Ushauri: Jirani yangu anataka kuuza nyumba ili akatafute maisha Uingereza ni sawa?

Kuna jamaa amerudi juzi baada ya miaka tisa anasema huko hapafai kama huna fani.
anyway kila mtu na zali lake
 
Kama ameshapata visa tayari auze tu haina shida, lakini kama visa bado simshauri auze.
 
Kwani Mumewe na Watoto wake wao wanasemaje!!??
 
Mwambie bora awe mganga wa kienyeji bongo, mtaji ni usinga na kaniki
 
inahitajika kama 20M, hana
Ndio wamemdanganya hivyo.... Kuwa auze nyumba na kila kitu.... Mama wa makamo... Huko ulaya anakwenda kuishije na alishakuwa makamo?? Nguvu za kuhangaika zishapungua....
 
Mwambie AACHE KABISA !!! AACHE KABISA !!

Atafute internet ni Waingereza wangapi hawana ajira. Anadhani yeye akienda atapataje??

Issue nzima ni UTAPELI MTUPU !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…