Ushauri kujenga nyumba ndogo kabla ya nyumba kubwa

Nakushaur jenga nyumba moja kwa moja.

Achana na hii ya kusema sijui unaanza servant alaf uje kujenga kubwa.

Inawezekana ukaanza ndogo na usiimalize pia.

Usiwe na haraka. Umesema hapo kuwa Kubwa unaweza kujenga kwa miaka 3.
Sasa nikuambie tu. Jipe miaka 6 ya kujenga nyumba yako kubwa.
Hakuna haraka na haukimbizan na mtu.

Ikifika hatua nzur unahamia umalizie ukiwa ndan.
 
Fuata guts zako. Jenga nyumba ndogo. Hamia. Hamna raha kana kujenga nyumba bila pressure,hio kubwa utaijenga kwa raha maana site ni hapo hapo nyumbani. Yaani unamaliza,unahamia halafu unaanza kula hela ya kodi. Done did.
 
Anza tu na hiyo ndogo..ujenzi wa nyumba ya ndoto zako ifanyike ukiwa umejipanga kikamilifu.
 
Hivi nyinyi mnaosumbuliwa na wenye nyumba huwa mnawatoa wapi?

Nyumba nilizowahi panga. Ya kwanza nilikaa miaka mitatu mwenye nyumba sijawahi muona.

Ya pili nilipanga na mwenye nyumba akiwa jirani tulisumbuana pale naondoka anataka nilipie mwezi unaofuata wakati kwenye mkataba hiyo clause haikuwepo.

Nyumba ya tatu nilikaa na mwenye nyumba pembeni kwenye nyumba mojawapo ya kupanga. Alinidanganya ni mpangaji nilikaa miezi 6 ndio nikajua mwenye nyumba ni yeye. Nilikuwa naanika nguo nje mvua ikinyesha ananitolea anaweka kwake nikirudi ananipa.

Ya nne tangu nipange mwenye nyumba kaja mara moja kukagua nyumba ya pembeni.

Sijioni nikijenga nyumba ya kuishi hivi karibuni. Mwenye nyumba #3 alijenga apartments akawa anaishi mojawapo. Maana yake akijenga nyumba ya ndoto zake atapangisha hii anayoishi.
 
Kodi ya 2.2m unailipaje mbona haigawanyiki kwa 3 au 6 au 12? Kwa mwezi ni 183,333.333333333333333 hivyo vitatu vitatu unamlipaje?
Hayo ni mapatano yetu na mwenye nyumba mwanzo nilikuwa nalipa 2M kwa mwaka baadae akaongeza laki 2 imekuwa 2.2M ambapo nalipa 1.1M kwa miezi 6
 
Hayo ni mapatano yetu na mwenye nyumba mwanzo nilikuwa nalipa 2M kwa mwaka baadae akaongeza laki 2 imekuwa 2.2M ambapo nalipa 1.1M kwa miezi 6
Daah hii system ya kulipa kodi miezi 6 inaumiza sana. Why tusilipe kwa mwezi tu?
Anyway back to the point.

Jenga nyumba kubwa kabsa. Ukifikia sehemu malizia chumba sebule hamia huku ujenzi unaendelea kuunga unga.
 
itakuwa ndio mipango yake hiyo anaishi na wapangaji kwenye appartment then anajenga nyumba ya ndoto yake taratibu akiwa na wapangaji bila stress mwisho wa siku akihama huku anapangisha na wapo wengi ambao wamewahi kufanya hivyo
 
Tena nyumba inakuwa ya kupangisha tangu mwanzo kwahiyo akiondoka anapata mpangaji haraka.
Na wala hapati hasara ya kupangisha nyumba kubwa ya kuanzia maisha kwa bei ndogo, maana mpangaji anajua huna options nyingi.
 
Kiwanja chako kina square meter ngapi?
 
Fanya hivyo faster...

Cc: Mahondaw
 
Daah hii system ya kulipa kodi miezi 6 inaumiza sana. Why tusilipe kwa mwezi tu?
Anyway back to the point.

Jenga nyumba kubwa kabsa. Ukifikia sehemu malizia chumba sebule hamia huku ujenzi unaendelea kuunga unga.
Inaumiza sana aisee hususani kwa wenye vipato vya kuungaunga
 
Tena nyumba inakuwa ya kupangisha tangu mwanzo kwahiyo akiondoka anapata mpangaji haraka.
Na wala hapati hasara ya kupangisha nyumba kubwa ya kuanzia maisha kwa bei ndogo, maana mpangaji anajua huna options nyingi.
Exactly
 
Umewaza vizuri sana mkuuu nyumba kubwa kwa kipato cha kuunga unga ni kisanga, mi nilikurupuka na jumba kubwa sa ivi nataka niezeke niitelekeze nijenge pembeni chumba sebule self nipumue
Kwa maelezo yako ni kwamba umefulia. Niuzie hilo pagale nifugie kitimoto au kuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…