Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Udungaembe maana yake ni Nini??.
 
bila uraia pacha hayo hayawezi kufanyika? Mimi naona linaweza kuwa jambo zuri ila mnaotoa mada bado mko too brief.
 
Israeli ina uraia pacha na raia wake bado wanaipenda nchi yao
 
Awatumie ndugu zake kuwekeza, au awekeze kama mgeni alipe mamilioni ambayo zingeenda kusaidia jamii. Unajua visa na vibali ni pesa ndefu.

Unawajua ndugu wa kibongo?
Hao ndugu si ndio atakuja kufanya nao biashara? Kama wawekezaji wanalipa mamilioni na hilo unaona ndilo tatizo, mbona wanazidi kuja? Je mamilioni hayo si yanalipwa serikalini na serikali ndiyo inayaingiza kwenye shughuli za kijamii? Kama tuna wasiwasi na serikali, then issue siyo uraia pacha bali utawala bora
 
Mfano wako wa Dangote, ni irrelevant.

Tunazungimzia watanzania wazawa ambao wanataka kurudi na wasiwekewe masharti kama ya wawekezaji wageni pale wanapotaka kurudi na kuwekeza nyumbani.
Kwa hiyo uraia pacha utakuwa wa kiubaguzi? Yaani Mhindi akitaka na uraia wa Tanzania akataliwe, ila Mtanzania akitaka na uraia wa India akubaliwe!
Hoja ya Dangote ilizaliwa na hoja kuwa watanzania walio nje (walioukana uraia) wanashindwa kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa si watanzania tena.
 
Labda nikuulize swali,ndani ya Tanzania kuna uwezekano wa mtu mmoja kuwa na makabila mawili tofauti?
Tumezoea hata kama mtoto ana wazazi wa makabila mawili tofauti,mtoto anatajwa kwa jina au kabila la baba yake.
Kwa mantiki hiyo habari ya kuwa na uraia wa nchi mbili au zaidi tusiuchekee,unaweza ukawanufaisha wachache lakini walio wengi wataumia.

Ushauri wangu kwa serikali kuhusu kuongeza diaspora ni kurekebisha mfumo mzima wa utoaji wa passport,
Mfumo wa sasa hivi wa kuulizwa swali la "unaenda wapi?'' ubadilishwe.
Chini ya swali hili waliotakiwa kupata passport wamekosa na wasiotakiwa wamepata, na wengi wamepata nyaraka hizo muhimu kwa uongo
na wale ambao hawakuwa tayari kuongopa wamekosa bila sababu za msingi.

Hakuna siri kwamba ajira hapa kwetu ni shida kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi duniani,lakini nchi nyingi zimeruhusu raia
wake kupata nyaraka za kusafiria ili kuwa ruhusu watu kutafuta maisha nje ya nchi zao kwa njia halali.
Wizara ibadilishe vigezo,kwa kuangalia labda tuseme elimu ya mtu,umri na shughuli anayoenda kuifanya badala ya maswali yasiyo na tija.

Kuna taasisi unakuta zinatoa nafasi za wafanyakazi kwenda nje kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi, na unakuta course hiyo
inajitokeza ghafla kufauatana na uhitaji let say kutengeneza mitambo na anatakiwa mtu mwenye passport iliyotayari
wewe ambaye huna unakosa fursa hiyo.Ukienda uhamiaji kuomba passport ili nawe uwe nayo ready to go uanaulizwa ''unaenda wapi?''
usipodanganya hupati maana kwa wakati huo unakuwa huna pa kwenda ila ni maandalizi.

Naomba wizara iangalie mambo kama haya,huwezi kwenda nje na kuishi huko mara moja
bila kwanza kwenda kutembelea kupitia fursa mbalimbali zinazojitokeza kupitia makampuni yetu.
kama kweli tunahitaji kuwa na diaspora wengi,turekebishe mfumo wetu wa utoaji wa passport.
kila mwenye umri wa miaka 18 aruhusiwe kupata passport bila mizengwe .
 
Waeleweshe basi maana yake, vigezo nk. Usikimbilie kusema wana chuki, wivu nk. maana unaposema hawaelewi halafu unawahukumu kuwa wana wivu, chuki nk hujawatendea sawa.
 
