Friday Malafyale
JF-Expert Member
- Jan 18, 2017
- 1,811
- 2,916
Mkuu hata Facebook ukifanya biashara na mtu akimark as sold bidhaa mlioziana chats zote zinakuwa cleared.Unachati na yeye anakuwa na uwezo wa kufuta chat zenu! Mtandao gani huo?
Simu ya aina gani?Wakuu kwema? Mimi kijana wenu mtiifu nimekuja kwenu nikiwa na majanga naomba mnisaidie.
Nilinunua simu mtandaoni kupitia kupatana.com, niliona bei ni nzuri nikamcheki jamaa nikachat nae kwenye hiyo website na akanipa namba.
Nikampigia kwa simu ya kawaida maana namba haikuwa WhatsApp, tukaongea akasema yupo mbezi nije tukutane niione.
Nikakutana nae pale mbezi stendi nikaicheki cheki nikaona ipo fresh niikampa hela nikaondoka na simu.
Baada ya kuitumia kama siku mbili nikagundua ina tatizo la charge ambalo sikuligundua muda ule. Nilipojaribu kumpigia nikashangaa namba zote nilizokuwa nawasiliana naye hazipatikani.
Niliumia lakini nikakubali tu kuishi nayo hivyo hivyo, nikakubali kupigwa. Sasa kimbembe kimekuja leo asubuhi wakati naitumia hii simu nikashangaa tu mara ghafla inawasha camera na kuanza kupiga 112, halafu inapiga milio kama ya ambulance, nikawahi nikaizima.
Nimekaa nimefikiria nimeshagundua itakuwa simu ilikuwa ya wizi na mwenye nayo anaitafuta, au huenda ilikuwa ni njama ya mapolisi kunifanyia hako kamchezo.
Sasa hapa nilichofanya nimeizima, ila bado nawaza nini nifanye sasa? Maana aliyeniuzia hapatikani na hata zile message za kupatana ameshazifuta hata mimi saivi sizioni.
Nilishaona watu wanakamatwa na polisi kwa hizi njama na kulipishwa pesa mingi au kubambikiziwa kesi.
Sasa nifanyeje wakuu?
Ipo hiyo hata telegramUnachati na yeye anakuwa na uwezo wa kufuta chat zenu! Mtandao gani huo?
Kanunua kitu cha wizi na siyo usedBro upo Dar na unanunua vitu USED?
Kuna sababu kwanini vinaitwa vitu USED.
Wasikutishe mkuu
Izo simu zinazoibiwa zinatumika sana na akuna kinachotokea sema haziwekwi line
Mzee simu nilinunua dar ila nshasepa mikoani saivi
Siku hizi imeungana na zoom inaitwa kupatana-zoom na pia kuna jiji buy onlineKu
Patana ipi mnayotumia mbona kwangu haifungukagi siku hizi
Jiji tamu ninayo app yakeSiku hizi imeungana na zoom inaitwa kupatana-zoom na pia kuna jiji buy online
Kutafuta kitonga au ganda la ndizi ndiyo tatizo mkuu..Hivi unaanzaje kununua kitu kama simu mkononi kwa mtu wakati maduka yamejaa Kariakoo mpaka vichochoroni?
Assume hiyo simu mtu alidungwa kisu akaporwa,au alibakwa akaporwa kisha simu ukamatwe nayo wewe!!!
Yaani mpaka Mahakama ije ikuone hauna Hatia ya Kuua au Kubaka utakuwa umeshakaa Segerea umejaa ukurutu mpaka makalioni!!acha kabisa kununua vitu vya electronics mkononi,utakuja kubeba msalaba usio wako!!!
Nunua kitochi cha elfu 25 kipyaaa wakati unajuchanga kuvuta Tecno ya laki moja na nusu... Nani kasema lazima umiliki Samsung??Ni kweli vitu used vina changamoto zake lakini kama pesa huna utafanyaje?
Kumbuka wengi tunaishi maisha Used used!
Magari karibu yote unayoyaona hapa nchini ni Used, unafikiri watu hawapendi Mapya? umasikini ni moja ya sababu ya watu kununua vitu Used.