Ushauri kuhusu kujenga nyumba ndogo pembeni kabla ya kumalizia nyumba kubwa

Ushauri kuhusu kujenga nyumba ndogo pembeni kabla ya kumalizia nyumba kubwa

Dodoma moja

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
307
Reaction score
182
Wakuu habarini za mihangaiko, nimejenga nyumba kubwa ya vyumba 3 nimeishia kuweka lenta lakini kutokana na kupanda Kwa gharama za vifaa vya ujenzi kuna uwezekano wa kuchukua hata miaka miwili Hadi kumaliza.

Kuna wadau wamenishauri ili nitoke kwenye upangaji basi nijenge chumba kimoja na sebule pembeni then nihamie halafu niwe naendelea na ujenzi wa nyumba kubwa nikiwa kwangu ili niondokane na kodi lakini pia itarahisha usimamizi wa nyumba kubwa.
 
Wakuu habarini za mihangaiko, nimejenga nyumba kubwa ya vyumba 3 nimeishia kuweka lenta lakini kutokana na kupanda Kwa gharama za vifaa vya ujenzi kuna uwezekano wa kuchukua hata miaka miwili Hadi kumaliza
Kuna wadau wamenishauri ili nitoke kwenye upangaji basi nijenge chumba kimoja na sebule pembeni then nihamie halafu niwe naendelea na ujenzi wa nyumba kubwa nikiwa kwangu ili niondokane na Kodi lakini pia itarahisha usimamizi wa nyumba kubwa
Hongera sana, fanya hivyo
 
Hiyo nyumba ya vyumba vitatu ni kubwa kiasi gani?

Kama ni ya kawaida, ni bora upaue hiyohiyo kubwa na uingie kibishi, mfano, unaweka madirisha hata chumba kimoja.

Ukisema uanze kujenga nyumba ya uani, ni gharama kubwa na unakuwa umelisogeza tatizo mbele. Nilichojifunza, hata chumba kimoja tu kinaweza kutumia milioni kadhaa!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kuha nyingine huoni kama ni gharama ya ziada,hapo jipige upaue tu,then weka madirisha na milango ya nje then amia tu.

Mdogo mdogo unamaliza mjengo
Ushauri bora kabisa
 
Mimi nakushauri hiyo hela umalizie nyumba kubwa upande mmoja then uamie wakati unamalizia mdogo mdogo
Hii ndiyo akili, tafuta vyumba viwili vilivyo karibiana then uvipaue nusu weka dirisha na mlango then hamia... Ukiwa humo anza kubandika mabati, mbao, simenti nk... Utashangaa baada ya miezi sita unapaua another two or three rooms...
 
Sasa nyumba kubwa utapauaje vyumba viwili wakati inatakiwa ipauliwe kisasa nyumba nzima au ndo unapaua kama slope then ukitaka kuipaua yote unang'oa mabati ya hivyo vyumba viwili?
 
Sasa nyumba kubwa utapauaje vyumba viwili wakati inatakiwa ipauliwe kisasa nyumba nzima au ndo unapaua kama slope then ukitaka kuipaua yote unang'oa mabati ya hivyo vyumba viwili?
Itakuwa hivyo, japo wataanza kusema nyumba za wasomi siku hizi zinafikirisha.

Bora apige bati nyumba nzima na aweke madirisha na mlango chumba kimoja.

Funzo kwa wengine, mtu akitaka kujenga nyumba, amtafute fundi amshauri gharama za ujenzi kulingana na ramani. Habari ya kujenga ramani kali kama ya fulani bila kuangalia uchumi, matokeo yake ndio haya

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sina cha kukushauri wengi hatujui uchumi wako. Mradi umesema utachukua hata miaka 2 nikushauri tu uwe mvumilivu miaka 2 sio mingi labda kama umepanga nyumba ya kuanzia 200k na kuendelea.

Inakuwa vigumu kukushauri kwa sababu hatujui ukubwa wa familia yako. Kama upo na wife tu nikushauri pandisha hiyo master ya nyumba yako uishi wakati unajenga polepole.

MUNGU AKUSAIDIE, UJENZI KWA MASIKINI NI MSUMALI WA MOTO
 
Tunashukuru kwa ushauri Ila hapo mwishoni unakosea ndugu. Mipango muda mwingine hufeli....mwenyewe Niko kama huyu mkuu kikubwa tutiane moyo tutoboe. Wanaume tunayoyapitia tunajua wenyewe.
 
Sina cha kukushauri wengi hatujui uchumi wako. Mradi umesema utachukua hata miaka 2 nikushauri tu uwe mvumilivu miaka 2 sio mingi labda kama umepanga nyumba ya kuanzia 200k na kuendelea.

Inakuwa vigumu kukushauri kwa sababu hatujui ukubwa wa familia yako. Kama upo na wife tu nikushauri pandisha hiyo master ya nyumba yako uishi wakati unajenga polepole.

MUNGU AKUSAIDIE, UJENZI KWA MASIKINI NI MSUMALI WA MOTO
Dah Mungu atusaidie
 
Back
Top Bottom