake niwana mabadiliko wanaotumia umri wao kutengeneza njia yakuelekea Tanzania huru, tusibeze njia wanazotumia bali tuwasaidie kujenga mfumo utakaowawezesha kulifikia lengo.
 
Ni wakati wenu huu wa kufurahi na kuongea kebehi zote. Ila kumbukeni tu kila jambo na wakati wake. Endeleeni kufurahi mkijua yameisha ila napenda tu kuwaambia kuwa mapambano ndo kwanza yanaanza.

Tunachofurahi ni kuwa mnazidi kutuondolea wanafiki na watu wanaojali matumbo yao wala si maslahi mapana ya watanzania.

Napenda kuwahakikishia, hakuna marefu yasio ya ncha. Wakati wenu wa kilio na kujuta upo na utafika.

Hamtaweza kuturubuni wote na wengine tutasimama kuwatetea kweli watanzania
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na wanaonaga kushabikia chadema ni ujanja kweli

Ona sasahivi wanavyotia huruma[emoji38]

Sasahivi ameweka matumaini yake huko ICC
Yaani jamaa analala anaamka yuko na ICC tu[emoji38]
Nani anatia huruma??? Mbona unawaongelea watu wakati wako sawa na wala hawana shida yeyote??
 
Ni wakati wenu huu wa kufurahi na kuongea kebehi zote. Ila kumbukeni tu kila jambo na wakati wake. Endeleeni kufurahi mkijua yameisha ila napenda tu kuwaambia kuwa mapambano ndo kwanza yanaanza.

Tunachofurahi ni kuwa mnazidi kutuondolea wanafiki na watu wanaojali matumbo yao wala si maslahi mapana ya watanzania.

Napenda kuwahakikishia, hakuna marefu yasio ya ncha. Wakati wenu wa kilio na kujuta upo na utafika.

Hamtaweza kuturubuni wote na wengine tutasimama kuwatetea kweli watanzania
Wacha bwana [emoji23]
Leo halima amekuwa si kamanda tena?[emoji1787]
Tena mkiwafukuza tu, chama kinawafia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom