Ushauri: Jirani yangu anataka kuuza nyumba ili akatafute maisha Uingereza ni sawa?

Kama ni engineer au Dr au ana utaalamu mkubwa wa shahada huenda akaja, matapeli wapo wengi sana na kama upo karibu nae mwambie aende ubalozi wa UK akahakikishe alichoambiwa kwani wao watamwambia bila kupepesa maneno

Bora asafiri na kwenda Dar kwa gharama nafuu kuliko kukosa vyote kwa utapeli

Kuna matapeli yanakuoiga sound mpaka unatoa kila kitu ni kama wamerogwa

Kuhusu kurudisha hela kwa miezi kadhaa hiyo ni ndoto labda analeta Unga na hiyo haina guaranteed ya kuingia nao

Namuombea kila la kheri ila kuna msoto huku sio yelemama
 
Mwambie anapigwa live bila chenga.. Mwambie ili umuokoe ulaya hakuna kazi za mserereko kiasi hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann una uhakika wa kilio? Toa sababu elezea fafanua tafadhali.
Kazi pekee anayoweza kupata ni ya kuosha vibabu na vibibi vizee kwenye nursing homes. Mshahara ni kama USD 3,000 kwa mwezi. Sijui akikatwa kodi na kulipia pango atabaki na Tsh ngapi za kutoboa
 
Hiyo million 20 ni hela ya visa,passport,flight ticket au ya nini?umesema anaenda kufanya kazi,hela hiyo ya nini??
 
Ana mwenyeji UK?
 
Nyumba za urithi zina shida sana angekuwa kajenga mwenyewe asingewaza huwo ujinga!
Kimfaacho mtu chake, kuna shida gani mtu kuuza Mali yake ili akamilishe plan nyingine?

Kila siku watu wanauza nyumba na wengine wananunuwa nyumba.

Kuna makampuni na viwanda vinauzwa wengine wananunuwa.

Bongo mtu akikwama hakuna wakumkopesha sasa akiuza asset yake kwenda kuangalia maisha mengine shida iko wapi?

Muhimu tu asikutane na Agency za wapigaji, hicho kipengere ndio pekee kinachohitaji umakini na upime Agency fee utapata ukweli.

Ziko njia za kuverify kama hiyo Agency ni genuine au mbambambaa.
 
Mshauri akope asiuze nyumba ....ulaya atapata hela ila kwa jasho hakuna free money kule pia umri wake ataweza kupifa kazi 2 ? Hataweza only 1 sasa kutoboa itamchukua Muda kdg sababu bills nyingi.......
 
Keyboard ina tabia mbaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…