Ushauri: Jirani yangu anataka kuuza nyumba ili akatafute maisha Uingereza ni sawa?

Nani kakwambia kua nje hakuna maisha? watu tunakomaa na box huku na mambo yanaenda shwari kabisa,tatizo jinsi ulivyoelezea hapa inaonekana wazi kabisa kua kuna mtu anaenda kupigwa.
Ahaa kumbe ishu ni hyo agency na wala sio huo uamuzi wa kwenda nje kutafuta maisha?
Sidhan kama ni matapeli maana alivyodai wanafanya kazi mpaka na wizara
 
Ndio wamemdanganya hivyo.... Kuwa auze nyumba na kila kitu.... Mama wa makamo... Huko ulaya anakwenda kuishije na alishakuwa makamo?? Nguvu za kuhangaika zishapungua....
Habari za kuuza nyumba hajawaambia.
 
Mzuie asije akajinyonga watoto wa mjini wanataka kufanya yao hapo
 
kachanganyikiwa
 
Mimi nahitaji hicho kiwanja please! Mnake wajinga ndio waliwao
 
Ukipata fursa ya kuishi nchi za ulaya na marekani usijiulize mara mbili piga bei mpka Figo, Tanzania hauwezi kufanikiwa kama sio chawa.
 
hao uliokutana nao ni matapeli wanataka hizo hela,watakupiga maneno mengi wao wataondoka na hela na wewe utarudi moro na majuto.usiuze wala usiende kazana hapahapa kama riziki ipo ipo tu.
 
Hiyo visa hata hajapata ,halafu huko Uingereza hakuna.jipya.Maisha popote bwana.Kama alifanikiwa hadi kujenga nyumba Tanzania,basi anaweza kufika mbali zaidi.Aendelee kupiga kazi hapo hapo Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…