Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Huyu Pasco anajifanya chizi.
 

Mahakama ambazo MAJAJI NA MAHAKIMU wake wanachukua form za kugombea uongozi kupitia tiketi ya CCM pale wanapostaafu.

Refer Jaji Augostino Ramadhani na kuchukua form za kugombea kupitishwa ili awe mgombea wa CCM
 
Maneno mazito sana haya ,nadhani hili ulilosema hapa halikua kwenye agenda ya kamati kuu ,wengi wetu tuna hasira kweli ila pia tujizuie na kutafakari kabla ya kusema ama kuandika jambo
 

Mkuu nyeusi ni nyeusi tu haiwezi kuonekana ni nyeupe hata siku moja ,unashauri watu waende Mahakamani huko huko unaposema kwa sasa pako chini ya boss anaeamua liwe na likawa..Mbona unajichanganya Mkuu.?.Hivi haki kwa vyama vya siasa kufanya siasa namna isiyopingaa na Katiba ni ya kuiombea tafsiri Mahakamani ?...
 
Chadema mbele kwa mbele dar arush mbeya tanga moshi shinyanga mwanza kagera geita wako tayar tunasonga mbele
 
Mkuu mada mezani ni kuwashauri CHADEMA mbona umekomalia urais wa dikteta wako na madaraka yanayomzidi kimo.
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Tusidharau Watanzania wanachoweza kukifanya!, Jamani tuheshimu sheria, kama Sheria zinaruhusu kufanyika kwa mikutano ya kisiasa basi haina budi kuheshimiwa.

Haina maana kuvunja nyumba zilizo katika hifadhi za barabara kwa kisingizio cha kufuata sheria lakini wakati huohuo hutaki kuiheshimu sheria inayosema kuwa vyama vya siasa vina haki ya kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima.

Tunapoapa kulinda katiba huku umeshika biblia au qur'an huku ukisema " eh Mwenyezi Mungu nisaidie" basi yapasa uwe mkweli wa nia na matendo!
 
Pasco wewe mwenyewe umekiri kwa maandishi yako kweli huyu Raisi dikteta kama unalitambua hilo kunyamaza kimya kunaweza kumpa nguvu kuendelea kuzidisha huo udikteta lazima zikafanyika juhudi za kupinga huo udikteta kwa nguvu zote zinaweza kuzaa mafanikio kiasi kikubwa sana.
Jana Chadema wametoa msimamo kupitia Naibu Katibu Mkuu Salimu Mwalimu maandamano yatafanyika kama yalivyopangwa na maandalizi nchi nzima yanaendelea . Maandamano yatafanyika kama yalivyopangwa
 
Shikamoo brother.. Hongera kwa kuandika nondo hiyo[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji111] [emoji111] [emoji111] [emoji111]
 
Kamanda nakushauri ukiondoka nyumbani acha kabisa umeandika wosia kuna uwezekano usirudi au ukarudi miguu imevunjika. Huyu siyo JK huyu ni Magu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Pasco kuna tofauti kati ya kuandamana na kufanya mikutano. CHADEMA wamedhamiria kufamya mikutano na sio kuandamana!
Mkuu wewe mwenyewe ulimsikia Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Mbowe kwa masikio yako, au ulifanya ulihadithiwa tuu kuwa Mbowe kasema hiki na kile?!, kwa sababu kuna watu wana masikio lakini hawasikii, na kuna watu wana macho lakini hawaoni!.

Sasa kwa kukusaidia wewe na wengine ambao hamkubahatika kumsikia Mwenyekiti wa Chadema, alisema nini, nakuwekea video yake uiangalie na kumsikiliza kwa makini alisema nini, pia nakuwekea na clip ya mwenyenchi mwenyewe, amesema nini, na ni hii clip mkuu wa nchi, ndio imepelekea kunifanya mimi kuutoa ushauri huu kwa Chadema, cho chonde msiandamane, this man mean business!, he mean what he says and will practice what he preach!.

Pasco
 
Hivi tukiangalia hizi clip mbili alizoweka hapa Pasco, halafu tukawa wakweli kabisa na tukamuogopa Mungu kwa kusimama upande wa haki....ni nani kati yao anaitetea katiba ya nchi hii? Ni nani kati yao kwa dhati kabisa anataka wananchi watendewe haki?

Mababa na mababu zetu walisimama kidete kupinga kunyanyaswa na kudhulumiwa, japo hawakukosekana vibaraka walioshirikiana na wakoloni. Ndiyo kusema leo hii kuna hekima mpya imezuka ya kukubali na kuhalalisha watu kufanyiwa dhuluma na kubaguliwa na jamii yote kutakiwa kukaa kimya?!
 

Kati ya kauli ya mdomo na kauli ya maandishi ipi ina uzito?
 
Kwa mujibu wa hizo clips, mtetezi wa kweli wa katiba ni Mhe. Mbowe, anachofanya Rais Magufuli ni udikiteta tuu per se!, huu udikiteta Magufuli hakuuanza leo, tangu ameanza huu udikiteta, Chadema wamo kwenye chombo cha kumdhibiti, Bunge, badala ya kulitumia bunge ambacho ni chombo rasmi kumdhibiti rais, wenzetu walikuwa wanaenda na kutoka bila kuchangia chochote, mara wanaweka plasta midomoni na vituko hivi na vile, kimya chao, kimemfanya Magufuli kuiweka pembeni katiba, na kutawala kwa kauli na matamko na siku zote wamenyamaza!, japo katiba inaruhusu maandamano, lakini mwenye nchi amesema hataki maandamano, ushauri wangu ni watu wasiandamane, mwenye nguvu mpishe, huyu jamaa yuko serious kweli, wakiandamana, atawatandika kweli!.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…