Ushauri kuhusu kujenga nyumba ndogo pembeni kabla ya kumalizia nyumba kubwa

Mshika mbili yote humponyoka. Ng'ang'ana na hiyo kubwa. Gharama ya kujenga nyumba ndogo inaweza tosha kukamisha vyumba viwili ktk nyumba yako kubwa.
 
Ushauri wenu wote nimeuchukua naenda kuchambua then niendelee na hatua zingine
 
Ujenzi wa hiyo chumba na sebule hadi kumaliza ni gharama za kupaua hiyo nyumba kubwa. Nakushauri, paua nyumba kubwa yote then chagua vyumba viwili vinavyofwatana, weka Magrili na milango. Madirisha piga makaratasi na wavu kwa juu, Hamia, then endelea na hatua za finishing ya nyumba nzima mdogo mdogo. Rafiki yangu amefanya hivi na nyumba jirani zangu kadhaa wamefanya hivi. Kumbuka gharama ya room moja hadi kuikamilisha ni not less than 3.5M
 
Kuongezea hapo ni kwamba mbali na kujua gharama ya ujenzi pia unajipima kwa kipato chako utajenga kwa muda gani. Maana mtu analipwa laki 8 kwa mwezi anataka kujenga nyumba ya milioni 60 kwa miaka miwili, haiwezekani. Tazama kipato chako jenga nyumba inayolingana na uwezo wako

Kwa mtoa mada, siku nyingine ukitaka kujenga andaa kitu kinaitwa land use plan yaani mpango wa matumizi ardhi. Sio unakuja kukurupuka tu kujenga chumba na sebule wakati haikuwa kwenye plan ya matumizi ardhi.

Ungekuwa umepanga kuweka hako kajumba ka pembeni ungeanza nako halafu baadae unakuja kuanza kubwa ukiondokana na kero ya upangaji. Ila kwa sasa nashauri kama walivyoshauri wengine komaa na bati kisha weka sawa vyumba viwili na choo zama ndani umalizie boma lako

Hiyo chumba na sebule ya pembeni kama ukijenga standard inakula 10m na zaidi sasa si bora ukomae na nyumba kubwa tu
 
Kama umefikia kwenye "lintel" hauna haja ya kujenga nyumba nyingine pembeni, nimeona huyu Mzee Abdul Ghafur anajitangaza humu JF, sijaona kwa macho yangu, bali nimeona kwenye whatsapp mpaka wamem feature wajenzi wa nje ya Tanzania kwa kubadilisha namna ya ujenzi Tanzania. Anaezeka chumba kimoja kimoja kwa kutumia precast slabs. Ongea nae, anaweza kukupa ufumbuzi wa kuezeka chumba kimoja kimoja katika hiyo hiyo nyumba yako kubwa, ukahamia hapo. Jana nilikua na chat kwa whatsapp kuhusu hilohilo la kuezeka kidogokidogo. Whatsapp yake +255625249605. Anajitangaza humu JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…