Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Tena wacha Vichwa vya Diaspora virudi ili Wafanye kazi na Raisi Samia Suluhu wanachoogopa hao makapuku ni kuwa nafasi zao zitatwaliwa na Watanzania wenye Elimu ya kweli na Exposure kutoka Diaspora.

View attachment 1810215
Wanaogopa tu mkuu. Watu wa Diaspora wanaotetea uraia pacha sababu hasa sio kuja kufanya kazi hizi za mishahara ya milioni mbili hadi nne na kuwanyang'anya nafasi zao au za watoto wao. Diaspora wanachotaka ni uhakika wa usalama wa mali zao kama raia wa Tanzania ikiwa watahamisha capital kuja Tanzania. Tena sasa iko wazi, kwamba nyakati fulani nchi inaweza kupata kiongozi kichaa akasumbua sana wawekezaji wasio raia.

Dangote amesumbuliwa sana katika kipindi kilichopita. Alipata vikwazo vingi kwa kuwa pia sio raia wa Tanzania. Sisemi kwamba Dangote ni mmoja wapo wa kupewa uraia pacha tukiuruhusu - maana sharti moja wapo la uraia pacha ni kuishi nchini kwa zaidi ya miaka mitano, lakini Dangote ni mfano mzuri wa tofauti ya treatment kwa mwekezaji aliye raia na asiye raia. Mwekezaji asiye raia unaweza kumpa masaa 24 kuondoka nchini kwa sababu za majungu tu. Akiwa raia huwezi kufanya hivyo.
 
Na sisi tunaotaka sio wenye nchi? Kuna watu mnajiona mna haki miliki ya Tanzania kuliko sisi wengine. Labda tatizo ndio linaanzia hapo.
nyie ndio wale mliokuwa mnasema katiba ibadilishwe nanii aongezewe miaka , mnastahili alipo.
 
Elimu yako na upeo wako wa nadharia ya dunia hii unatia shaka. Anyway kutoa comments ni haki yako kikatiba.
 
Hili swala la uraia wa nchi mbili sidhani kama serikali imefanya utafiti wa kujua faida na hasara zake. Na huu ni uvivu tu kwani wangeweza kwenda kwenye balozi ambazo nchi zao zina ruhusu uraia pacha na kuuliza faida na hasara zake.

Mie na unga hoja ya uraia wa nchi mbili kwa wa Tanzania lakini tusiruhusu mataifa mengine kupata uraia wa Tanzania kwa njia ya makazi.

Taifa letu limeshindwa kutoa ajira za kutosha kwa raia, tukianza kuruhusu wageni wapate uraia kirahisi vijana wengi watakosa ajira.

Sheria ipite kwamba, mtanzania atakae chukua uraia wa nchi nyingine , bado ataendelea kuwa raia wa Tanzania bila kupoteza haki zozote. Thats it. Hapo mchina na mkenya watafaidika vipi?

Kuruhusu uraia pacha kwa mtanzania haimaanishi mchina, mmarekani, mkenya nae anaruhusiwa kuja Tanzania na kupewa uraia. Hio ni sheria nyingine kabisa.

Tusijitese kwa kuogopa mataifa mengine. Diaspora hao hao ndio wanawasaidia ndugu zao kila siku sasa kuna kosa gani wakiwa na uraia wa nchi mbili? Wanachuma kule wanakuja kula nyumbani kitu ambacho ni kizuri kwa uchumi wetu.
 
Wewe kuna mawili. Either ni masikini, na kama una maisha mazuri, either umekwiba, umepokea rushwa, au mzazi/mlezi wako ndio aliyetoboa. Na kama ametoboa, inawezekana na yeye alitoboa kwa wizi. In short, una mentality ya kimasikini.
Povu kubwa limekutoka !!?
hamtafanikiwa
 
Uraia pacha hapana. Hakuna mgao kwenye uzalendo. Sisi hatuhitaji kuja kua na wabunge na rais wenye uraia pacha. Mtu alikua mwanajeshi jeshi la marekani juzi mtu alikua jasusi wa marekani juzi leo aje anagombea ubunge au anakua balozi au rais wa tanzania. Acheni mawazo yasiyokua maana.
 
Wewe unajuaje hawa wabunge, mabalozi, na viongozi wengine tulionao sasa hivi, hakuna anayefanya ujasusi kwa manufaa ya nchi kama marekani? Tena ni hawa wanasiasa ambao hata Nyerere aliwaita malaya na kusema heshima yao ina bei. Wananunulika kirahisi sana.
 
Ndio maana nasema watu mnaojibu vitu hivi hamna ufahamu wa kutosha. Kwani nani amesema tukiwa na uraia pacha basi ni lazima tuwaruhusu walio na uraia pacha kuwa wabunge au raisi wetu? Kwani wabunge na maraisi wetu tunaokoteza tu, hatuna vigezo?

Na mtu aliye mwanajeshi au jajsusi Marekani leo, hajawahi kuishi Tanzania, itakuwaje aje awe raia pacha na Tanzania?

Watu msioelewa mambo ndio mnabisha zaidi.
 
Mkiambiwa mlete hoja nzito za kwa nininiraia pacha hamna hoja nzito.
Kama muda wa kikwete nae alikataa basi sahauni...
 
