chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Haina shaka kwamba pombe na sigara, soda na vinywaji aina yake, na pengine sekta ya madini, ndio visababishi vikubwa vya maradhi. Visababisha maradhi basi viwe na mchango katika tiba.
Serikali ikae ifanye tathmini ili kujua endapo itaongezwa shilingi 100 kwa kila kinywaji, itapatikana shilingi ngapi.
Halafu iangaliwe huduma ya mama na mtoto huwa inagharimu shilingi ngapi, zipelekwe huko. Mama mjamzito, mama aliyejifungua na mtoto, wapewe huduma bure. Pia mtoto yeyote anayelazwa apewe huduma bure pamoja na wazee.
Wataalamu wakae wafanye tathmini ya makadirio ya gharama hizo. Hii inaweza kugusa huduma maalum za matibabu ya moyo kwa watoto. Hii itampa nafuu Malisa kuchangisha watu huko mitandaoni, na pia ugonjwa hauna chama.
Wanaume tukisaidiwa gharama za kuwatibu mke na mtoto, sisi tutajitibu wenyewe