Ushauri: Jirani yangu anataka kuuza nyumba ili akatafute maisha Uingereza ni sawa?

Wajuvi,wajuzi,wakulungwa na makontawa na matycoon mnaitwa huku mtoe ushauri.

Nina jirani yangu huku Morogoro ni mmama wa makamo, alienda dar kibiashara lakini katika pitapita zake amekutana na kampuni posta wanasaidia kuprocess watu kwenda nje.
Sasa amepewa plan ya kuunganishwa kwenda UK akafanye kazi.

Kimbembe amerudi anataka auze Kila kitu kuanzia nyumba mpaka kiwanja chake kipo msamvu ili aende.

Anasema ana Imani ndani ya miezi 6 anaweza kuzirudisha hizo asset.

Wakuu, hii imekaaje?
Hawezi kwenda kufeli akarudi na stress na majuto?
Kuna jamaa amerudi juzi baada ya miaka tisa anasema huko hapafai kama huna fani.
anyway kila mtu na zali lake
 
Kama ameshapata visa tayari auze tu haina shida, lakini kama visa bado simshauri auze.
 
Wajuvi,wajuzi,wakulungwa na makontawa na matycoon mnaitwa huku mtoe ushauri.

Nina jirani yangu huku Morogoro ni mmama wa makamo, alienda dar kibiashara lakini katika pitapita zake amekutana na kampuni posta wanasaidia kuprocess watu kwenda nje.
Sasa amepewa plan ya kuunganishwa kwenda UK akafanye kazi.

Kimbembe amerudi anataka auze Kila kitu kuanzia nyumba mpaka kiwanja chake kipo msamvu ili aende.

Anasema ana Imani ndani ya miezi 6 anaweza kuzirudisha hizo asset.

Wakuu, hii imekaaje?
Hawezi kwenda kufeli akarudi na stress na majuto?
Kwani Mumewe na Watoto wake wao wanasemaje!!??
 
Mwambie bora awe mganga wa kienyeji bongo, mtaji ni usinga na kaniki
 
Mwambie AACHE KABISA !!! AACHE KABISA !!

Atafute internet ni Waingereza wangapi hawana ajira. Anadhani yeye akienda atapataje??

Issue nzima ni UTAPELI MTUPU !!
 
Back
Top Bottom