Mkuu, imesemwa hapo juu Membe akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alilifanyia utafiti sana, na kukutana na viongozi wa Afrika na nchi za Magharibi kuelewa undani wake, na uzoefu wao baada ya kuruhusu uraia pacha. Ndio maana akatoa tamko kwamba akiwa raisi hilo ni jambo ataruhusu mara moja. Na kumbuka Membe alikuwa Mkurugenzi wa TISS, kwa hiyo hili suala la usalama wa nchi yeye aliliona kwa mapana kuliko hawa mabulikoko humu ndani wanaodai kwamba uraia pacha utaathiri usalama wa nchi
 
Hebu toa definition ya uzalendo kwa uelewa wako.
 
Sidhani kama watakuja na point nzito zaidi ya kusema watawekeza.
Actually faida kubwa ni kuwekeza na kitu kinaitwa profit repatriation to your country of chieftainship. Ukiwa nje, kunakuwa na masharti ya kutoia fedha za kigeni, kama ilivyo hapa Tanzania. Lakini ikiwa unataka kupeleka fedha ya kigeni katika nchi ya uraia wako basi unakuwa na uhuru zaidi.

Pia unapowekeza katika nchi ambayo huna uraia nayo, kunakuwa na tax implications fulani katika nchi uliyo na uraia nayo, kwa kuwa nchi unayoishi inachukulia umetoa capital yao kwenda nchi ambayo siyo yako na hivyo kuifaidisha nchi ya wengine kuliko nchi yako. Sasa pia, ikiwa nchi uliyowekeza pia ni nchi uliyo na uraia nayo inakuwa na tax implication tofauti. Na mwisho ni kwamba, watu hawako comfortable kuwegeza katika nchi ambayo yeye anaonwa kama mgeni. Anaweza kuja raisi kichaa akabadilisha sheria za uwekezaji kwa watu wasio raia. Ethiopia kama wewe sio raia ni vigumu sana kumilikishwa chochote. Ni lazima uwe raia ndio unakuwa na uhuru wa kumiliki assets fulani fulani.

Ndio maana basi watu wanasema wazi, unaporuhusu uraia pacha, inafungulia sana capital inflow kutoka watu o wataruhusiwa kuwa na uraia pacha na Tanzania. Lakini watu wasielewe kwamba kupewa uraia pacha na Tanzania ni suala la sadaka. Kuna vigezo na mashart ya kufuata, na ni ombi ambalo Tanzania inaweza kukubali au kukataa kwa kila mtu anayeoomba, kutokana na vigezo vilivyowekwa.

Sasa unakuta mpumbavu mmoja anasema tukiruhusu uraia pacha siku moja tunaweza kujikuta tuna mbunge au raisi aliyekuwa jasusi wa Marekani, au wahindi wote watachukua uraia wa Tanzania na kuchukua ardhi yetu. Hivi watu hawa wana akili lakini? Halafu unakuta mtu anaetoa point kama hizo ni mbunge!
 
Hebu toa definition ya uzalendo kwa uelewa wako.
Sintashangaa akikuambia mzalendo maana yake Mtanzania wa kuzaliwa nchini kama Ole Sabaya! Yaani watu vihiyo ndio wako mstari wa mbele kusema uraia pacha una risk za uzalendo na usalama.
 
Tunawaonea wivu nyinyi diaspora ?

Sasa kwa nini tuhangaike kubadilisha sheria kuwasapoti watu ambao wanatukashfu tuliopo hapa nchini wakisema wao wako njema mpaka tunawaonea wivu ?

Hoja nyepesi za wana diaspora ndio hizi maskini ya Mungu.
Tunawaonea wivu kufagia vyoo ughaibuni
 
Sidhani kama watakuja na point nzito zaidi ya kusema

Sidhani kama watakuja na point nzito zaidi ya kusema watawekeza.
Mkuu dunia sikuhizi imekuwa kijiji. Jambo hili la uraia pacha sio ajenda ngeni tena pamoja na kwamba hapa nyumbani bado inaonekana kama ni cancer isiokuwa na tiba. Tambua;
  • si jukumu pekee la Diaspora kuja na point nzito za ushawishi bali ni issue ya mtanzania yoyote mwenye uelewa mpana kuliongelea.
  • Serikali haiitaji kushawishiwa kuhususiana na jambo hili bali wanatakiwa kujipanga katika kuweka mipambo na taratibu za kuratibu na kutekeleza.
  • Tukiachana na hoja ya uwekezaji wa Diaspora. Hivi unamtreat vipi mtanzania aliechukua uraia wa nchi nyingine ili kupata unafuu wa gharama za masomo na leo kafudhu katika sekta adimu kama udaktari, engineer ktk sector za gas na mafuta nk. Je, utamwajiri kama expert na umpe marupurupu kama tunavyowapa experts wengine ( particularly wazungu) au vipi?
 
Tunawaonea wivu kufagia vyoo ughaibuni
Akifagia vyoo anapoteza utanzania? Au kama ni mjomba wako, kaka, dada yako unamkana kwakua anasugua vyoo ulaya. Je, wanaosugua vyoo hapa nyumbani si watanzania kamali au nini hoja yako?
 
Mleta mada, hoja iwe moja:- Uraia pacha tu, faida na hasara zake. Usichanganye na mengine itakutoa kwenye mstari.
kweli kabisa. Thread imeandikwa kwa hasira kiasi kwamba haionyeshi ushawishi. Jikite kwenye faida na hasara zake then hata hao wanaopinga waweze kubadilika, na labda wanaounga mkono nao wabadilike pia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…