Ushauri: Hataki kuolewa na mimi, anaogopa kuchekwa kuolewa na "asiyesikia"

Ushauri: Hataki kuolewa na mimi, anaogopa kuchekwa kuolewa na "asiyesikia"

Pole sana huyo hakupendi ila anapenda Pesa zako, achana naye Mungu atakupatia wakuendana naye.
 
Mimi nina tatizo linalofanana na lako kwa kiasi fulani, nina tatizo linaitwa tinnitus nilipata nikiwa form one 2007. Nilipoteza uwezo wa kusikia kwa 80%.

Kwa experience yangu sidhani kama its a big issue maana nishakua na relationship kibao tu since niko secondary mpaka chuo na mpaka sasa walikua mademu wananielewa sana and the ladies didn’t give a shit about my problem. Na saiv nna pisi moja kali sana tunaoana mwaka huu, tena ni mdada mzuri haswa.

I can say uyo dada hakupendi tu. Pia jiamini na tafuta pesa, narudia tena make sure uko na pesa. Mapenzi hayaangalii hizo issues ni kwamba uyo anakutafutia sababu tu akuache ila hakupendi.

Mimi nafundisha chuo pia, wanafunzi kibao have crush on me. Wako wengine wananiibukia live. So siwezi sema kuwa na shida hio inaweza kuwa sababu mtu asipendwe.

Jaribu kujitathmini kwny maisha yako kuna mahala unakosea au haujiamini au hauchkui nafasi yako kama mwanaume. Kuhusu tatizo lako weka pembeni kwanZa focus on building yourself
Safi sana ni mfano mzuri ,Huo ndo uanaume kujikubali.
 
Umesema wewe ni kiziwi, hapo hapo unasema "UMESIKIA" tetesi.. Is it possible?
 
Muache, usimlazimishe

Utampata atayekupenda na udhaifu wako
 
Huyo alikupendea pesa. Bora kakuonyesha tabia halisi mapema. Pole
 
Dah! Pole sana mkuu, mim pia ni kiziw kama wewe nilipatwa na tatizo mwaka 2013 nikiwa kidato cha pili, hata mimi napitia chamgamoto kama yako imekuwa ngumu sana kwangu kuanzisha mahusiano kwan kila ninaejaribu kumweleza hisia zangu mwisho huishia kunikataa, nawaza sana cjui nitaishi maisha gani mim, nataman na mim niwe na familia sababu umri nao unasonga lakin ndo hivyo tena najikuta sina namna. Kiukwel inaumiza sana kwan sikupenda niwe hiv
Husikii kabisa au unasikia kwa mbalii?
Ninapoishi kuna kijana anatufanyia usafi ana usikivu wa mbali ukiongea nae unavuta kwanza pumzi ndefu ndio utoe sauti kali ili akusikie lakini mbona yupo fresh na anagonga mademu mtaan kama kawaida
 
Jf kila mtu ana uelewa wake😅😅 wengine hawaelewi aliyekwambia Mwamba hagongi ni Nan? Kaa utulie usome vzuri ndo utoe ushauri
 
Wadau naomba msaada wenu.

Mimi ni kijana mwenye tatizo la usikivu. Kuna mwanamke nilikuwa nataka kumuoa, sasa nimesikia tetesi kutoka kwa ndugu yake anasema hawezi kuolewa na kiziwi anaogopa kuchorwa japo yeye hujawahi kunitamkia.

Financial huwa namsaidia sana ila ndoa anasumbua, anasema hayupo tayari, ndugu yake kasema hataki kuolewa na wewe kisa kiziwi. Dah, nimejisikia vibaya.
Nasikitika kusikia hilo, lakini kumbuka kwamba kuwa kiziwi siyo sababu ya kutopata mwenza. Ni muhimu kuwa na mawasiliano wazi na mpenzi wako na kuelezea hali yako. Pia, unaweza kujaribu kumuomba msaada wa rafiki yake au ndugu yake kuwasiliana na mpenzi wako ili kufafanua mambo na kumsaidia kuelewa hali yako. Pia, ni muhimu kuelewa kwamba ndoa sio lazima, unaweza kujenga maisha mazuri na mwenza bila kufunga ndoa.
 
Dah! Pole sana mkuu, mim pia ni kiziw kama wewe nilipatwa na tatizo mwaka 2013 nikiwa kidato cha pili, hata mimi napitia chamgamoto kama yako imekuwa ngumu sana kwangu kuanzisha mahusiano kwan kila ninaejaribu kumweleza hisia zangu mwisho huishia kunikataa, nawaza sana cjui nitaishi maisha gani mim, nataman na mim niwe na familia sababu umri nao unasonga lakin ndo hivyo tena najikuta sina namna. Kiukwel inaumiza sana kwan sikupenda niwe hiv
Pole mkuuu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wadau naomba msaada wenu.

Mimi ni kijana mwenye tatizo la usikivu. Kuna mwanamke nilikuwa nataka kumuoa, sasa nimesikia tetesi kutoka kwa ndugu yake anasema hawezi kuolewa na kiziwi anaogopa kuchorwa japo yeye hujawahi kunitamkia.

Financial huwa namsaidia sana ila ndoa anasumbua, anasema hayupo tayari, ndugu yake kasema hataki kuolewa na wewe kisa kiziwi. Dah, nimejisikia vibaya.
Kuna rafiki yangu wakike anakufaa maana hata yeye anatatizo kama lako
 
Back
Top Bottom