Ushauri: Iundwe Kamati huru kubaini chanzo cha nyufa JNHP maana kuna harufu ya uhujumu uchumi

Ushauri: Iundwe Kamati huru kubaini chanzo cha nyufa JNHP maana kuna harufu ya uhujumu uchumi

nyufa tena? tumejiingiza kwenye kukata miti mingi bureee...na deni kubwa lisilolipika kirahisi hilo bwawa litaleta maafa makubwa sana kama lina nyufa kabla ya kujaa!???
 
Ujio wa Major General Tanesco ndugu Paul Kisesa Simuli usaidie kubaini ikiwa uhujumu ulifanyika na hatua stahiki zichukuliwe.
 
Watanzania wenzetu,wanatuhujumu,wanahujumu nchi, lakini watalindwa au wanalindana.Mwenyezi Mungu atuepushe mbali na hawa wahujumu
 
Tumeona Naibu waziri mkuu, Mh Dotto Biteko akifanya ziara katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na Kutoa ushauri jinsi ya kuziba nyufa zilizoanza kuonekana kwenye ukuta wa Bwawa.

Haiwezekani kuacha jambo hili lipite hivi hivi bila kufanyika uchunguzi na kuchukua hatua Kali dhidi ya wahusika wote.

Nashauri kamati huru ya Bunge iundwe kuchunguza sakata hili huku wahusika wote wakiwa nje ya ofisi za umma.

Ikiwezekana kamati hiyo huru ihusishe wataalamu Kutoka nje ya Serikali na nje ya nchi kupata UKWELI Ili kupendekeza solution sahihi.

Mkopo hata nusu ya robo haujalipika, na Mwekezaji aliongeza gharama zaidi ya Trilioni 1.5 zaidi ya Gharama halisi alizosaini mkataba na Bado tunaona mapungufu haya hata kabla ya uzalishaji kuanza.

Tusipokuwa serious katika masuala muhimu ya nchi, tukiruhusu kuoneana Aibu, kamwe hatutafanikiwa lolote .

NB: Tunapojadili Mada hii inayogusa maslah mapana ya nchi, tuepuke udini, ubinafsi, uchama nk nk, Uzalendo uwe Dira yetu.


Nawasilisha.🙏

Amen.
Msikuzee vitu, ni minor settlement, tena kwenye wings, kuweni na amani
 
Nyufa kwenye Kuta za Bwawa lililobeba ziwa la JNHP ni minor issue?
Sikiliza kijana, maximum pressure ya msukumo wa maji ya bwawa upo kwenye center ambapo mashine zimefungwa, kule pembezoni kwenye wings msukumo ni mdogo sana, kikubwa ni kuhakikisha panaimarishwa tu na kudhibitiwa pasiongezeke, lakini kule pembeni hata ukamwaga ukuta wa kifusi (saddle dam) bado ni salama, achilia mbali zege.
 
No research no right to speak.

Nawashauri tumieni muda kidogo kufanya tafiti nyepesi ya kimtandao "simple internet research" kabla ya kuja kudanganyana. Nimeitaama hiyo video sijaona "concern" yoyote ya masingi iiliyooneshwa na engoineer anaetowa maelezo wala waziri biteko. Au tunasikiliza vitu tofauti?

Kuna wanaonesha wamelishika neno "nyufa" na hawajali hizo nyufa ziko wapi. Nyufa zinazoongelewa hazipigiki picha kama ule uharo uliosambazwa.

Yaani Watanzania mmeshindwa kuelewa maana ya nyufa za kwenye mwamba zinazofanyiwa "grouting" ambazo engineer anazielezea hapo. Hizo kwa macho hazionekani, huwa kwa siku hizi zinaonekana kwa vifaa maalum au vipomo maalum, mradi hakuna nyufa kwenye "diaphragm walls" silioni tatizo.

Huo unaoongelewa kwenye hiyo video ni uboreshaji wa kawaida sana kwenye ujenzi, kama vifaa vilivyowekwa vimeonesha "abnormality".

Mara nyingi kutokana na vipimo vya awali vya mwamba unaweza kuweka grouting kwenye "design" au ikaamuliwa kuwa "grouting" itafanyika au isifanyike baada ya kuwepo na "load" kwenye bwawa. Kwa ujenzi na vifaa vya siku hizi Uwepo au usiwepo, mara nyingi au mara zote hufanyika ujenzi ukifikia stage fulani.

Hilo mbona ni jambo la kawaida kwenye miradi yoyote ya ujenzi mkubwa. Soma:


THE CONSTRUCTION CHALLENGES ASWAN HIGH DAM, EGYPT

View: https://m.youtube.com/watch?v=0VaCxQnrAFY
The designing of the Aswan High Dam faced many difficulties, for it has to be constructed on a pervious foundation in the lake of the existing Aswan Dam.

The whole extent of the main dam foundation will be covered with a layer of compacted dune sand about 82 feet deep.

The rockfill above this layer will have a clay core made of Nile silt. The dam will be protected against seepage by two lines of defence, a horizontal impervious blanket in the upstream part and a vertical grout curtain descending in the pervious bed of the river to a depth of 690 feet until it strikes natural bed rock.

This grout curtain will plug the voids in the layers of sedimentary materials underneath the dam.
 
Kuhamisha MD,kuleta mkurugenzi mpya bila uchunguzi, Bado hatutajua Hasa kiini Cha tatizo!!
 
Nimesikiliza clip ya maelezo yanayotolewa kwa naibu waziri mkuu na waziri wa nishati (Mh. Biteko).
Kinachozungumziwa pale ni kudhibiti maji kupenya kwenye miamba (permeability) na siyo nyufa kwenye ujenzi. Ujenzi umefanyika juu ya mwamba.
Kiasili udongo na miamba hupitisha vimiminika na hewa kwa viwango tofauti. Kwa miamba ya asili inayozunguka bwawa, lazima upitishaji huo udhibilitiwe kwa kushindilia grout kwa mashine maalum. Ni sehemu ya ujenzi na siyo makosa ya kiufundi.
Nyufa za kwenye zege ni tofauti na hili la kuzuia kwa grouting na madhara yake ni makubwa, ikiwemo kupasuka au kubomoka moja kwa moja kwa bwawa.
Hili tatizo linamhusu moja kwa moja mjenzi.
Nyufa za kwenye zege zitaongezeka ukubwa kuendana na muda au mzigo utakaoingia kama kilichosababisha hakitarekebishwa.
Kamati huru itatufungua macho,

Ujue Serikali imekopa pesa nyingi sana, lazima Tuhakikishe hapatokei dosari.
 
Mwenda zake kafanyaje?mbona Flyover ya Ubungo haina nyufa?
Hapa January ndiyo muhusika Mkuu na Bodi yake ya TANESCO iliyojaa Bankers badala ya Engineers!
RIP Mfugale.
 
Back
Top Bottom