Watu wanalazimika kuukana uraia wa Tanzania sio kwamba hawaipendi nchi yao, ni wazalendo kuliko hata hao wanaopinga bungeni na wanamanufaa kwa nchi kuliko hao wanaoikamua serikali kwa mishahara minono isiyotozwa kodi.

Diaspora wanatuma pesa kwa ndugu na kuongeza mzunguko wa pesa...hao wanaojiona ni wazalendo wao asilimia kubwa wanachukua pato kubwa kuliko wajibu wao.

Ni ngumu kuacha fursa ambayo huwezi ipata hapa bongo, na ambayo unaweza itumia kuajiri watu wengine nyumbani kupitia miradi ama support. Je, warudi kubanana kugombania kazi bongo? Nimejifunza kwa waghana, Nigerians, Somalis na waabeshi jinsi wanavyoinua uchumi wao, remittance ktk hizi nchi ni muhimu sana kwa pato la nchi.


Sasa sisi tubaki uraia pacha ati ni najisi kwa taifa....najisi hiyo kwiyo!!
 
Mbona walisumbuliwa wengi tu hata ambao ni raia wa Tanzania? Kiongozi akisha kuwa kichaa (kama ulivyoandika) ukichaa wake unakuwa kwa wote. Mbowe, Manji, NGOs nk ni mifano michache ya waliosumbuliwa (au walidanganya?)
 
Uko sahihi Boss...nyumbani ni nyumbani tu. Ughaibuni kuzuri sana, ila asikudanganye mtu nyumba ni mwisho wa reli...utapakumbuka tu na siku zote utatamani nyumbani pawe bora zaidi.
 
Kuwa na Uraia pacha ni Uoga , Wapigaji akipiga Bongo akimbilie Marekani , utamfanya nini wakati yeye ni Mu USA !

Mleta maada pengine hoja zako juu ya Mjadara huu wa Uraia pacha ina mashiko sana, but Why ? Hoja yako inakosa supportive facts

Umeeleza vyema ya kwamba huo uraia Pacha hautolewi na nchi Mama(Inchi ulozaliwa) bali hutolewa na hiyo inchi ya pili , kwani wewe apo kama tayari unakigezo cha kuwa Raia wa china, Germany, Uk etc kwa nini uhangaike na inchi ambayo uraia wake tayari unao ?

Kwani Mnataka Kusema kwamba Mpaka leo hii hamna Watanzania ambao either wapo Tz au inje ya Tz ambao wana uraia zaidi ya huo utz? Naamini jibu ni kwamba Wapo na wanafanya shughuri zao vyema bika bughuza.

Na kama wapotayari wenye huo urai na mambo yao yanaendaaa, why kelele nyingi mpaka kudemandi hili liwepo kisheria ? What is behind of those Legal demands
 
Sijui watanzania tunakosa exposure au sera ya Ujamaa imetukaa sana
 

Mkuu, umeona mbali sana.. Naunga mkono hoja kwa asilimia zote. Hili swala la uraia pacha ni muhimu, tunaomba Mulamula alipokee na alifanyie kazi. Mungu asaidie, na Amuongoze Mulamula katika majukumu yake, pamoja na Raisi wetu mama samia suluhu hassan.


Ahsante kiongozi wangu Synthesizer Mungu awe nawe!
 
Ndio maana hii nchi haiendelei, Roho mbaya na wivu ni laana Kubwa sana, ukiwaangalia usoni, ukiwasikiliza ni umasikini mtupu umejaa
Tuonyesheni vya maana mlivyofanya huko mlipo wehu nyie, mabox yakubeba yameisha mnataka kurudi
 
Naanza kuelewa - kwamba uraia pacha uwe wa kiubaguzi fulani hivi yaani Mtanzania aliyepoteza utanzania wake kwa kuukana alipotaka kufanikiwa akiwa nje ya Tanzania, aruhusiwe ku-reclaim uraia wake wa awali bila kupoteza uraia wake wa nchi ya pili; na iwe kwa kesi hizo tu na si vinginevyo.
Pili tusichanganye diaspora na uraia pacha maana diaspora kusaidia ndugu zake hakulazimishi mpaka awe na uraia pacha, au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…