Dodoma moja
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 320
- 209
Wakuu habari, ninaishi kwenye upangaji kwa sasa hivyo naendelea kupambana na adha za baba mwenye nyumba lakini kwa bahati nzuri nimeweza kununua kiwanja na sasa najipanga na ujenzi lakini wakati huo mawazo ni mengi kichwani mwangu nikiwaza kujenga nyumba ya ndoto yangu ambayo itanichukua muda mrefu zaidi kuikamilisha lakini hapo hapo yapo mawazo ya kuanza kujenga nyumba ndogo ya kuanzia maisha yaani chumba self, sebule na jiko ambayo nitaijenga kwa muda mfupi zaidi then nitahamia chap hata kama itakuwa haijakamilika 100% ilimradi iwe na mazingira ya kuniwezesha kuishi lengo ni kutoka kwenye upangaji na wakati nitaanza kujenga nyumba ya ndoto yangu bila stress za kodi na changamoto za upangaji. Nimepata idea zote hizo kwa sababu nikisema nianze nyumba ndogo itanichukua mwaka 1 kuijenga na kuhamia na nyumba ya ndoto yangu itanichukua zaidi ya miaka 3 kuhamia na upande wa kodi ninayolipa kwa sasa ni Tsh. 2,200,000/= kwa mwaka hapa bado umeme, maji na usumbufu mwingine
Nimepanga kuwa nitakapohamia kwenye nyumba kubwa hii ndogo nitaifanya kuwa appartment
Naombeni ushauri wenu wakuu ili nisije kujilaumu baadae wazo lipi la kuanza nalo?
Nimepanga kuwa nitakapohamia kwenye nyumba kubwa hii ndogo nitaifanya kuwa appartment
Naombeni ushauri wenu wakuu ili nisije kujilaumu baadae wazo lipi la kuanza nalo?