Ushauri kuhusu kujenga nyumba ndogo pembeni kabla ya kumalizia nyumba kubwa

Ushauri kuhusu kujenga nyumba ndogo pembeni kabla ya kumalizia nyumba kubwa

Wakuu habarini za mihangaiko, nimejenga nyumba kubwa ya vyumba 3 nimeishia kuweka lenta lakini kutokana na kupanda Kwa gharama za vifaa vya ujenzi kuna uwezekano wa kuchukua hata miaka miwili Hadi kumaliza
Kuna wadau wamenishauri ili nitoke kwenye upangaji basi nijenge chumba kimoja na sebule pembeni then nihamie halafu niwe naendelea na ujenzi wa nyumba kubwa nikiwa kwangu ili niondokane na Kodi lakini pia itarahisha usimamizi wa nyumba kubwa
Mshika mbili yote humponyoka. Ng'ang'ana na hiyo kubwa. Gharama ya kujenga nyumba ndogo inaweza tosha kukamisha vyumba viwili ktk nyumba yako kubwa.
 
Ushauri wenu wote nimeuchukua naenda kuchambua then niendelee na hatua zingine
 
Ujenzi wa hiyo chumba na sebule hadi kumaliza ni gharama za kupaua hiyo nyumba kubwa. Nakushauri, paua nyumba kubwa yote then chagua vyumba viwili vinavyofwatana, weka Magrili na milango. Madirisha piga makaratasi na wavu kwa juu, Hamia, then endelea na hatua za finishing ya nyumba nzima mdogo mdogo. Rafiki yangu amefanya hivi na nyumba jirani zangu kadhaa wamefanya hivi. Kumbuka gharama ya room moja hadi kuikamilisha ni not less than 3.5M
 
Itakuwa hivyo, japo wataanza kusema nyumba za wasomi siku hizi zinafikirisha.

Bora apige bati nyumba nzima na aweke madirisha na mlango chumba kimoja.

Funzo kwa wengine, mtu akitaka kujenga nyumba, amtafute fundi amshauri gharama za ujenzi kulingana na ramani. Habari ya kujenga ramani kali kama ya fulani bila kuangalia uchumi, matokeo yake ndio haya

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kuongezea hapo ni kwamba mbali na kujua gharama ya ujenzi pia unajipima kwa kipato chako utajenga kwa muda gani. Maana mtu analipwa laki 8 kwa mwezi anataka kujenga nyumba ya milioni 60 kwa miaka miwili, haiwezekani. Tazama kipato chako jenga nyumba inayolingana na uwezo wako

Kwa mtoa mada, siku nyingine ukitaka kujenga andaa kitu kinaitwa land use plan yaani mpango wa matumizi ardhi. Sio unakuja kukurupuka tu kujenga chumba na sebule wakati haikuwa kwenye plan ya matumizi ardhi.

Ungekuwa umepanga kuweka hako kajumba ka pembeni ungeanza nako halafu baadae unakuja kuanza kubwa ukiondokana na kero ya upangaji. Ila kwa sasa nashauri kama walivyoshauri wengine komaa na bati kisha weka sawa vyumba viwili na choo zama ndani umalizie boma lako

Hiyo chumba na sebule ya pembeni kama ukijenga standard inakula 10m na zaidi sasa si bora ukomae na nyumba kubwa tu
 
Wakuu habarini za mihangaiko, nimejenga nyumba kubwa ya vyumba 3 nimeishia kuweka lenta lakini kutokana na kupanda Kwa gharama za vifaa vya ujenzi kuna uwezekano wa kuchukua hata miaka miwili Hadi kumaliza
Kuna wadau wamenishauri ili nitoke kwenye upangaji basi nijenge chumba kimoja na sebule pembeni then nihamie halafu niwe naendelea na ujenzi wa nyumba kubwa nikiwa kwangu ili niondokane na Kodi lakini pia itarahisha usimamizi wa nyumba kubwa
Kama umefikia kwenye "lintel" hauna haja ya kujenga nyumba nyingine pembeni, nimeona huyu Mzee Abdul Ghafur anajitangaza humu JF, sijaona kwa macho yangu, bali nimeona kwenye whatsapp mpaka wamem feature wajenzi wa nje ya Tanzania kwa kubadilisha namna ya ujenzi Tanzania. Anaezeka chumba kimoja kimoja kwa kutumia precast slabs. Ongea nae, anaweza kukupa ufumbuzi wa kuezeka chumba kimoja kimoja katika hiyo hiyo nyumba yako kubwa, ukahamia hapo. Jana nilikua na chat kwa whatsapp kuhusu hilohilo la kuezeka kidogokidogo. Whatsapp yake +255625249605. Anajitangaza humu JF.
 
Back
Top Bottom